Baraza la mtihani Tanzania (NECTA) hapa mmenichanganya

chaliko

Senior Member
Apr 1, 2019
180
802
Habari ndugu zangu wa Jf,

Leo katika kuperuzi kwangu mitandaoni nikaona ngoja nipitie na Website ya NECTA ili na mimi niwe na taarifa za motomoto kutoka huko. Nilifanikiwa kuperuzi hapa na pale na pia kupata maarifa kidogo.

Pia nikaona ngoja nisome kwa mara nyingine VISION na MISSION ya BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA ili nizidi kupata na kujiongezea maarifa.

Baadae nikaona niangalie kwa umakini NEMBO (LOGO) ya BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA, hapa naomba niseme wazi kuwa tangu nimeanza kulifahamu BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA sijawahi kuangalia NEMBO (LOGO) yao kwa umakini.

Lahaula! baada ya kuangalia nimekutana na vitu vinne;

1. Jembe

2. Nyundo

3. Chepe

4. Kitabu

Binafsi nilidhani hii NEMBO / LOGO ingefaa iwe ya WIZARA YA ELIMU NA ikimaanisha Namna ambavyo unaweza kutumia ujuzi uliopata Darasani katika kutatua changamoto za maisha yetu ya kila siku. NECTA wao wangebaki na hicho Kitabu peke yake.


Hivi vitu vya kwenye LOGO / NEMBO vimenifanya nije hapa nikiamini JF ni kisima cha MAARIFA.


Nauliza hivi ndugu zangu,

1. Jembe

2. Nyundo

3. Chepe

Kwenye LOGO / NEMBO ya NECTA vinamaanisha nini?
necta image.jpg
 
Bora hiyo.. Mimi matokeo ya kidato cha nne nilifeli lakini cha kushangaza niliwekea masomo ambayo nilikuwa siyasomi ambayo ni PHYSICS ( F) na CHEMISTRY (D) alafu sikuwekewa somo la FINE ART ambalo nilifanya mtiani wake

Wakati matokeo yanatoka ni mtu aliniangalizia hivyo kutokana na presha ya kufeli sikuweza kuligundua hilo kwa haraka.....

ila ndio ivo sikuwa na la kufanya
 
chaliko, Unaposema kitabu peke yake unamaanisha Nini? Kwani ndani ya vitabu Kuna maarifa gani, mm binafsi sijaona tatizo lolote hapo kwani vitabu vinatoa maarifa ya kazi
Baraza la mitihani linasimamia mitihani ya shule za msingi , sekondari ,vyuo vya ufundi na vyuo vya ualimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana yake Ni kua rukaruka wee lakini ukimaliza chuo...izo chepe..jembe na nyundo ndo vitakupa msosi...they mean makhirikhiri tools for self reliance
 
mtoa post upo sahihi... wanaodai nembo ipo sahii basi wangeweka na mtumbwi kwa ajili ya uvuvi etc...
NB. nembo ya baraza la mtihani la taifa ilibidi iwe pen na kitabu tu basi.
 
Back
Top Bottom