Baraza la Mitihani: Fukuza fukuza bila utaratibu hadi Ajira bila utaratibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Mitihani: Fukuza fukuza bila utaratibu hadi Ajira bila utaratibu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fikramakini, Sep 25, 2012.

 1. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kipindi kirefu sasa kumekua na kashfa mbalimbali ambazo zimelikumba Baraza la Mitihani la Tanzania. Kupitia vyombo vya habari tumesoma taarifa ya wizi/upotevu wav yeti na hata results slip ndani ya majengo ya taasisi hiyo. Pia tumeshuhudia uvujaji mkubwa sana wa mitihani ulio husisha taasisi hiyo ambao ulipelekea baadhi ya wafanyakazi kuwajibishwa. Mwaka huu tumeshuhudia saga la waisilamu na taasisi hiyo nyeti.
  Kwa leo napenda tuangazie mwenendo wa ajira wa taasisi hii.

  Kipindi cha kama miaka mitatu iliyopita, wafanyakazi wa taasisi hiyo wamekua wakiachishwa kazi bila ya kufuata utaratibu. Taarifa ziliwahi kuvuja kwamba kuna wafanyakazi watatu wa baraza (Elizabeth Mtoka, Severe na Aloyce Atanasi) ambao wali achishwa kazi kiutata. Cha ajabu ni kwamba, mwanasheria wa Shirika alipotoa angalizo kwamba kuwafukuza wafanyakazi hao itakua ni kinyume cha utaratibu, kwa hasira katibu mtendaji akamtoa mwanasheria (Company Secretary) kutoka miongoni mwa management team.

  Kwa bahati mbaya, kwasababu mwanasheria huyo alikua bado kwenye “probation”, baada ya mwaka mmoja wa utumishi wake akaachishwa kazi kwa kisingizio cha utendaji wake kutoridhisha. Mwanasheria huyo (Stella) alifungua shauri katika mahakama ya kazi ambapo alishinda kwa kishindo na shirika kujikuta likimlipa fedha nyingi (takribani milioni sabini).

  Majuma machache baadae wale vijana watatu waliofukuzwa awali pia walishinda kesi na shirika likajikuta kuwalipa fedha nyingi pia.

  Kutokana na mwenendo wa wanaofukuzwa kazi kushinda kesi, basi ufukuzwaji holela wa wafanyakazi ukakoma. Inasemekana ili mtu afukuzwe kazi sasa ni lazima kwanza apate nafasi ya kuhojiwa na kamati ya ajira na nidhamu ya bodi.

  Habari zinaeleza kwamba sasa mwenendo umebadilika na kuwa wa kuajiri wafanyakazi wa upendeleo … upendeleo mkubwa. Wakati ajira zote zinatakiwa kupitia wizara ya utumishi, pale baraza la mitihani watu wanaajiriwa bila kufuata utaratibu. Imefikia mahali watu wanaajiriwa bila hata ya kazi yenyewe kutangazwa magazetini kama ilivyo kawaida.
  Habari mbaya zaidi nay a kusikitisha, imefikia mahali Katibu mtendaji Dr. Joyce Ndalichako amemwajiri mfanya kazi mmoja (Jerita) bila kutangaza kazi, na bila kufanya usaili wowote. Inasemekana kwamba huyu dada ni mpenzi (girl friend) wa mototo wa Dr. Ndalichako! Cha kusikitisha mno, huyu binti ambae ni fresh from school analipwa mshahara hata kuwapita wenye uzoefu mkubwa zaidi yake.

  Sasa katika kufunika hilo la Jerita, imebidi Dr. Ndalichako atafute wahitimu wengine kadhaa kutoka vyuo vikuu na mchakato unafanyika kuwaajiri bila ya kutangaza kazi (ili kuwe na ushindani) wala kushirikisha idara zinazo husika na ajira pale baraza. Inasemekana hakuna uhakika kama anafanya hivyo kufunika ajira ya mkwe mtarajiwa au hao vijana watakao ajiriwa pia ni ndugu.

  Kwa maoni yangu, nadhani huyo mama amelewa madaraka sasa anaanza kuvurunda. Serikali inahitaji kumwangalia kwa jicho la kumchunguza nap engine kumchukulia hatua madai haya kama ni ya kweli.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  Mmmmmmh,
   
Loading...