Jamani hili baraza la mawaziri linatangazwa lini? na Raisi anatakiwa kukaa muda gani kukamisha hii process ya kutangaza baraza lake?
nadhani baraza lake la mawaziri litakuwa na sura kama hii:
rais atafuta baadhi za wizara na zingine kuziunganisha na atakuwa na baraza dogo sana!!!!
1) waziri mkuu-
2) mambo ya nje na uhusiano wa EA-
3) fedha na uchumi-
4( sheria na katiba (mambo ya ndani kufutwa)-
5) ulinzi-
6) elimu-
7) kilimo, mifugo na uvuvi-
8) kazi na maendeleo ya jamii-
9) afya na mazingira-
10) ardhi, mawasiliano na miundo mbinu-
11) madini, mali asili na utalii
12) utamaduni,wanawake, na watoto
Wizara kama habari na michezo azifute na kila wizara iwe ina msemaji wake huku michezo ikisimamiwa na vilabu vyao.
Mambo ya ndani ifutwe na kazi zake zifanywe na wizara ya katiba na sheria.
Hakuna haja ya kuwa na mawaziri wadogo kazi zao zifanywe na makatibu wakuu na kwa hakika serikali itawajibika vilivyo na kupunguza gharama!!!
ombi langu kwa rais ni kuwa awajumuishe wapinzani ktk serikali yake ili kujenga umoja wa kitaifa na kwa kuanzia ampe Lipumba wizara ya fedha na uchumi huku dr. Slaa apewe wizara ya sheria na katiba!!!
mkuu mawazo yako mazuri lakini wizara ya mambo ya ndani haiwezi hata siku moja, hiyo ni sawa na kusema wizara ya fedha au mambo ya nje ifutwe
Tatizo liko kwenye kulipa fadhila ndo maana tunakuwa na WAHE she MIWA wengi!
Sasa nimeelewa kwa umakini:smile-big:Mpenzi kwa taarifa zilizopo iko hivi,wabunge wanakutana Dodoma kwaajili ya kufanya yafuatayo:kuapishwa,kuchagua spika na naibu wake,kupitisha majina ya wabunge wa viti maalum na kuunda kamati za bunge,kuchagua viongozi wa kambi ya upinzani bungeni na kupitisha jina la waziri mkuu.Kwa mujibu wa katibu wa bunge zoezi hilo litakuwa na la siku kama tatu hivi na itafanyika ndani ya mwezi huu ila tarehe nimesahau.
Hivyo basi,akishapatikana waziri mkuu;yeye ndiye atakayeshirikiana na rais kuunda baraza la mawaziri;sawa mpenzi kama kuna lolote la ziada tuwasiliane.