Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Kuna kila dalili kwamba mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri yapo njiani. Hii ni kwasababu sio tu kwamba upinzani na umma umekuwa ukilalamika kwa muda mrefu juu ya ubabaishaji wa mawaziri kadhaa kiutendaji, bali sasa kilio hiki kimeingia hadi ndani ya chama Tawala ambapo watendaji wake wakuu (kinana na nape) wametamka waziwazi juu ya umuhimu wa kufanyika kwa mabadiliko.

Iwapo Rais Kikwete atafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri, hii baraza husika litakuwa ni kama la tano tangia aingie Ikulu. Kwa maana hii, na kwa kuzingatia kwamba mabadiliko haya yatakuwa ni ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu 2015, ni dhahiri kwamba selection ya mawaziri itafanywa kwa ustadi mkubwa ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali ya ccm, lakini hasa ili kutekeleza kauli za Kinana mikoani kwamba sasa ni wakati wa serikali ya ccm kurudi katika mstari na kuanza kutekeleza sera zake kwa vitendo.

Ingekuwa wewe ni Rais au mshauri wa Rais, je ungependekeza:

*Nani abaki, Nani atoke, na nani aingie?
*Je, kwa hoja zipi ambazo ni nje ya ushabiki wa kisiasa?
*Je, nje ya mabadiliko ya baraza la mawaziri, nini kingine inatakiwa kifanyike ili kuwezesha mawaziri watakaoteuliwa wawewe deliver katika kipindi kilichobakia kuelekea 2015? Je, sera na mikakati iliyopo ni mizuri, kinachokosekana ni usimamizi na utekelezaji? Je, kuna haja ya kubadili sera, mfumo na mikakati? Kama ipo haja, ni mfumo, sera na mikakati ipi ina mapungufu na ambayo haitasaidia sana mawaziri wapya kuboresha performance ya serikali katika kuhudumia wananchi?

Matarajio ya uzi huu ni mchango wa hoja zinazolenga kujenga, sio kubomoa kwa mujibu wa muktadha uliowasilishwa hapo juu, na mchango wa aina hiyo utathaminiwa sana. Isitoshe, hauwezi jua, pengine consistency ya hoja zenye kujenga zita influence mamlaka ya uteuzi baada ya sauti zetu wananchi kusikika ngazi husika. Mawaziri hawa wataenda kuendesha serikali kupitia kodi tunazolipa sasa na kwenda mbele, hivyo hata kama tumechoshwa na ubabaishaji wa viongozi, basi angalau tufanikishe kodi zetu zifanye kazi kwa ufanisi kwa kipindi kilichobakia, kabla ya kutumia haki zetu za kikatiba kwa ukamilifu kwa kuchagua viongozi wanao ona wanafaa, na kwa wale watakaoamua kwenda mbali zaidi, kuchagua chama cha siasa wanacho ona kinafaa, 2015.

Pengine kwa nia ya kuchokoza mada, nitaje watu watano ambao ningeshauri Rais Kikwete awape wizara zifuatazo:

1. John Magufuli - Waziri Mkuu. Kama alivyobainisha david kafulila bungeni, wa sasa hatoshi kwani ni mpole mno, hivyo mawaziri wanampuuza na kumdharau. Kafulila anasema kwamba anahitajika waziri mkuu mwenye uwezo na mwenye ushawishi au atakayeogopwa na mawaziri pamoja na watendaji serikalini. Kuogopwa sio sifa ya uongozi lakini kama itasaidia kunyoosha utendaji serikalini, kama anavyosema Kafulila, ni bora kuwa basi na waziri mkuu anayeogopwa iwapo hatopatikana waziri mkuu mwenye ushawishi na mwenye uwezo wa kutekeleza sera, maazimio ya bunge, ahadi za serikali bungeni, na kusimamia sheria. Magufuli anatosha kote - katika kusimamia sera, maamuzi ya bunge, sheria, lakini pia utendaji wake utawajaza woga viongozi legelege.

2.Mark Mwandosya - Nishati Na Madini kwa sababu ana uzoefu na hili akianzia kama kamishna wa nishati, katibu mkuu wizara ya nishati, mwanzilishi wa taasisi ya utafiti wa masuala ya nishati na mazingira inayotambulika kinataifa (CEEST), na ame publish tafiti nyingi sana zinazotumiwa ndani na nje ya nchi.

3. Samuel Sitta - Waziri wa Sheria na Katiba. Huyu ni mtaalamu wa sheria, amewahi kuwa waziri hapa awamu ya pili, na ameonyesha uwezo na nia ya kusimamia haki na sheria kupitia uspika na katika jamii kwa ujumla. Mtu wa aina hii atatusaidia kutupatia katiba bora na sio bora katiba.

4. Edward Lowassa - hapa, Rais aiondoe TAMISEMI kutoka ofisi ya waziri mkuu na badala yake ijitegemee kama wizara. Lowassa anaweza rekebisha mapungufu yaliyopo katika wizara hii nyeti inayogusa wananchi wengi kuliko wizara yoyote. Alionyesha uwezo mkubwa akiwa ardhi, na baadae maji, na kujizolea sifa nyingi za uchapa kazi pamoja na mrema awamu ya pili.

5. Anna Tibaijuka - Wizara ya fedha. Huyu ni professor wa uchumi mwenye uzoefu na uwezo unaotambulika, hivyo sina haja ya kumjadili kwa kirefu.

6. Professor Hassa Mlawa - mkuu wa kitengo cha IDS UDSM, amteue ubunge na kumpa wizara ya sayansi, mawasiliano na tekinolojia. Mlawa ni msomi na mtaalamu katika masuala ya innovation, science and technology, hasa roles za haya katika industrialization, na anaheshimika kimataifa katika utafiti wa maeneo haya. Moja ya vikwazo vikubwa vya kuendelea kiuchumi nchini ni nchi yetu kukosa msingi ya kutuwezesha kuwa na uwezo wa ushindani katika uchumi wa sasa wa dunia ambao upo more knowledge driven.

Hawa ni wachache ambao naamini watabadili sana sura ya serikali, hasa katika maeneo hayo. Nje ya kuteua watu wenye uwezo na sifa za kutosha, kuna haja ya kuangalia tena sera, mfumo na mikakati iliyopo ili kuongeza ufanisi katika utendaji serikalini. Tutayaangalia haya baadae.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mh Rais Kikwete anahitaji waziri mkuu mkali kidogo.Pinda anatia aibu kwakweli hasa mawaziri wanamdharau na maagizo yake yanapuuzwa.
Mimi naamini mwarobaini wa yote ni kupata waziri mkuu mtendaji kama Magufuli.
 
Nadania Mama Migiro anaandaliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje ama Waziri Mkuu
 
E bwanae ..du ulihcoandika na watakachoandika wengi naamini vyote vitaonyesha jinsi gani CCM imebaki na magarasa.Mtu amwambie Sitta kuwa safu ya CCM sio nene km alivyokuwa akiamini.
 
Kipaumbele cha kwanza kabla ya kupendekeza majina ya mawaziri tungeanza na wapi baraza jipya watafanyia semina elekezi. Tafadhali pendekeza hotel ya kuanzia nyota tano.

Ni vizuri na muhimu tusisahau vipaumbele vya nchi yetu, utaifa kwanza mengine baadaye. Haya tuanzie hapa.
 
Nadania Mama Migiro anaandaliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje ama Waziri Mkuu

Kwa mujibu wa katiba, waziri mkuu lazima atokane na mbunge wa jimbo, hivyo hili halitawezekana. Mapungufu ya mama migiro ni kwamba hatujaweza kupima uwezo wake kwa wananchi (kupitia jimboni hata kama angeshika nafasi ya tatu), kwahiyo inabakia tafsiri tu kwamba ushawishi wake pengine ni kwa watu waliokuwa nae karibu ambao wameweza kumpima. That said and done, kwa database ya wabunge wanawake (au wale waliowahi kuwa wabunge katika awamu ya nne), ni heri migiro arudishwe kuliko kuwa na mawaziri kama ghasia, sofia simba na kombani.

Pamoja na haya, migiro hawezi kumfikia mtu kama anna tibaijuka, na tulishajadili hili muda mrefu. Akiingia, she will become second best kwa upande wa kina mama. Na kuhusu suala la kuwa waziri wa mambo ya nje, katika nyakati hizi, lakini hasa ndani ya kipindi ambacho nchi haina dira ya taifa inayoeleweka, na nje ya nchi tukitambulika zaidi kwa kuzungusha bakuli la omba omba kama matonya, uzito wa wizara ya mambo ya nje upo over exaggerated, in my humble view. Wamweke tu, it will matter kwa wale wasiokubaliana na mtazamo wangu finyu.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ukishauri Mwakyembe aende Elimu lazima uwe na mbadala wake pale Wizara ya Uchukuzi, vivyo hivyo kwa Magufuli pia..

Upo sahihi. Taja taja yangu ililenga zaidi kuchokoza mada, natarajia wachangiaje wengine waje na mapendekezo yao au kupinga ya kwangu KWA HOJA kuliko SIASA.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Heeee!Yaani miaka nane amekuwa 'dhaifu' sasa hii miaka miwili itabadilisha nini?
Hakuna jipya hapo!May be we should wait 2015!
 
E bwanae ..du ulihcoandika na watakachoandika wengi naamini vyote vitaonyesha jinsi gani CCM imebaki na magarasa.Mtu amwambie Sitta kuwa safu ya CCM sio nene km alivyokuwa akiamini.

Ungenisoma mstari kwa mstari na, nina uhakika ungekuja na hoja makini zaidi ya hii. Lakini haina maana kwamba hoja yako sio makini, naongelea "makini zaidi";


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom