Baraza la Mawaziri Sri Lanka lajiuzulu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Baraza zima la mawaziri la Sri Lanka limejiuzulu kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali, yaliyofanyika licha ya sheria ya kutotoka nje iliyotangazwa mwishoni mwa juma lililopita.

Mawaziri wote 26, isipokuwa tu rais na waziri mkuu, wamewakilisha barua zao za kujiuzulu usiku wa kuamkia leo.

Sheria ya kusalia majumbani ilitangazwa Ijumaa, baada ya maandamano yaliyofanyika karibu na makaazi ya Rais Gotobaya Rajapaksa kugeuka ghasia.

Hata hivyo waandamanaji wengi waliikaidi amri hiyo, na mamia kadhaa miongoni mwao walikamatwa.

Serikali pia ilikata mawasiliano ya mitandao ya kijamii katika jaribio la kuzia maandamano hayo kuenea zaidi.

Asasi inayochunguza shughuli za kimtandao, imesema Facebook, Youtube, twitter, Instagram na Whatsapp yote ilikuwa haifanyi kazi. Taifa hilo la kisiwa katika Bahari ya Hindi linakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi, uliosababisha uhaba mkubwa wa chakula, mafuta na dawa.
 
Back
Top Bottom