Zamazangu
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 827
- 465
Kumekuwa na tatizo jipya la wasimamizi wa mitihani ya taifa ambao ni walimu kukopwa posho zao za usimamizi wa mitihani hiyo ya taifa kidato cha Pili na cha Nne. Utaratibu huo umefanyika kwa miaka miwili mfululizo kwa baadhi ya Halmashairi hapa nchini.
Mwaka 2015 malipo yalifanywa kwa 75% na hiyo 25% ikabaki na haijalipwa mpaka Leo. Mwaka 2016 tatizo hilohilo limejirudia kwa usimamizi wa kidato cha Pili wasimamizi wamekopwa kwa takribani 50%. Mambo haya yanadhoofisha sana utendaji na ufanisi wa mwalimu.
JE NI KWELI BARAZA HALINA PESA ZA KULIPA NA KWANINI HATA TAARIFA ZOZOTE HAZITOLEWI.
Tunaomba kama ninyi wenye mamlaka kubwa mnayajali muwajali pia walimu. Kwani kumbukeni kuwa wote mmepita mikononi mwa Mwalimu.
Naomba kuwasilisha wana JF