Baraza la Taifa la Katiba Tanzania linahitajika haraka sana !!!!??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Taifa la Katiba Tanzania linahitajika haraka sana !!!!???

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MPadmire, Jan 18, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Tanzania inaelekea siko?

  Kama kungekuwa na Baraza la Taifa la Katiba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) isingekuwa ovyo!!!

  Baraza la Taifa la Katiba linatakiwa liwe na wajumbe wasiofungamana na chama chochote cha siasa.

  Baraza la Taifa la Katiba linakuwa ndo Boss wa NEC.

  Baraza la Taifa linaweza kuundwa na wajumbe kutoka chama cha wafanyakazi, Chama cha wakulima, chama cha wafanyabiashara, mjumbe kutoka vyombo vya ulinzi, Wajumbe kutoka taasisi za elimu,wanaharakati wa haki za Binadamu, gender na wengine useme.....

  Kwa sasa hivi inatakiwa Kwanza kuundwa Baraza la Taifa la Katiba, baada ya hapo tuendelee na mchakato wa kuandika katiba mpya.

  Kazi za Baraza la Taifa la Katiba ni:-
  -Kuvunja Tume ya Taifa ya uchaguzi na kuunda tume ya muda
  -kuteuwa wajumbe wachunguze mapungufu ya uchaguzi wa 2010, ili kuondoa manung'uniko mioyoni mwa watanzania.
  -Kuchunguza masuala yanayosemwa kuhusu udini na kutoa Tamko
  -Kuunda tume ya ukweli na maridhiano - kuwaambia mafisadi warudishe hela zetu, wabakishiwe kidogo na wasamehewa.
  -Kuondoa inflation za bei kwa serikali kutoa ruzuku katika huduma muhimu za jamii kama umeme, sukari,mafuta ya kupikia, gas, fuel, ili kupunguza mfumuko wa bei.

  Ewe Dr Slaa, Ewe Prof. Lipumba, Ewe TLP, Ewe NCCR, Ewe CCM - kama mnaitakia Tanzania Mema, anzeni mchakato sasa.

  Natumaini ushauri wangu utapokelewa na kufikishwa katika ngazi husika
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Taratibu jamani!
   
 3. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Tanzania tuna Bunge la Congress na Je Tuna Senate???
   
 4. M

  Mwadada Senior Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wazo zuri! Nadhani laweza saidia taifa likizingatiwa kwa makini. Inapaswa kuwa wazi wajumbe watapatikana vipi.je kwakuchaguliwa vipi? Kuteuliwa nanani? Na vigezo vingine muhimu.
   
 5. w

  waluwalu Member

  #5
  Sep 19, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama watashirikiana kwa nia moja, nguvu moja,sauti moja,bila kujali itikadi zao na kutanguliza uzarendo na mapenzi ya nchi hii kwakweli litafanikiwa kwa asilimia miamoja
   
 6. M

  Mr. Chi Member

  #6
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pengine inawezekana kuna wazo zuri katika hili unalojaribu kuzungumzia, lakini nitofautiane na wewe katika moja ya mapendekezo yako: Haiwezekani na ninarudia tene kwamba haiwezekani kumpata mtu asiyefungamana na chama chochote (Difficult to find someone who is purely ideological free).
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Baraza hili linahitajika kama tangu mwaka majuzi vile; swala la kitiba tumechelewa sana.
   
 8. w

  waluwalu Member

  #8
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama kichwa cha habari kinavyo jieleza na kama nilivyokwisha changia mada hii,ningependa kuongeza mambo machache kuhusu njia zitumikazo kukusanya taarifa au kero zitolewazo na wananchi.Nitajitaidi kukumbuka machache ambayo muheshimiwa rais J K KIKWETE aliyazungumzia wakati wa mchakato wa katiba mpya,alisema ataakikisha katiba inatengenezwa kutokana na kero za wananchi na wawakilishi watawekwa kuusanya kero,maoni,na vipengere vinavyo hitaji marekebisho katika katiba iliyopo,na watakua katika ngazi mbali mbali na kwakila raia atapata muda wa kutoa mchangowake katika marekebisho ya katiba.
   
 9. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  kama hayo maoni hapo juu yangechukuliwa, sasa tanzania tungekuwa mbali. Tatizo watawala wametia pamba masikioni
   
 10. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Matendo ya police kama akina Zuberi ni matokeo ya Serikali kutowajibika kwa wananchi. Kungekuwa na baraza la kitaifa la katiba, nchi ingenyooka.

  Sasa hivi uchumi umeyumba na demokrasia inakandamizwa, kwa sababu kuna watu wanafikiri hii nchi ni yao na wanaweza kufanya lolote.

  Kwanza mchakato wa Katiba mpya kabla haujaanza, inatakiwa iundwe baraza la katiba ambalo ndo litatoa hadidu rejea za katiba mpya.

  Baraza la katiba lifute tume huru ya uchaguzi ambayo itasimamia chaguzi zote ndogo ili tuepuke upuuzi kama wa Igunga.

  Jamani nashangaa wanaharakati wa Tanzania LHLC na wengine, wanafanya nini? Wakajifunze kwa wenzao wa Malawi
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wananchi huenda wakalazimika kuishangaza serikali kwa kutokuambilika kitu chochote tofauti na 'katika ya wananchi' kwa njia ya kuundwa kwa baraza la katiba (si la rais) la taifa kuratibu kila kitu bila ya kubughudhiwa kitu.
   
Loading...