Baraza la Mawaziri la Rais Mgufuli mbona Raia Wamelipotezea?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,702
71,013
Kuna jambo sio la kawaida linaendelea kwa sasa. Baraza la Mawaziri kwa Serikali yeyote ndio timu ya nchi katika utawala na chombo muhimu sana katika maendeleo ya nchi.

Lakini jambo la ajabu ni kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 Rais Magufuli amechukua zaidi ya wiki tatu hajataja baraza lake na tofauti na zamani jambo hilo lilipokuwa la muhimu, sasa hivi hakuna hata mwenye kufuatilia au kushauri nani awe nani katika baraza.

Je, kukosekana msisimko huo ni ishara kuwa baraza chini ya JPM huwa ni muhuri tuu? Au ni upotevu wa pesa kwani hata wasipokuwepo hakuna tofauti?
 
Ninavyosemaga hapa kuwa Watanzania ni magoigoi huwa sitanii.Nakuhakikishia hata kama Magufuli ataendesha hii nchi kwa mwaka mzima bila baraza la mawaziri wala hutasikia chochote kutoka kwa wananchi.Yaani wananchi kwao kila kitu ni sawa tu,kiwe kina manufaa kwa nchi,kiwe hakina manufaa kwa nchi au kiwe cha kuliangamiza Taifa kwao ni sawa tu.Ni magoigoi haswa!
 
Amesema wabunge ni wengi na anachukua miezi mitatu hadi Sita kupitia majina yao. Tarajia baraza mwezi wa Tatu 2021 na sio lote. Anaweza ibuka na mawaziri 6 baadae wanne, wawili nk. Hawezi kutangaza lote siku moja nimjuavyo Mtu yule. Ikumbukwe 2015 alichelewa Sana kutangaza pia baraza, Nani ana hamu ya kusubiri baraza lake?
 
Kuna wabunge walichungulia kwenye hadubini zao wakajiona hawapo so wanapga tunguli huko ili majina yao yarudi kwenye baraza
 
Kuna jambo sio la kawaida linaendelea kwa sasa. Baraza la mawaziri kwa serikali yeyote ndio timu ya nchi katika utawala na chombo muhimu sana katika maendeleo ya nchi.
Lakini jambo la ajabu ni kuwa baada ya uchaguzi Mkuu wa 2020 ambao wengi wameuita uchafuzi Mkuu Rais JPM amechukua zaidi ya wiki tatu hajataja baraza lake na tofauti na zamani jambo hilo lilipokuwa la muhimu, sasa hivi hakuna hata mwenye kufuatilia au kushauri nani awe nani katika baraza.
Jee kukosekana msisimko huo ni ishara kuwa baraza chini ya JPM huwa ni muhuri tuu? Au ni upotevu wa pesa kwani hata wasipokuwepo hakuna tofauti?
Ulimsikiliza wakati anamuapisha waziri mkuu?
 
Had wewe umeliandikia uzi, ujue linafuatiliwa
 
Ninavyosemaga hapa kuwa Watanzania ni magoigoi huwa sitanii.Nakuhakikishia hata kama Magufuli ataendesha hii nchi kwa mwaka mzima bila baraza la mawaziri wala hutasikia chochote kutoka kwa wananchi.Yaani wananchi kwao kila kitu ni sawa tu,kiwe kina manufaa kwa nchi,kiwe hakina manufaa kwa nchi au kiwe cha kuliangamiza Taifa.Ni magoigoi haswa!
Makatibu wakuu wanatosha
 
alishasema "mimi ni rais sipangiwi"
sasa wewe Paulo maconda umeamkia hapa jukwani kujigonga gonga labda akuchague si ujitulize kila mtu anaratiba zake acha kulamba lamba viatu kama kwa ridhiwani umeshasahaulika tulioshiba hatuna habari na wewe mwenye njaa. gonga gonga

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom