Baraza la Mitihani kuwafanyisha tena mitihani kidato cha kwanza watakaofeli kutoswa

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,842
Baraza la Mitihani.jpg
 
Hapo ndio utashangaa mikurupuko juu ya mihemko!!! Wametoa mitihani form 2 leo wanawachuja wa form 1.....utaelewa maana yak nini?? Watoto wamekaa zaidi miezi 4 wameanza kusahau mambo ya primary.....wafanye paper za primary mwezi 2 huu wakiwa secondary,,,,,,,,,,,,mihemko kazini!!!
 
elimu bure imeshafeli tayari..sisi tulioko huko kwenye elimu tunajua namna gani hali ilivyo mbaya

kingine naunga mkono maana hawa wanafunzi waform one kuna wengine hata kuandika shida yaani vurugu tupu,concept za mathematics za primary zinawashinda yaani its a huge crisis...

wanafunzi hawa wa maksi100 out of 250 kwa kweli ni shida unafundisha mpk unatamani kulia ...

Ila swali kwa nini wawape mtihani sasa hivi wakati walishafanya mitihani ya Taifa?
au ndo sinema za bure za kutaka kujitetea baadae kwa wananchi kua waliochaguliwa hawakua na sifa?

Kwa nini msingewaondoa mwanzo?mzazi ameshagharamika uniform,madaftari nk kwelii?
 
Sioni tatizo hapo, kama umefaulu kwa merit hata ukifanya mtihani mwingine utapita tu. Hapo lazima kuna harufu ya kupitisha wasiostahili i.e failures ambao hawataweza mikiki mikiki ya sekondari. Kama wizara wameliona hilo big up, tunataka watoto vipanga waje kuliendeleza hili taifa.

Vile vile tuanze sasa kuwasaidia hata wale ambao hawawezi kusoma sekondari waende moja kwa moja kwenye kozi mbali mbali ambazo wanaonyesha uwezo/vipaji kuzifanya.
 
Wangebadili mfumo wa kutahini shule za msingi. Mtoto anafaulu kwa ku shade majibu. Hivyo hata mahamuma wanafaulu. Hivyo kuwachuja mara ya pili inadhihirisha umbilikimo wa fikra za alietahini mwanzo.
 
AIBUUUUUU! UnaMCHUJA Mtu ambaye HUJAMFUNDISHA? Hapa wazazi wanaoshtakiwa kwa KUWAZUIA watoto wao wasiende Sekondari (Licha ya Kufaulu), watapata sababu. Watawaambia watoto wao: FELINI Mjirudiage nyumbani.... Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi..
 
Hakuna mtaala wenyetija ndomana mazingaumbwe hayaishi kwenye shule za serikali. Hapo watasema shule zinataka wanafunzi wengi ili zipewe pesa nyingi toka serikalini!!
Kuna viongozi wao huwaza kupunguza gharama tuuu badala ya kuwaza kuzalisha zaidi na ziada.
 
Back
Top Bottom