Baraza la Mawaziri likibadilishwa Kalemani aondolewe kwa hoja ya Tanesco kutokaguliwa, Mwanasheria Mkuu kusimamia awamu ya 5 kuvunja sheria

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
6,064
2,000
Nasikia tetesi za mabadiliko ya Baraza la mawaziri.

Namshauri mama asimuache Kalemani, kwa muda wote ameacha Tanesco bila kukaguliwa hesabu wakati anajua Tanesco inameza zaidi ya trilioni ishirini za nchi kwenye mradi wa bwawa la Stiegler's, mabilioni mengine pia.

Kuna uwezekano huko kuna uchotaji mkubwa wa pesa.

Kandarasi zote na sub contract za stiglers zikaguliwe kwa kuwa mwendazake alikuwa na tabia ya kuchomekea kampuni zake katika tenda za miradi ya kitaifa.

Pia tuelezwe ile miti iliyokatwa pale selous ilipelekwa wapi, nani kauziwa, pesa ilipelekwa wapi.

Hii iende kwa standard gauge railway, shirika la reli halijakaguliwa japo linatazamiwa kumeza trilioni zaidi ya 20, kama hapakaguliwi maana yake kuna watu wameweka mjira wa kula, hawataki uguswe.

ATCL pia

Mwanasheria Mkuu wa serikali ndiye alisimamia sheria kandamizi na kusimamia kesi kandamizi dhidi ya watanzania, bila shaka mtu huyu ni irrelevant kwa awamu ya sita inayofata sheria pamoja na haki za binadamu na utu.

Huyu aliyetunga sheria za kidikteta ili kuustawisha atupishe mapema, katiba ilivunjwa mbele ya macho yake, sheria zilivunjwa akiona, wananchi waliozea gerezani akinywa waini.
 

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
6,064
2,000
Hayo maswali ungemuuliza Mama maana alikuwa sehemu ya mfumo ila nashangaa unamuuliza waziri?

Mbona hauja ulisa repoti ambayo rais alitoa maelezo kuhusu BoT?
Hao watu waliwajibika kwa Rais ambaye aliwateua, sio mama, mama alisimamia muungano na mazingira, huko palikuwa safi
 

MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
604
1,000
CAG hufanya ukaguzi kwa mujibu wa Sheria sio chini ya Waziri. Ofisi ya CAG iwajibike kwa nini haiku act kisheria.
Acha kuelekeza attacks zako kwa watu au mtu, elekeza kwa taasisi, Jenga taasisi imara.
 

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
6,064
2,000
CAG hufanya ukaguzi kwa mujibu wa Sheria sio chini ya Waziri. Ofisi ya CAG iwajibike kwa nini haiku act kisheria.
Acha kuelekeza attacks zako kwa watu au mtu, elekeza kwa taasisi, Jenga taasisi imara.
Waziri anawajibika kama msimamizi was taasisi zilizo chini yake, pia anawajibika kisiasa kama ninavyopendekeza atumbuliwe. Haiwezekani nchi nzima tunalipa LuKu halafu hizo pesa hazikaguliwi zimetumikaje, labda kuna watu wanakula tu hiyo hela inayochangwa na watanzania masikini na wanyonge
 

keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,695
2,000
N.B: mashirika nyeti yote C.E.O ni wasukuma, kuna kitu kilikuwa kinalindwa/kulindana
Mkuu mie sio msukuma Ila umeongea kichuki Sana. Kama vile wao sio watanzania ama sio binadamu.kama Wana sifa za kuwekwa hapo acha wakae ama hawana elimu Kama ya kwako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom