Baraza la mitihani, wizara ya elimu na hatima ya wahitimu waliositishiwa matokeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la mitihani, wizara ya elimu na hatima ya wahitimu waliositishiwa matokeo

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Hume, Sep 3, 2008.

 1. H

  Hume JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Natatizwa na kasi ya utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayojitokeza katika kipindi hiki cha utawala,

  Leo nahitaji tujadili na kuangalia mustakabali mzima wa wahitimu katika vyuo vya ualimu ambao matokeo yao hayakutolewa mnamo mwezi wa saba, na hasa chuo cha Kange ambacho walisitisha kutangaza matokeo ya chuo kizima.

  Shida moja kubwa ni kuwa kuna wahitimu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2006, ambao inamaanisha walichelewa kujiunga na vyuo kwani wakati wenzao walianza chuo july 2006 wao walichelewa na kujiunga na vyuo hivyo mnamo february 2007 baada ya matokeo yao ya mtihani wa kidato cha nne walioufanya november 2006 kutoka. Tatizo wanaloliona wao baraza ni kuwa vijana hawa hawakutimiza miaka miwili ya kuwa chuoni, suala ambalo haliingii akilini kwani serikali hiyo hiyo iliwahi kuruhusu kozi za mwaka mmoja, na hata miezi kadhaa kwa vijana wa form six ili wakafundishe sekondari.

  Baraza lilitoa namba za mitihani kwa watu hao baada ya kutimiza vigezo, licha ya vyeti vyao vya kidato cha nne kuonyesha wazi walimaliza lini; hata kabla ya namba kutolewa walitumwa wakaguzi kutoka Moshi kwenda chuo cha Kange ambao walifanya kazi yao na cha kujiuliza hiyo report ilipelekwa wapi?

  Na suala la kufoji vyeti, hivi inawezekana kweli kuwa chuo kizima wakafoji vyeti? Kwa nini kuendelea kuumiza waliomo na wasiokuwemo?
  Kwa nini wanaendelea kuwatesa kisaikolojia?

  Walio makazini mpaka sasa wanaendelea kufanya kazi bila amani kwani hawajui hatima yao, wataendelea kufanya kazi bila matokeo hadi lini?
  Na kwa wale ambao wameshindwa kuripoti baada ya hali hii kujitokeza, serikali itawalipa fidia itakapogundulika hana hatia na bado amepewa adhabu ya kutofanya kazi kwa kipindi chote hicho?

  Kwa nini serikali isiwaruhusu kuendelea na kazi na wapate haki zote wakati uchunguzi unaendelea? na ni uchunguzi gani huo usio na mwisho?
   
Loading...