Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limezuia matokeo ya mitihani ya utabibu ngazi ya stashahada baada ya kuvuja

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limezuia matokeo ya mitihani ya utabibu ngazi ya stashahada ikisubiri uchunguzi unaofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto kutokana na kuvuja kwa mitihani hiyo.

Vyanzo vya taarifa vinadai mitihani hiyo iliyofanywa kati ya Agosti 12 na Septemba 11 katika vyuo 147 nchini, ilivuja kwa baadhi ya vyuo kuinunua hadi kwa Sh30 milioni.

Taarifa zinadai mitihani hiyo ilivuja kupitia mamlaka zilizopo chini ya Wizara ya Afya na zikishirikiana na baadhi ya vyuo kisha wanafunzi kutumiana mitihani hiyo pamoja na mwongozo wa usahihishaji katika mitandao ya kijamii hasa Telegram na Whatsapp.

Kugundulika kwa jambo hilo kumetokana na kuchelewa kwa matokeo hayo na wazazi wanapoulizia katika vyuo wanavyosoma watoto wao, wanajibiwa kuwa yamezuiwa na wizara kutokana na kuvuja.

“Taratibu za mitihani zinasema mtihani uki leak (ukivuja) unazuiwa na unatoa mitihani mingine na wahusika waliovujisha au kufanya udanganyifu wanatafutwa. Mpaka sasa hatujasikia lolote,” kilidai chanzo chetu.

Oktoba 15, Wizara ya Afya iliwaandikia barua wakuu wote wa vyuo vyenye zaidi ya wanafunzi 4,000 ikieleza imepokea barua kutoka Nacte ikieleza matokeo yote ya wanafunzi wa clinical medicine (uganga) yamazuiwa.

Barua hiyo ya Nacte iliyoandikwa Oktoba 12, ina kumbukumbu CA.64/170/01B/7 inayohusu kutolewa kwa matokeo ya awali (provisional results) ya mitihani iliyofanyika kitaifa Agosti katika vyuo vyote vya kati vya afya.

“Baraza linapenda kuwafahamisha kuwa matokeo yote ya wanafunzi wa ngazi ya NTA level 5, program ya utabibu yamezuiwa mpaka taarifa ya uchunguzi kutoka Wizara ya Afya itakapokamilisha na kuwasilishwa Nacte kwa ajili ya maamuzi,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo imeeleza kuwa “matokeo ya wanafunzi 35 kutoka vyuo mbalimbali yamefutwa na wanafunzi hao kusimamishwa kuendelea na masomo (discontinued) kutokana na kufanya udanganyifu kwenye mitihani.

Lakini Oktoba 15, Katibu wa Afya na Mkufunzi wa Taasisi ya Center for Educational Development in Health (CEDHA), Joel Masaule naye aliwatumia barua hiyo wakuu wa vyuo vya afya kanda ya kaskazini vilivyo chini ya Wizara ya Afya.

Mkuu wa Chuo cha Afya Tanga, Dk Kweka Luchari alikataa kuthibitisha au kukanusha kupokea barua hiyo ya Nacte lakini akasema kwa ufupi tu “sehemu sahihi ya kuulizia hilo jambo ni Nacte. Watafute Nacte wenyewe.”

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Nacte, Dk Adolf Rutayunga alipoulizwa jana alisema suala hilo ni la Wizara ya Afya na wao hawafahamu uchunguzi unaofanywa hivyo kama kuna ufafanuzi unaohitajika basi waulizwe wizara.

Mwananchi
 
Wafute yote udanganyifu kotekote kwenye hiyo mitihani,hao ni mbuzi wa kafara
 
Back
Top Bottom