Baraza la Mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Mawaziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Heri, Jul 4, 2009.

 1. H

  Heri JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwa muda mrefu pamekuwa na mawazo kuwa baraza la mawaziri ni kubwa . Hii inatokana na katiba kumpa Rais uwezo wa kuamua kuwa na ukubwa gani wa baraza hilo.
  Ingekuwa vizuri, ikiwezekana (kabla ya 2010), bunge lipitishe muswada kuhusu ukubwa wa baraza hilo. Ioneshe ni wizara zipi ziwepo na ikiwezekana na muundo wa wizara hizo.
  Kwa upande moja hii itasaidia katika kupanga matumizi na ufanisi wa serikali.
   
 2. SOARES

  SOARES Member

  #2
  Jul 4, 2009
  Joined: Jul 6, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  He tuna mpaka "Wizara ya kitoweo" mmmh. tulishawahi pia kuwa na Waziri asiye kuwa na Wizara maalum, sijui ilikuwa na watumishi wangapi!!
   
 3. M

  Mong'oo Member

  #3
  Jul 4, 2009
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili tumuachie raisi mwenyewe. Idadi ya mawazi ukiangalia inategemea malengo na mikakati ya raisi.
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  katiba ndio iwe lengo sio hayo tu yanahitaji kubadilishwa kuna mambo mengi
   
 5. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Huu nadhani ndo upuuzi ambao watanzania tumekuwa tukiuendekeza.
  rais tunampa dhamana ya kuongoza nchi kwa niaba yetu ni vyema tukampa mipaka pia,Kutakuja tokea rais kichaa ataweka wizara mpaka ya kushughulikia mahouse girl kama hatutaliangalia kwa mapana.
  Ni busara sasa kumpunguzia rais baada ya mamlaka ili waweze kuwatumikia wananchi vyema madaraka aliyo nayo sasa hivi ni kwamba hashikiki,unauwezo wa kumpa kura na kumwingiza madarakani lakini kuna mizengwe ya kumwondoa anapo haribu.ndokwa maana viongozi wetu wana jeuri,kiburi kisichosemekana kwani ulimpa madaraka lakini huwezi kumwondoa anapo haribu.
  Kama tutaweka mipaka/idadi ya wizara itatupunguzia mizigo ya kuwabeba wastahafu kadha wanaopewa wizara zisizo na kazi maalumu"k.m waziri asiyekuwa na wizara" huyu mtu anakuwa mzigo kwa walipa kodi lakini kwa vile ni rafiki wa rais anamtafutia ulaji.
  Ni lini watanzania tutaamuka?
  Kwanza tulitakiwa kabla ya uteuzi wa mawaziri awataje wapitishwe na bunge japokuwa bunge lenyewe ndo hilo.Kwa kuwataja mapema siajabu baadhi ya wanaharakati waandishi na vyanzo mbalimbali vinaweza kusaidia
  kumweka wazi mtu kwani sisi tunao kaa nao tunawajua zaidi kuliko hata washauri wa rais.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,603
  Trophy Points: 280
  Nafikiria wizara ziwe fixed na ziunganishwe naona hata SA pia wana wizara nyingi sana sana....rais amepewa nguvu nyingi sana apunguziwe maana analipa fadhila tu hakuna lingine....anajaza washikaji zake kina SSimba,HGhasia,LMasha,na wengineo vimeo.....
   
Loading...