Baraza la mawaziri maswali bado ni mengi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,099
Baraza la mawaziri maswali bado ni mengi
TANZANIA DAIMA

JANA Rais Jakaya Kikwete, alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya kulivunja la awali wiki iliyopita kutokana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu.
Lowassa, alijiuzulu baada ya kuhusishwa na kashfa ya ushindi wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond Development (RDC).

Katika baraza jipya, Rais Kikwete amepunguza idadi ya mawaziri kutoka 29 hadi 26 na manaibu mawaziri kutoka 31 hadi 21. Kwa maana hiyo, baraza la sasa lina jumla ya mawaziri 47 kutoa 61 wa awali.

Miongoni mwa mawaziri hao, sita ni wapya kabisa huku akiwaachaa mawaziri tisa na manaibu wanane waliokuwa katika baraza la awali ambao kutokana na ukubwa wake, lilikuwa mzigo kwa walipa kodi.

Awali, kabla ya kutangazwa kwa baraza hilo la mawaziri, Rais Kikwete alisema Kingunge Ngombale - Mwiru na Joseph Mungai, wameomba kustaafu. Hawa inawezekana wamesoma alama za nyakati, hivyo wameamua kuomba kustaafu, ili kulinda heshima zao katika jamii.

Hata hivyo, kutangazwa kwa baraza hili kunaacha maswali mengi miongoni mwa wananchi baada ya asilimia 81 ya mawaziri wa zamani kuendelea kubaki. Mbaya zaidi, baadhi yao wakilalamikiwa kwa maamuzi mabovu yaliyoigharimu serikali na kusababisha hasara.

Tunaamini kuwa nia ya rais kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri ni njema, kwa sababu husikiliza na kufanyia kazi vilio vya wananchi wake, lakini kitendo cha kumrudisha Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ni kufuga ufisadi.

Tunasema hivyo kutokana na Chenge kuhusishwa kwenye ufisadi, anatuhumiwa pia kuliingiza taifa kwenye hasara alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kupitisha mikataba mibovu ya madini.

Chenge huyu pia aliwahi kukiri kwamba yeye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tangold inayotuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha za walipa kodi pale Benki Kuu (BoT). Tunashangazwa na uamuzi wa Rais Kikwete kumrudisha mtuhumiwa huyu wa ufisadi.

Pamoja na Chenge, ni matumaini ya Watanzania wengi kwamba Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa na Naibu wake, Dk. Aisha Kigoda, hawakustahili kurudi ndani ya baraza hilo kutokana na uzembe wakati wa upasuaji tata uliotokea kwenye Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI).

Ni maswali yanayokosa majibu kwa kila anayejiuliza, Rais Kikwete alikuwa na ulazima gani wa kuwarudisha mawaziri hawa? Ni siri gani imejificha ndani yake? Au hakuwa anafahamu hayo kuhusu mawaziri hao?

Tuna amini rais kwa kuteua tena mawaziri hao kutapunguza imani kwa wananchi kwa serikali yao, kwani wanaweza kudhani kuwa rais anawalinda watu hao au ameweka pamba masikioni mwake.

Aidha, tunaweza kuamini kuwa Rais Kikwete ameshauriwa vibaya katika hili na watendaji wake ambao kwa kiasi kikubwa wamepuuza vilio vya wananchi walio wengi.

Ndiyo maana tunasema, kutokana na baraza hilo lililotangazwa jana, kunazua maswali mengi kuliko majibu miongoni mwa wananchi.



 
Ni kweli maswali ni mengi kuliko majibu na hata ukiangalia uteuzi wa Shamsa Mwangunga kuwa waziri wa utalii huu ni utani kwa taifa hili na kwa watanzania kwa ujumla wake kuna haja ya kumwambia rais atuelewe kwani hapa naona hataki kutuelewa.
 
Nafikiri rais amewaacha hawa mawaziri hasa Chenge ili waje kusurubiwa wakati ripoti ya BOT itakapowasilishwa.
Kwamba Chenge ni mkurugenzi wa Tangold -rais analijua, kwamba Tangold imechota hela BOT isivyo halali - rais anajua maana ripoti ya BOT anayo!
Tusubiri
 
Back
Top Bottom