RAKI BIG
JF-Expert Member
- Apr 26, 2020
- 394
- 456
Uamuzi huo ulifikiwa kufuatia mkutano uliyofanywa siku ya Alhamisi chini ya uongozi wa Makamu wa Rais wa kwanza Gaston Sindimwo.
Kufikia sasa bado haijabainika ni lini kiongozi mpya ataapishwa, japo katiba iko wazi kuwa Spika wa bunge la kitaifa Pascal Nyabenda alitakiwa kuapishwa kushikilia wadhifa wa Rais kwa kipindi cha mpito hadi Rais Mteule atakapoapishwa rasmi kuchukua hatamu ya uongozi.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema Rais Mteule, JeneralI Évariste Ndayishimiye, pia ni mgonjwa Mke wake alipigwa picha akitia saini kitabu cha maombolezo japo Ndayishimiye hajaonekana hadharani.
Chama cha Mawakili nchini Burundi kimetoa wito wa kuapishwa mara moja kwa Rais mteule.
Tovuti ya Kibinafsi pamoja na vyombo vingine vya habari vimesema kuwa mawaziri waliifahamisha mahakama hiyo kuhusu nafasi iliyo wazi katika ofisi ya rais.
Mahakama ya Katiba sasa inasubiriwa kutoa uamuzi ni nani anastahili kuapishwa kuwa rais, ilisema taarifa iliyochapishwa na tovuti ya Iwacu.
Kwa mujibu wa katiba Spika wa Bunge, Pascal Nyabenda, anatakiwa kuapishwa kama kiongozi wa mpito. Hata hivyo, Evariste Ndayishimiye wa chama tawala cha CNDD-FDD aliyechaguliwa Mei 20 anatakiwa kuapishwa mwezi Agosti.
Rais wa zamani, Sylvestre Ntibantunganya, ametoa wito Ndayishimiye aapishwe mara moja kama rais wa Burundi.
Huku hayo yakijiri kundi la upinzani linataka uchaguzi ufanywe upya.
BBC Swahili