Baraza la mawaziri

Mpenzi

Member
Nov 3, 2009
49
0
Jamani hili baraza la mawaziri linatangazwa lini? na Raisi anatakiwa kukaa muda gani kukamisha hii process ya kutangaza baraza lake?
 
Jamani hili baraza la mawaziri linatangazwa lini? na Raisi anatakiwa kukaa muda gani kukamisha hii process ya kutangaza baraza lake?

nadhani baraza lake la mawaziri litakuwa na sura kama hii:
rais atafuta baadhi za wizara na zingine kuziunganisha na atakuwa na baraza dogo sana!!!!

1) waziri mkuu-
2) mambo ya nje na uhusiano wa EA-
3) fedha na uchumi-
4( sheria na katiba (mambo ya ndani kufutwa)-
5) ulinzi-
6) elimu-
7) kilimo, mifugo na uvuvi-
8) kazi na maendeleo ya jamii-
9) afya na mazingira-
10) ardhi, mawasiliano na miundo mbinu-
11) madini, mali asili na utalii
12) utamaduni,wanawake, na watoto

Wizara kama habari na michezo azifute na kila wizara iwe ina msemaji wake huku michezo ikisimamiwa na vilabu vyao.
Mambo ya ndani ifutwe na kazi zake zifanywe na wizara ya katiba na sheria.

Hakuna haja ya kuwa na mawaziri wadogo kazi zao zifanywe na makatibu wakuu na kwa hakika serikali itawajibika vilivyo na kupunguza gharama!!!

ombi langu kwa rais ni kuwa awajumuishe wapinzani ktk serikali yake ili kujenga umoja wa kitaifa na kwa kuanzia ampe Lipumba wizara ya fedha na uchumi huku dr. Slaa apewe wizara ya sheria na katiba!!!
 
Aisee mawazo yako mazuri na kiukweli baraza liwe dogo kama uliorodhesha lakini kumbuka akili na upeo uliokuwa nao wewe ni tofauti na za unayemshauri.
Kwa kuwa katiba inampa madaraka yakuamua na kuchagua mawaziri ndo hivyo atachagua wote toka CCM aka (Chaka Chua Matokeo).
 
kuwaingiza wapinzani BLM ni kuumaliza upinzani totally, kama mnbisha subirini CUF Zenj!
 
nadhani baraza lake la mawaziri litakuwa na sura kama hii:
rais atafuta baadhi za wizara na zingine kuziunganisha na atakuwa na baraza dogo sana!!!!

1) waziri mkuu-
2) mambo ya nje na uhusiano wa EA-
3) fedha na uchumi-
4( sheria na katiba (mambo ya ndani kufutwa)-
5) ulinzi-
6) elimu-
7) kilimo, mifugo na uvuvi-
8) kazi na maendeleo ya jamii-
9) afya na mazingira-
10) ardhi, mawasiliano na miundo mbinu-
11) madini, mali asili na utalii
12) utamaduni,wanawake, na watoto

Wizara kama habari na michezo azifute na kila wizara iwe ina msemaji wake huku michezo ikisimamiwa na vilabu vyao.
Mambo ya ndani ifutwe na kazi zake zifanywe na wizara ya katiba na sheria.

Hakuna haja ya kuwa na mawaziri wadogo kazi zao zifanywe na makatibu wakuu na kwa hakika serikali itawajibika vilivyo na kupunguza gharama!!!

ombi langu kwa rais ni kuwa awajumuishe wapinzani ktk serikali yake ili kujenga umoja wa kitaifa na kwa kuanzia ampe Lipumba wizara ya fedha na uchumi huku dr. Slaa apewe wizara ya sheria na katiba!!!

Mkuu mawazo yako mazuri lakini Wizara ya mambo ya ndani haiwezi hata siku moja, hiyo ni sawa na kusema wizara ya fedha au mambo ya nje ifutwe
 
mkuu mawazo yako mazuri lakini wizara ya mambo ya ndani haiwezi hata siku moja, hiyo ni sawa na kusema wizara ya fedha au mambo ya nje ifutwe

kama nimemuelewa alimaanisha wa merge mambo ya ndani na sheria soma maelezo yake vizuri
 
Kwa hali ilivyo siyo siri sina hamu hata ya kujua manake nahisi watakuwa ni walewale maswahiba walomchangia pesa za kampeni kama kipindi kile cha Lowasa na Karamagi!
 
Kwa picha hizi ktk link hiyo hapo chini, hakika huyu bwana aweza pewa uwaziri mkuu au hata wizara nyeti. Ni waziri machachari tumjuaye.

mjengwa
 
Safi kweli kweli, bali mawaziri wawe kama ifuatavyo.

1.PM - Lowassa
2.Finance - Mramba (ateuliwe mbunge toka zile nafasi kumi za JK)
3.Constitution - Chenge
4.Infrastucture - Karamagi
5.Foreign - Rostam
6.Tourism - Lau Masha
7.
8.
9.
10.
11.
12.
 
Mpenzi kwa taarifa zilizopo iko hivi,wabunge wanakutana Dodoma kwaajili ya kufanya yafuatayo:kuapishwa,kuchagua spika na naibu wake,kupitisha majina ya wabunge wa viti maalum na kuunda kamati za bunge,kuchagua viongozi wa kambi ya upinzani bungeni na kupitisha jina la waziri mkuu.Kwa mujibu wa katibu wa bunge zoezi hilo litakuwa na la siku kama tatu hivi na itafanyika ndani ya mwezi huu ila tarehe nimesahau.
Hivyo basi,akishapatikana waziri mkuu;yeye ndiye atakayeshirikiana na rais kuunda baraza la mawaziri;sawa mpenzi kama kuna lolote la ziada tuwasiliane.
 
Sasa nimeelewa kwa umakini:smile-big:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom