Baraza la Mitihani kuwafanyisha tena mitihani kidato cha kwanza watakaofeli kutoswa

Unafahamu kwa nini wanafanya mchujo mwingine? Lazima wameona kuna makosa/kasoro
kasoro ni idadi kubwa ya wanafunzi wanaohitaji pesa za elimu bure. walitaka sifa za kua wamefaulisha na wamewachagua wote, sasa wameshindwa kuwahudumia ktk elimu bure.
hii elimu bure kama imewashinda, waifute wawape watanzania wengi fursa za kusoma. kuna wengine hawakujifunza vyema shule za msingi kwa sababu nyingi ikiwemo utoto, ila wakiingia elimu ya vidato wakajitambua wanabadilika sana.
 
Serikali iende study tour private schools zinazofanya vizuri kujua wanatumia mbinu gani! Juzi kati hapa walitaka "kuwaingilia" eti kutaka kuwapangia ada. Wakome! Waboreshe zao automatically wazazi watapeleka watoto huko.
nimeipenda sana. wajiulize hivi kwanini ukienda dukani unakuta mchele wa aina tofauti na wenye bei tofauti, ila mchele wa aina zote unapata wateja?
 
Sioni tatizo hapo, kama umefaulu kwa merit hata ukifanya mtihani mwingine utapita tu. Hapo lazima kuna harufu ya kupitisha wasiostahili i.e failures ambao hawataweza mikiki mikiki ya sekondari. Kama wizara wameliona hilo big up, tunataka watoto vipanga waje kuliendeleza hili taifa.

Vile vile tuanze sasa kuwasaidia hata wale ambao hawawezi kusoma sekondari waende moja kwa moja kwenye kozi mbali mbali ambazo wanaonyesha uwezo/vipaji kuzifanya.
Ni kazi bure, kama mtihani unaratibiwa na hao hao NECTA waliopitisha hao makapi, bila shaka ni upotezaji wa muda. Mfumo wa utahini kwa shule za msingi ni mbovu.
 
Naona umetoa mawazo yako kwa kuchanganya sana, sio kila mwanafunzi anayeenda shule ya kata analazimishwa na mfumo. Ukijaribu kuangalia wengi wa wanafunzi wanaoenda shule za kata ni kutokana na uwezo wa wazazi wao kifedha. Na mzazi kuwa na uwezo mdogo wa kifedha haumaanishi kwamba mtoto wake ana uwezo mdogo wa kielemu. Tofauti kubwa ya shule za kata na shule za private ni idadi ya wanafunzi kwa darasa na uwezo wa waaalimu kuwahudumia katika darasa. Katika shule za private waalimu wanabanwa na mwajiri kiasi kwamba wanafanya kazi iliyowapeleka na wote huwa wanatakiwa kutoa feedback ya wanafunzi wake mara kwa mara bila kusahau motisha kwa wanafunzi hao. Huko shule za umma/kata wanafunzi wanajaa darasani kama sokoni, walimu wana uwezo mdogo na wengi wanafanya kazi hiyo kama sehemu ya kuvutia muda kwani hawana motisha yoyote na hakuna anayejali ubora wa kile anachofundisha. Matokeoa ya kutokufundishwa vya kutosha na kuwa na kazi nyingi shuleni unakuta wanafunzi wanageuza shule kama eneo la rasmi la uzururaji na hapo ndio wanafunzi wanafundishana tabia zilizo nje ya maadili.
mawazo yako mengi ni mazuri na yakujenga. ila hapo kwenye red, huo uwezo mdogo wa mwalimu ni wa kifedha?
 
Hii nihasara sana kwa wazazi maisha yenyewe ni siri ya mtu yani unakuta mzazi kajitutumua mpaka basi mbaya zaid mpaka leo wengine bado hawaja report mpaka leo unakuta mzazi hana hela yakumtekelezea mtt mahitaji leo hii mnasema watoto wanachujwa tena
Daaah bora elimu ingekuwa kama mwanzo tu kila mtoto alipie hii yote inatokana na kukurupuka kusema elimu bora ss yamewashinda mnaanza kuleta sababu mngesema toka mwanzo wanafunzi wote kabla hamjaanza masomo yenu tuwahakiki kwanza
 
Katika taasisi za serikali zote Nina iyamino necta ila kwa hili wanajikosoa wenyewe kuwa awajui kazi yao .Bora wangesema kama mwaka 2012 na 2013 walikuwa wanapima kusoma kuandika na kuhesabu .mwaka huu wanafanya ujinga
 
Mi nasubir utekelezaji, ila kama kuna hali ya siasa hamna litakalofanikiwa
Sioni tatizo hapo, kama umefaulu kwa merit hata ukifanya mtihani mwingine utapita tu. Hapo lazima kuna harufu ya kupitisha wasiostahili i.e failures ambao hawataweza mikiki mikiki ya sekondari. Kama wizara wameliona hilo big up, tunataka watoto vipanga waje kuliendeleza hili taifa.

Vile vile tuanze sasa kuwasaidia hata wale ambao hawawezi kusoma sekondari waende moja kwa moja kwenye kozi mbali mbali ambazo wanaonyesha uwezo/vipaji kuzifanya.
 
labda wangesema wale waliofaulu sana la saba,wapewe full sponsorship ya secondary wengine wajitegemee,yaani ibaki kama ilivyo sasa,hamna mtihani wa kufanya tena,sema waliofaulu sana wasomeshwe.
 
Mama Ndalichako,

ondoa huu upuuzi,

hii move itawaumiza watoto wa maskini,

since wazazi wenye uwezo huwapeleka watoto wao shule za private,

mara nyingi shule za serikali hujaa wanafunzi ambao wazazi wao wana kipato cha chini,ama cha kati,

sasa wazazi wenye uwezo watawapeleka watoto wao shule za private,wakifeli huu mtihano.

sijui watoto wa maskini wataenda wapi?

THINK AGAIN PLEASE.
 
Bora wafanye tu, maana kama mtoto kafaulu hata jina lake hawezi kuandika nini kifanyike sasa.Shule zimejaa mambumbumbu halafu mtu anadai walimu wanafelisha! Mfumo mbovu wasiasa kwenye elimu ndiyo matokeo yake kujaza mazero tu.
 
Ukisema kupima usahihi unamaanisha Mara ya kwanza mpimaji hakuwa sahihi.
Kuna tatizo kwenye mfumo huku sio bure
 
Mama Ndalichako,

ondoa huu upuuzi,
yeye ndiye kaagiza hili swala, kutokana na ukata wa pesa za elimu bure. sasa unataka atengue utaratibu aliouweka tena kwasababu fulani!!! kwani wanyonge wanamuhusu? kila mtu abebe msalaba wake. au umesahau ule utaratibu alioagiza kufuatwa wa kuwapa wanafuzi wa elimu ya juu mikopo ya shilingi mia tatu (Tsh300) na kuwanyima wengi pia?

hayo yote ya kuwaumiza wanyonge anayapokea kwa mikono miwili kutoka juu. wajuu wanamuagiza afanye hivyo kutokana na ukata wa pesa uliopo!!!
 
Bora wafanye tu, maana kama mtoto kafaulu hata jina lake hawezi kuandika nini kifanyike sasa.Shule zimejaa mambumbumbu halafu mtu anadai walimu wanafelisha! Mfumo mbovu wasiasa kwenye elimu ndiyo matokeo yake kujaza mazero tu.
tulitaka sifa. watu watusifu kua tumefaulisha wote. sasa tumekosa pesa za kuwahudumia ktk elimu bure.
sasa unataka wafute ili iweje? mtihani waandae wao, wasimamie wao, wahihishe wao, wapange matokeo wao na wao ndio wamewaongezea maksi wanafunzi ili waufulu wote; sasa leo unataka wafanye nini?
kama hakuna ajenda ya ukata wa pesa, wawaache watawachuja kidato cha pili!!!
 
Ukisema kupima usahihi unamaanisha Mara ya kwanza mpimaji hakuwa sahihi.
Kuna tatizo kwenye mfumo huku sio bure
kwa kusema kupima usahihi kwa mwaka huu, wanamaanisha miaka mingine kulikua na usahihi, ila mwaka huu wameona kuna mashaka ktk usahihi hivyo wanataka waupime.
mimi naona upimaji wa mwaka jana ulikua sawa na wa miaka mingine na pote kulikua hakuna usahihi ndio maana waliruhusu hadi wasiojua kosoma na kuandika wakafaulu. ila kuzuka kwa kupima usahihi kwa mwaka huu ni kwasababu ya ukata wa pesa za elimu bure.
walitaka sifa za kufaulisha wote kwa kuandaa mtihani mibovo na kuwaongezea maks wanafunzi, leo wameshindwa kuwahudumia.
MIMI NAONA USAHIHI HUO WAUPIME KIDATO CHA PILI.
 
APA wako sahihi BT at a wanaoingia form five mwaka 2017 bac wapge pepa tena me najua kuna impurities nyng xna mama yetu ndarichako Fanya kaz tena Fanya kwa moyo wako wrote tunakuombea afya njema ikiwezeka chukua dvn one only mwaka huu wengne tukutane nao shambani
 
Back
Top Bottom