Baraza la Mawaziri la Kikwete lagawanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Mawaziri la Kikwete lagawanyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Nov 12, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mawaziri kumi wataka watuhumiwa waadhibiwe
  [​IMG]Wanane wanawatetea, waliosalia hawana msimamo
  [​IMG]Sophia Simba asonywa na wenzake

  BAADA ya Kamati inayoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuzungumza na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi na kuibuka malumbano, kejeli na matusi kwenye mkutano huo, imebainika kuwa sasa mpasuko si tu miongoni mwa wabunge; bali umesogea hadi kwenye Baraza la Mawaziri na kugawa mawaziri hao.

  Uchunguzi wa Raia Mwema, ukihusisha mazungumzo na baadhi ya wabunge na mawaziri, umebaini kuwa mpasuko katika baraza la mawaziri kwa kiasi fulani umechukua sura tofauti na ule wa wabunge wa CCM.

  Katika Baraza la Mawaziri, hali ni tofauti. Siku kadhaa mara baada ya mkutano wa Mwinyi, Dodoma, wapo mawaziri walioanza kuwapuuza manaibu mawaziri wao, lakini pia wapo manaibu mawaziri walioanza kuwapuuza mawaziri wao, hali inayotajwa kuwa huenda ikasogea hadi kwa watendaji wa chini kwenye wizara na hatimaye kugawa watendaji wote.

  Lakini pia katika mazungumzo hayo ya Raia Mwema, pia imebainika kuwa kuna baadhi ya wizara zenye mawaziri wanaofanana kimtazamo wakiwa kundi moja kwenye mpasuko huo; hali inayotajwa kuwa huenda ikazua mvutano kama watendaji wengine waandamizi wizarani watakuwa na misimamo pinzani.

  Mpasuko huo chanzo chake kinatajwa kuwa kashfa ya Richmond, na hususan kuhusika kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwenye sakata hilo ambapo mawaziri na manaibu mawaziri wanaodaiwa kuwa karibu naye wameendelea kumtetea kwa siri na hadharani; huku wengine wakitafsiri hatua hiyo kuwa ni upuuzi na hata kuwaona wenzao wanaoendesha harakati hizo ni wapuuzi.

  Mmoja wa mawaziri hao ni Sophia Simba, ambaye sasa si tu imedaiwa anatazamwa kwa jicho tofauti na baadhi ya mawaziri wenzake, lakini pia CCM imeanza kukana baadhi ya shutuma alizotoa kwa baadhi ya watu katika juhudi zake za kutetea watuhumiwa wa kashfa mbalimbali. Simba anadaiwa kueleza kuwa Mfanyabiashara Reginald Mengi, si mwanachama wa chama hicho.

  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kati ya mawaziri 26 waliopo ukimwondoa Waziri Mkuu, 10 wamedaiwa kuwa na msimamo unaofanana na baadhi ya wabunge wapambanaji wa ufisadi wakiwa na msimamo watuhumiwa wa ufisadi waadhibiwe, wakati mawaziri wengine wanane wakiwa katika kundi la utetezi.

  Mawaziri wanaodaiwa kuwa na msimamo wa kupinga ufisadi ukiwamo wa Richmond ni pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Uvuvi, John Magufuli, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Bunge, Philip Marmo.

  Wengine ni Waziri wa Afya, Profesa David Mwakyusa ambaye anatajwa kuwa na msimamo wa chini chini, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani, Waziri wa Afrika Mashariki, Diodorous Kamala na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Margaret Sitta.

  Mawaziri wanaodaiwa kuwa msimamo wao haueleweki katika sakata la Richmond ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Waziri wa Kilimo, Stephen Wasira.

  Hata hivyo, inaelezwa kuwa kundi la mawaziri wenye msimamo mkali wanaotaka hatua kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa, wengi wao wamekuwa na rekodi nzuri kiutendaji ikilinganishwa na wale watetezi wa watuhumiwa.
  Baadhi ya wabunge waliozungumza na Raia Mwema wamedai kuwa mawaziri wengine wanane msimamo wao umeshindwa kubainika moja kwa moja kutokana na kuwapo katika kila kundi.

  Katika mkutano uliopita wa Bunge, utekelezaji wa lala salama wa mazimio ya Bunge kuhusu Richmond ulipaswa kutolewa taarifa na serikali lakini haikuwa hivyo, bila kuelezwa sababu za wazi.

  Uchunguzi huo wa muda mrefu wa Raia Mwema bungeni pia umebaini kuwa athari za makundi kwa kiasi fulani zimekuwa zikimgusa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye ndiye aliteuliwa na Rais baada ya Lowassa kujiuzulu.

  Uchunguzi huo umebaini kuwa katika mkutano wa 16 wa Bunge na baadhi ya vikao vya mkutano wa 17 uliokwisha, hivi karibuni, wakati akitoa hoja au kujibu maswali ya papo kwa papo yenye utetezi wa Serikali ni sehemu ya mawaziri wachache tu wamekuwa wakimpongeza kwa kumpigia makofi na wengine wakibaki kuduwaa, wengine wakiwa katika mazungumzo yao.

  Kutokana na hali hiyo, mmoja wa wabunge amedai kuwa wapo mawaziri wasiompa nafasi ya heshima na utiifu unaostahili Waziri Mkuu Pinda na kwamba, wameendelea kuwa watiifu zaidi kwa kundi lao kuliko kwa waziri mkuu.

  Wizara ambazo zimejipambanua kuwa na waziri mwenye msimamo wa utetezi kwa Lowassa na watuhumiwa wengine ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Utawala Bora, inayoongozwa na Sophia Simba.

  Wizara nyingine ambazo zimebainika kuwa na mawaziri wenye misimamo ya makundi ni pamoja na Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, inayoongozwa na Profesa Juma Kapuya, na Naibu wake Dk. Makongoro Mahanga.

  Kapuya alitajwa na kundi mojawapo kwenye mpasuko huo kuwa ni kati ya watu wanaopaswa kuchukuliwa hatua akidaiwa kumtetea Lowassa kwa gharama za wanasiasa wengine akiwamo Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Naibu wake, Makongoro naye pia alijipambunua kuwamo kwenye kundi la Lowassa, wakati wa mkutano wa Mwinyi.

  Baadhi ya wabunge pia wanaitazama Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa inaongozwa na viongozi wenye mgongano wa makundi, japokuwa ikidaiwa kuwa Naibu Waziri Khamis Kagasheki, amejitahidi kwa muda mrefu kuficha hisia zake tofauti na Waziri wake, Lawrance Masha, anayedaiwa kuwa kundi la Lowassa.

  Katika hatua nyingine, baadhi ya wabunge waliozungumza na Raia Mwema kutoka makundi yote wamebainisha matarajio yanayozidi kukinzana mara baada ya kukamilika kwa mkutano kati yao na Kamati ya Mwinyi.

  Wakati upande mmoja ukiendelea kusisitiza kuwa watuhumiwa wenye nyadhifa katika chama hicho wang’olewe, wenzao wamekuwa na msimamo tofauti.

  Hata hivyo, kundi la wabunge wanaotaka wenzao watuhumiwa watimuliwe ndilo linaonekena kuwa na nguvu zaidi hata mbele ya wananchi na taasisi nyeti zikiwamo za elimu ya juu nchini kama ambavyo imekuwa ikiandikwa na baadhi ya magazeti nchini.

  Kwa upande mwingine, hali ya kuwapo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mvutano huenda ikaendelea. Kuwapo kwa dalili hizo kunatokana na kuendelea kukinzana kati ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta na baadhi ya wanasiasa wa kundi linalomwandama, akiwamo Kingunge Ngombale-Mwiru.

  Kingunge katika mkutano uliopita wa NEC-CCM Dodoma aliripotiwa kutaka Spika Sitta ang’olewe kwa kuwa anaendesha Bunge vibaya kwa kuruhusu mijadala ya ufisadi na hivyo kuhatarisha chama na serikali na kuimarisha hoja yake kwa kusema ubaya wa Spika unathibitishwa na hatua yake ya kuandika kitabu kinachoitwa “Bunge lenye Meno” akishirikiana na wabunge wengine machachari, akiwamo Dk. Harrison Mwakyembe.

  Inaelezwa kuwa Kingunge alirejea msimamo wake huo katika mkutano wa Mwinyi lakini akionyesha kukejeli msimamo huo, Spika wa Bunge wakati akizungumza bungeni muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, alijigamba kuwa Bunge lake bado lina meno.

  Sitta alitamka; “Ni Bunge lenye meno” wakati akielezea uamuzi wa kuwatuma wabunge kwenda eneo la Loliondo lenye mgogoro kati ya wananchi na mwekezaji, mgogoro ambao serikali kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsha Mwangunga, iliwasilisha ripoti yake iliyotokana na kamati aliyounda kubaini kama kulikuwa na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

  Ripoti hiyo ya Mwangunga ilikataliwa na Bunge baada ya Waziri kueleza kuwa hapakuwa na haki za binadamu huku wananchi walioathirika wakieleza kuwa haki zao zilikiukwa, ikiwa ni pamoja na kuchomewa makazi na karaha nyingine zikiwamo za vitendo vya udhalilishaji wa wanawake.

  Awali, kabla ya Spika kuingia bungeni kikao cha Bunge kilikuwa kikiongozwa na Mwenyekiti, Job Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa CCM, ambaye alionekana kutaka kuikubali ripoti hiyo ya Serikali kabla ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kusimama na kueleza Bunge kuwa kwa sehemu kubwa ripoti ya Waziri Mwangunga imejaa uongo na hivyo kuomba mwongozo wa Spika ili kutoa uamuzi utakaolinda maslahi ya wananchi.

  Kutokana na uamuzi huo, Ndugai alikubali na kueleza kuwa atalifikisha suala hilo kwa Spika ambaye atatoa uamuzi na ilipofika kikao cha jioni siku hiyo, Spika akatoa msimamo kuwa atatuma timu ya wabunge kwenda Loliondo, hatua ambayo bila shaka mbele ya kina Kingunge itaendelea kumtafsiri Sitta kama kikwazo kwa mambo ya serikali kupita bila kujali yana maslahi ya wananchi au la.

  Ripoti ya kamati ya Mwinyi inatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano ujao wa NEC-CCM bila shaka baada ya kupitia mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.

  Kwa muda mrefu kumekuwa na wito wa kutaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aenguliwe katika wadhifa huo kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwamo za kuendelea siasa za makundi kwenye chama hicho. Kati ya matukio yanayomuhukumu Makamba ni kitendo chake cha kumlaani kada machachari wa CCM, Nape Nnauye, aliyejitokeza hadharani na kudai kuwa mkataba wa ujenzi katika jengo la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Upanga Dar es Salaam ni wa wizi na unaonyonya jumuiya hiyo.

  Katika shutuma zake hizo, Nape alitaka baadhi ya viongozi wa Baraza la Wadhamini wa UVCCM akiwamo Edward Lowassa, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na kujiuzulu kwa kashfa ya Richmond , awajibike. Makamba aliwatetea wadhamini hao akishirikiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Dk. Emmanuel Nchimbi.

  Hata hivyo, suala hilo lilifikishwa kwenye NEC-CCM na uamuzi ulitolewa kuwa iundwe kamati kuchunguza na ikibidi kurekebisha mkataba huo. Kamati hiyo ilifanya marekebisho makubwa, uamuzi ambao kwa namna fulani unaathiri umakini wa Makamba katika utetezi wake kwa baadhi viongozi wanaodaiwa kuwamo katika kundi lake ndani ya CCM.

  Source: Raia Mwema
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,148
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Tumechoka na hizi ngojera za CCM, badala ya kusimama maendeleo na ustawi wa nchi hiki chama kimebaki kusimamia ufisadi na migogoro. Sidhani ikiwa kuna kitu cha maana kitafanyika hapa chini ya CCM ya akina Makamba.

  Anyway, ni kwa nini Kawambwa na akina Mwinyi wanashindwa kujipambanua upande wao katika vita hii ya ufisadi?
   
 3. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Yote haya yanasababishwa na Muungwana JK, wahalifu wapo wazi anawalea, lowasa, rostam, hosea n.k, basi ajiuzulu yeye sasa. Ingekuwa mwl Nyerere saizi mjadala ungekuwa ulishamalizika siku nyingi. kwa rais hatuna wa tz wenzangu. Tufanye changes 2010.
   
 4. b

  barakab New Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du ni balaa maana ,......................
   
 5. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mods hii habari tayari ipo kwenye thread ya JK awaita mawaziri wake
   
 6. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  [​IMG]
  Godfrey Dilunga​
  [​IMG]
  [​IMG]Mawaziri kumi wataka watuhumiwa waadhibiwe

  [​IMG]Wanane wanawatetea, waliosalia hawana msimamo

  [​IMG]Sophia Simba asonywa na wenzake

  BAADA ya Kamati inayoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuzungumza na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi na kuibuka malumbano, kejeli na matusi kwenye mkutano huo, imebainika kuwa sasa mpasuko si tu miongoni mwa wabunge; bali umesogea hadi kwenye Baraza la Mawaziri na kugawa mawaziri hao.
  Uchunguzi wa Raia Mwema, ukihusisha mazungumzo na baadhi ya wabunge na mawaziri, umebaini kuwa mpasuko katika baraza la mawaziri kwa kiasi fulani umechukua sura tofauti na ule wa wabunge wa CCM.
  Katika Baraza la Mawaziri, hali ni tofauti. Siku kadhaa mara baada ya mkutano wa Mwinyi, Dodoma, wapo mawaziri walioanza kuwapuuza manaibu mawaziri wao, lakini pia wapo manaibu mawaziri walioanza kuwapuuza mawaziri wao, hali inayotajwa kuwa huenda ikasogea hadi kwa watendaji wa chini kwenye wizara na hatimaye kugawa watendaji wote.
  Lakini pia katika mazungumzo hayo ya Raia Mwema, pia imebainika kuwa kuna baadhi ya wizara zenye mawaziri wanaofanana kimtazamo wakiwa kundi moja kwenye mpasuko huo; hali inayotajwa kuwa huenda ikazua mvutano kama watendaji wengine waandamizi wizarani watakuwa na misimamo pinzani.
  Mpasuko huo chanzo chake kinatajwa kuwa kashfa ya Richmond, na hususan kuhusika kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwenye sakata hilo ambapo mawaziri na manaibu mawaziri wanaodaiwa kuwa karibu naye wameendelea kumtetea kwa siri na hadharani; huku wengine wakitafsiri hatua hiyo kuwa ni upuuzi na hata kuwaona wenzao wanaoendesha harakati hizo ni wapuuzi.
  Mmoja wa mawaziri hao ni Sophia Simba, ambaye sasa si tu imedaiwa anatazamwa kwa jicho tofauti na baadhi ya mawaziri wenzake, lakini pia CCM imeanza kukana baadhi ya shutuma alizotoa kwa baadhi ya watu katika juhudi zake za kutetea watuhumiwa wa kashfa mbalimbali. Simba anadaiwa kueleza kuwa Mfanyabiashara Reginald Mengi, si mwanachama wa chama hicho.
  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kati ya mawaziri 26 waliopo ukimwondoa Waziri Mkuu, 10 wamedaiwa kuwa na msimamo unaofanana na baadhi ya wabunge wapambanaji wa ufisadi wakiwa na msimamo watuhumiwa wa ufisadi waadhibiwe, wakati mawaziri wengine wanane wakiwa katika kundi la utetezi.
  Mawaziri wanaodaiwa kuwa na msimamo wa kupinga ufisadi ukiwamo wa Richmond ni pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Uvuvi, John Magufuli, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Bunge, Philip Marmo.
  Wengine ni Waziri wa Afya, Profesa David Mwakyusa ambaye anatajwa kuwa na msimamo wa chini chini, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani, Waziri wa Afrika Mashariki, Diodorous Kamala na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Margaret Sitta.

  Mawaziri wanaodaiwa kuwa msimamo wao haueleweki katika sakata la Richmond ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Waziri wa Kilimo, Stephen Wasira. Hata hivyo, inaelezwa kuwa kundi la mawaziri wenye msimamo mkali wanaotaka hatua kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa, wengi wao wamekuwa na rekodi nzuri kiutendaji ikilinganishwa na wale watetezi wa watuhumiwa. Baadhi ya wabunge waliozungumza na Raia Mwema wamedai kuwa mawaziri wengine wanane msimamo wao umeshindwa kubainika moja kwa moja kutokana na kuwapo katika kila kundi.
  Katika mkutano uliopita wa Bunge, utekelezaji wa lala salama wa mazimio ya Bunge kuhusu Richmond ulipaswa kutolewa taarifa na serikali lakini haikuwa hivyo, bila kuelezwa sababu za wazi.
  Uchunguzi huo wa muda mrefu wa Raia Mwema bungeni pia umebaini kuwa athari za makundi kwa kiasi fulani zimekuwa zikimgusa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye ndiye aliteuliwa na Rais baada ya Lowassa kujiuzulu.
  Uchunguzi huo umebaini kuwa katika mkutano wa 16 wa Bunge na baadhi ya vikao vya mkutano wa 17 uliokwisha, hivi karibuni, wakati akitoa hoja au kujibu maswali ya papo kwa papo yenye utetezi wa Serikali ni sehemu ya mawaziri wachache tu wamekuwa wakimpongeza kwa kumpigia makofi na wengine wakibaki kuduwaa, wengine wakiwa katika mazungumzo yao.
  Kutokana na hali hiyo, mmoja wa wabunge amedai kuwa wapo mawaziri wasiompa nafasi ya heshima na utiifu unaostahili Waziri Mkuu Pinda na kwamba, wameendelea kuwa watiifu zaidi kwa kundi lao kuliko kwa waziri mkuu.
  Wizara ambazo zimejipambanua kuwa na waziri mwenye msimamo wa utetezi kwa Lowassa na watuhumiwa wengine ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Utawala Bora, inayoongozwa na Sophia Simba.
  Wizara nyingine ambazo zimebainika kuwa na mawaziri wenye misimamo ya makundi ni pamoja na Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, inayoongozwa na Profesa Juma Kapuya, na Naibu wake Dk. Makongoro Mahanga.
  Kapuya alitajwa na kundi mojawapo kwenye mpasuko huo kuwa ni kati ya watu wanaopaswa kuchukuliwa hatua akidaiwa kumtetea Lowassa kwa gharama za wanasiasa wengine akiwamo Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Naibu wake, Makongoro naye pia alijipambunua kuwamo kwenye kundi la Lowassa, wakati wa mkutano wa Mwinyi.
  Baadhi ya wabunge pia wanaitazama Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa inaongozwa na viongozi wenye mgongano wa makundi, japokuwa ikidaiwa kuwa Naibu Waziri Khamis Kagasheki, amejitahidi kwa muda mrefu kuficha hisia zake tofauti na Waziri wake, Lawrance Masha, anayedaiwa kuwa kundi la Lowassa.
  Katika hatua nyingine, baadhi ya wabunge waliozungumza na Raia Mwema kutoka makundi yote wamebainisha matarajio yanayozidi kukinzana mara baada ya kukamilika kwa mkutano kati yao na Kamati ya Mwinyi.
  Wakati upande mmoja ukiendelea kusisitiza kuwa watuhumiwa wenye nyadhifa katika chama hicho wang’olewe, wenzao wamekuwa na msimamo tofauti.
  Hata hivyo, kundi la wabunge wanaotaka wenzao watuhumiwa watimuliwe ndilo linaonekena kuwa na nguvu zaidi hata mbele ya wananchi na taasisi nyeti zikiwamo za elimu ya juu nchini kama ambavyo imekuwa ikiandikwa na baadhi ya magazeti nchini.
  Kwa upande mwingine, hali ya kuwapo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mvutano huenda ikaendelea. Kuwapo kwa dalili hizo kunatokana na kuendelea kukinzana kati ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta na baadhi ya wanasiasa wa kundi linalomwandama, akiwamo Kingunge Ngombale-Mwiru.
  Kingunge katika mkutano uliopita wa NEC-CCM Dodoma aliripotiwa kutaka Spika Sitta ang’olewe kwa kuwa anaendesha Bunge vibaya kwa kuruhusu mijadala ya ufisadi na hivyo kuhatarisha chama na serikali na kuimarisha hoja yake kwa kusema ubaya wa Spika unathibitishwa na hatua yake ya kuandika kitabu kinachoitwa “Bunge lenye Meno” akishirikiana na wabunge wengine machachari, akiwamo Dk. Harrison Mwakyembe.
  Inaelezwa kuwa Kingunge alirejea msimamo wake huo katika mkutano wa Mwinyi lakini akionyesha kukejeli msimamo huo, Spika wa Bunge wakati akizungumza bungeni muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, alijigamba kuwa Bunge lake bado lina meno.
  Sitta alitamka; “Ni Bunge lenye meno” wakati akielezea uamuzi wa kuwatuma wabunge kwenda eneo la Loliondo lenye mgogoro kati ya wananchi na mwekezaji, mgogoro ambao serikali kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsha Mwangunga, iliwasilisha ripoti yake iliyotokana na kamati aliyounda kubaini kama kulikuwa na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.
  Ripoti hiyo ya Mwangunga ilikataliwa na Bunge baada ya Waziri kueleza kuwa hapakuwa na haki za binadamu huku wananchi walioathirika wakieleza kuwa haki zao zilikiukwa, ikiwa ni pamoja na kuchomewa makazi na karaha nyingine zikiwamo za vitendo vya udhalilishaji wa wanawake.
  Awali, kabla ya Spika kuingia bungeni kikao cha Bunge kilikuwa kikiongozwa na Mwenyekiti, Job Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa CCM, ambaye alionekana kutaka kuikubali ripoti hiyo ya Serikali kabla ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kusimama na kueleza Bunge kuwa kwa sehemu kubwa ripoti ya Waziri Mwangunga imejaa uongo na hivyo kuomba mwongozo wa Spika ili kutoa uamuzi utakaolinda maslahi ya wananchi.
  Kutokana na uamuzi huo, Ndugai alikubali na kueleza kuwa atalifikisha suala hilo kwa Spika ambaye atatoa uamuzi na ilipofika kikao cha jioni siku hiyo, Spika akatoa msimamo kuwa atatuma timu ya wabunge kwenda Loliondo, hatua ambayo bila shaka mbele ya kina Kingunge itaendelea kumtafsiri Sitta kama kikwazo kwa mambo ya serikali kupita bila kujali yana maslahi ya wananchi au la.
  Ripoti ya kamati ya Mwinyi inatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano ujao wa NEC-CCM bila shaka baada ya kupitia mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.
  Kwa muda mrefu kumekuwa na wito wa kutaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aenguliwe katika wadhifa huo kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwamo za kuendelea siasa za makundi kwenye chama hicho. Kati ya matukio yanayomuhukumu Makamba ni kitendo chake cha kumlaani kada machachari wa CCM, Nape Nnauye, aliyejitokeza hadharani na kudai kuwa mkataba wa ujenzi katika jengo la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Upanga Dar es Salaam ni wa wizi na unaonyonya jumuiya hiyo.
  Katika shutuma zake hizo, Nape alitaka baadhi ya viongozi wa Baraza la Wadhamini wa UVCCM akiwamo Edward Lowassa, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na kujiuzulu kwa kashfa ya Richmond , awajibike. Makamba aliwatetea wadhamini hao akishirikiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Dk. Emmanuel Nchimbi.
  Hata hivyo, suala hilo lilifikishwa kwenye NEC-CCM na uamuzi ulitolewa kuwa iundwe kamati kuchunguza na ikibidi kurekebisha mkataba huo. Kamati hiyo ilifanya marekebisho makubwa, uamuzi ambao kwa namna fulani unaathiri umakini wa Makamba katika utetezi wake kwa baadhi viongozi wanaodaiwa kuwamo katika kundi lake ndani ya CCM.  Source: Raia Mwema
   
 7. j

  jonbalele Member

  #7
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki Tanzania......
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Nov 13, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  IBARIKI NA WATU WAKE WOTE, NA AWALAAN walafi wot na mafisadi, kwa kuanzia na RA, na mzee wa Monduli plus Manji Yusuph
   
 9. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ameen
   
 10. m

  mtangi Member

  #10
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tutafika Kweli kwa hali hii ??
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kura ilipigwa lini na wapi..mwandishi anatuchanganya..lol CCM wote ni mafisadi hakuna cha wanane wazuri wala wawili..please let them quit akiwemo JK come 2010.
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Na JM Kikwete
   
 13. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga.
   
 14. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,961
  Trophy Points: 280
  Na Waandishi Wetu

  SAKATA la vita dhidi ya ufisadi limezidi kuchukua mwelekeo mpya baada ya baadhi ya mawaziri kutuhumiwa kuwa wamewekwa mfukoni na matajiri wachache, huku wanaotuhumiwa kwa ufisadi wakitakiwa kuungama mbele ya wananchi badala ya kutaka mambo yao yamalizwe ndani ya vikao.

  Tuhuma kuwa mawaziri wamewekwa mfukoni na matajiri wachache zimekuja miezi michache baada ya wabunge kulituhumu Baraza la Mawaziri kuwa na ubinafsi na kwamba, linabariki mikataba mibovu wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge la Muungano uliotaliwa na kauli kali dhidi ya serikali.

  Madai hayo pia yametolewa katikati ya mjadala mkubwa baina ya matajiri na wanasiasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na watoaji tuhuma, huku baadhi ya mawaziri wakijitokeza kuwatetea watuhumiwa hao.

  Juzi, naibu katibu mkuu wa CUF upande wa Zanzibar, Juma Duni Haji alisema kuwa mawaziri wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete wamewekwa mifukoni na matajiri wachache nchini ndio maana wanashindwa kuwajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi wao.

  Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Zakheim, Mbagala jijini Dar es Salaam juzi jioni, Duni alisema kitendo cha mawaziri wa Rais Jakaya kuingizwa mifukoni mwa matajiri kimeathiri maendeleo ya nchi.

  “Ndugu zangu, mawaziri wa Kikwete wote wameingizwa mifukoni mwa matajiri; hawafurukuti na wala hawana kauli mbele ya matajiri hao kwa sababu matajiri hawatawaliki. Wanaotawaliwa ni maskini na wajinga watu wasio na elimu, alisema Duni ambaye pia ni mkurugenzi wa fedha na uchumi wa chama hicho.

  Hivi sasa matajiri wachache wanayumbisha nchi, serikali pamoja na chama tawala (CCM). Kila mtu anajua hilo wala halihitaji akili ya ziada kulibaini. Mara (mwenyekiti wa IPP, Reginald) Mengi ni mwanachama wetu mara si mwanachama wetu.

  Alifafanua kuwa, mabadiliko ya Tanzania hayawezi kutokea bungeni bali yataanzia katika ngazi ya jamii, akifafanua kuwa ni mitaa, kata, jimbo, wilaya, mikoa na baadaye taifa.

  “Ndugu zangu kama mabadiliko yanatokea bungeni, wabunge si wanazungumza, kamati si zimeundwa na ripoti si zinatolewa? Kwa nini hakuna mabadiliko bungeni na hata ndani ya nchi, alihoji Duni akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.

  Alisema hata wabunge wanaopambana na ufisadi “hadi kutokwa na povu mdomoni” kwa sababu ya hasira na uchungu, ndio wanaodaiwa kuwa mabingwa wa kula posho mbili na wengine kufadhiliwa sherehe za harusi zao na mafisadi.

  Duni alifikia wakati kukejeli malumbano baina ya wabunge wa CCM na mawaziri akisema kuwa yanaonyesha kutia wasiwasi kwa anayewateua.

  Alirejea kitendo cha mbunge wa Mtera, John Malecela kumuelezea Waziri wa Utawala Bora, Sophia Simba kuwa ana kichaa baada ya kutoa tuhuma dhidi ya waziri huyo mkuu wa zamani kuwa kinaonyesha kuwepo na matatizo katika uteuzi.
  Hivi kama hivyo ndivyo, yaani Sophia Simba ni kichaa, aliyemchagua atakuwa na hali gani? Jibu mtatoa nyinyi wananchi ambao wengi wenu hadi sasa saa 12:00 jioni hamjajua cha kula, alisema Duni.

  Duni aliwataka wananchi hao kuchukua mfano wa watu wa Kilimanjaro na kwamba, wao waliwekeza katika elimu na uchumi na hivyo kutokubali kutawaliwa ovyo.

  Kilimanjaro lami hadi ******; umeme hadi migombani; shule nzuri zenye sifa za shule bora yote... zote ziko kwao hata vigogo wa nchi hii wengi wao wameoa katika mkoa huo kwa sababu wana maendeleo, alidai Duni.

  Alisema wananchi katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga wanaishia kunywa pombe tu licha ya mikoa yao kuwa na rasilimali kubwa na kwamba, badala yake maendeleo yanayotokana na rasilimali zao yanawanufaisha wengine ambao ni wajanja na waliosoma.

  Aliwataka wananchi hao kutokata tamaa ya kupambana kudai haki zao kwa sababu mwisho wa mapambano ni kufanikiwa, huku akitolea mfano Afrika Kusini ambayo alisema chama cha ANC kilipambana kwa zaidi ya miaka 70 hadi kufanikiwa mwaka 1994.

  Naye mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro amewajia juu viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi akiwataka waungame mbele ya wananchi badala ya kutaka mambo yao yamalizwe ndani ya vikao.

  Kimaro alisema kutumia utaratibu huo ni sawa na Mkristo kuungama mbele ya padri bila waumini wengine kufahamu dhambi zake na kusisitiza kuwa mafisadi lazima watajwe kwa majina.

  Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi wakati akiwapa pole wananchi wa Kijiji cha Goha, Same ambao ndugu zao 24 walifariki dunia baada ya kufukiwa na vifusi vya mlima ulioporomoshwa na mvua.

  Kabla ya kauli hiyo, Kimaro alisema maafa hayo ni ya Watanzania wote na anaungana na mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecela na wananchi wake kuomboleza msiba huo mkubwa.

  Kimaro aliwataka wananchi hao kuungana na kushikamana na mbunge wao ambaye alisema yuko mstari wa mbele kutetea maslahi yao na ya Watanzania wote kwa ujumla.

  “Kilango anapambana na rushwa hadi dunia nzima inamtambua kumpa sifa ya mwanamke jasiri! anapambana na wala rushwa na siku zote anataka watajwe kwa majina, alisema.

  Alisema bungeni si sawa na kanisani kwamba mchungaji akishasema basi, bali ndani ya chombo hicho kinachotawala ni hoja na kuongeza kuwa anaamini mafisadi ni kundi dogo sana ambalo halitaweza kuwayumbisha.

  “Wengine wanasema ooh hayo mambo pelekeni kwenye vikao hiyo ni sawa na kuungama mbele ya padri! sisi tunataka waungame na tuwajue wameungama nini ili tuwasamehe, alisisitiza.

  Kimaro aliwataka viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi kutosubiri hadi wafikishwe mahakamani na mahakama kutoa hukumu kwani kitendo cha kuhisiwa tu ni dosari kubwa kiuongozi.

  “Ile kuhisiwa tu ni lazima kiongozi uachie ngazi usisubiri hadi mahakamani… kule kuhisiwa tu kunakupotezea sifa ya uongozi na hawa waondoke ili kukipa chama sifa, alisema.

  Kwa upande wake, Kilango ambaye kabla ya kuzungumza alitembelea eneo la maafa na kuangua kilio kwa dakika 30, aliahidi kujenga mnara wa kumbukumbu katika eneo hilo.

  Tumelia sana lakini tumwambie Mungu asante! ndugu zetu wamekufa kifo kibaya sana; naomba Mungu anisaidie nijenge mnara wa kumbukumbu tuandike majina yao,alisema.

  Mbunge huyo, mbali na kupeleka misaada mbalimbali kwa wananchi hao, aliamua kupiga kambi eneo hilo kwa siku nne kuwafariji wananchi wake na kuzungumza nao kwa karibu.

  Kilango alipeleka msaada wa chakula, mafuta ya kupikia, sukari na ng'ombe huku mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya akitoa Sh100,000 na Kimaro aliyetoa kiasi kikubwa cha maharage.
  Habari hii imendaliwa na Daniel Mjema, Same, Salim Said na Fidelis Butahe.

  Source: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16031

  Haya ndo niliyokuwa nayasema humu ndani! watu wa Shinyanga na Mwanza wamelaaniwa? kwanini wasiwe mstari wa mbele kuipinga CCM? Inakuwaje wanadanganywa na siasa chafu kama ati Chadema ni chama cha Wachagga na CUF chama cha Waislam ilhali wanataabika kwanini wasijaribu? Kama Mababu zetu waliweza kumuamini Mwl Nyerere na kumruhusu kuwaongoza dhidi ya Mkoloni mbali na vizingiti alivyopata toka kwa Wakoloni hao, inamaana Mababu zetu walikuwa na hekima zaidi yetu sisi tunaoshindwa kutafakari na kupambanua! Leo hii imendikwa article ya kuhusu Chadema na Uchagga ambayo imekosoa sana tena kwa chuki juu ya hawa Wachagga lakini tujiulize hawa watu wana shida gani haswa mpaka kutaabika na mageuzi kama huduma wanazo na tunajua ni kwanini? kwa vile waliitetesha na kuichachafya CCM vilivyo(ikumbukwe Kilimanjaro ilwahi kuwa na wabunge wa upinzani majimbo yote ukiacha Same a record in Bara) hata ikabidi wapeleke huduma vivyo hivyo na Wapemba CCM Visiwani inajenga barabara asikuambie mtu huko Upembani! Mtanzania jikomboe acha siasa za propaganda shukuru hata huyo Mchagga au Mpemba kuwepo kukuamsha weye Msukuma uliyelala ukiibiwa urithi wako!
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,453
  Likes Received: 81,691
  Trophy Points: 280
  Date::11/16/2009Mawaziri wa Kikwete wadaiwa wamemezwa na mafisadi

  Na Waandishi Wetu
  Mwananchi

  SAKATA la vita dhidi ya ufisadi limezidi kuchukua mwelekeo mpya baada ya baadhi ya mawaziri kutuhumiwa kuwa wamewekwa mfukoni na matajiri wachache, huku wanaotuhumiwa kwa ufisadi wakitakiwa kuungama mbele ya wananchi badala ya kutaka mambo yao yamalizwe ndani ya vikao.

  Tuhuma kuwa mawaziri wamewekwa mfukoni na matajiri wachache zimekuja miezi michache baada ya wabunge kulituhumu Baraza la Mawaziri kuwa na ubinafsi na kwamba, linabariki mikataba mibovu wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge la Muungano uliotaliwa na kauli kali dhidi ya serikali.

  Madai hayo pia yametolewa katikati ya mjadala mkubwa baina ya matajiri na wanasiasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na watoaji tuhuma, huku baadhi ya mawaziri wakijitokeza kuwatetea watuhumiwa hao.

  Juzi, naibu katibu mkuu wa CUF upande wa Zanzibar, Juma Duni Haji alisema kuwa mawaziri wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete wamewekwa mifukoni na matajiri wachache nchini ndio maana wanashindwa kuwajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi wao.

  Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Zakheim, Mbagala jijini Dar es Salaam juzi jioni, Duni alisema kitendo cha mawaziri wa Rais Jakaya kuingizwa mifukoni mwa matajiri kimeathiri maendeleo ya nchi.

  Ndugu zangu, mawaziri wa Kikwete wote wameingizwa mifukoni mwa matajiri; hawafurukuti na wala hawana kauli mbele ya matajiri hao kwa sababu matajiri hawatawaliki. Wanaotawaliwa ni maskini na wajinga watu wasio na elimu,” alisema Duni ambaye pia ni mkurugenzi wa fedha na uchumi wa chama hicho.

  “Hivi sasa matajiri wachache wanayumbisha nchi, serikali pamoja na chama tawala (CCM). Kila mtu anajua hilo wala halihitaji akili ya ziada kulibaini. Mara (mwenyekiti wa IPP, Reginald) Mengi ni mwanachama wetu mara si mwanachama wetu.

  Alifafanua kuwa, mabadiliko ya Tanzania hayawezi kutokea bungeni bali yataanzia katika ngazi ya jamii, akifafanua kuwa ni mitaa, kata, jimbo, wilaya, mikoa na baadaye taifa.

  “Ndugu zangu kama mabadiliko yanatokea bungeni, wabunge si wanazungumza, kamati si zimeundwa na ripoti si zinatolewa? Kwa nini hakuna mabadiliko bungeni na hata ndani ya nchi,” alihoji Duni akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.

  Alisema hata wabunge wanaopambana na ufisadi “hadi kutokwa na povu mdomoni” kwa sababu ya hasira na uchungu, ndio wanaodaiwa kuwa mabingwa wa kula posho mbili na wengine kufadhiliwa sherehe za harusi zao na mafisadi.

  Duni alifikia wakati kukejeli malumbano baina ya wabunge wa CCM na mawaziri akisema kuwa yanaonyesha kutia wasiwasi kwa anayewateua.

  Alirejea kitendo cha mbunge wa Mtera, John Malecela kumuelezea Waziri wa Utawala Bora, Sophia Simba kuwa ana kichaa baada ya kutoa tuhuma dhidi ya waziri huyo mkuu wa zamani kuwa kinaonyesha kuwepo na matatizo katika uteuzi.

  Hivi kama hivyo ndivyo, yaani Sophia Simba ni kichaa, aliyemchagua atakuwa na hali gani? Jibu mtatoa nyinyi wananchi ambao wengi wenu hadi sasa saa 12:00 jioni hamjajua cha kula, alisema Duni.

  Duni aliwataka wananchi hao kuchukua mfano wa watu wa Kilimanjaro na kwamba, wao waliwekeza katika elimu na uchumi na hivyo kutokubali kutawaliwa ovyo.

  Kilimanjaro lami hadi ******; umeme hadi migombani; shule nzuri zenye sifa za shule bora yote... zote ziko kwao hata vigogo wa nchi hii wengi wao wameoa katika mkoa huo kwa sababu wana maendeleo, alidai Duni.

  Alisema wananchi katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga wanaishia kunywa pombe tu licha ya mikoa yao kuwa na rasilimali kubwa na kwamba, badala yake maendeleo yanayotokana na rasilimali zao yanawanufaisha wengine ambao ni wajanja na waliosoma.

  Aliwataka wananchi hao kutokata tamaa ya kupambana kudai haki zao kwa sababu mwisho wa mapambano ni kufanikiwa, huku akitolea mfano Afrika Kusini ambayo alisema chama cha ANC kilipambana kwa zaidi ya miaka 70 hadi kufanikiwa mwaka 1994.

  Naye mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro amewajia juu viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi akiwataka waungame mbele ya wananchi badala ya kutaka mambo yao yamalizwe ndani ya vikao.

  Kimaro alisema kutumia utaratibu huo ni sawa na Mkristo kuungama mbele ya padri bila waumini wengine kufahamu dhambi zake na kusisitiza kuwa mafisadi lazima watajwe kwa majina.

  Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi wakati akiwapa pole wananchi wa Kijiji cha Goha, Same ambao ndugu zao 24 walifariki dunia baada ya kufukiwa na vifusi vya mlima ulioporomoshwa na mvua.

  Kabla ya kauli hiyo, Kimaro alisema maafa hayo ni ya Watanzania wote na anaungana na mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecela na wananchi wake kuomboleza msiba huo mkubwa.

  Kimaro aliwataka wananchi hao kuungana na kushikamana na mbunge wao ambaye alisema yuko mstari wa mbele kutetea maslahi yao na ya Watanzania wote kwa ujumla.

  “Kilango anapambana na rushwa hadi dunia nzima inamtambua kumpa sifa ya mwanamke jasiri… anapambana na wala rushwa na siku zote anataka watajwe kwa majina, alisema.

  Alisema bungeni si sawa na kanisani kwamba mchungaji akishasema basi, bali ndani ya chombo hicho kinachotawala ni hoja na kuongeza kuwa anaamini mafisadi ni kundi dogo sana ambalo halitaweza kuwayumbisha.

  Wengine wanasema ooh hayo mambo pelekeni kwenye vikao hiyo ni sawa na kuungama mbele ya padri… sisi tunataka waungame na tuwajue wameungama nini ili tuwasamehe, alisisitiza.

  Kimaro aliwataka viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi kutosubiri hadi wafikishwe mahakamani na mahakama kutoa hukumu kwani kitendo cha kuhisiwa tu ni dosari kubwa kiuongozi.

  Ile kuhisiwa tu ni lazima kiongozi uachie ngazi usisubiri hadi mahakamani… kule kuhisiwa tu kunakupotezea sifa ya uongozi na hawa waondoke ili kukipa chama sifa,” alisema.

  Kwa upande wake, Kilango ambaye kabla ya kuzungumza alitembelea eneo la maafa na kuangua kilio kwa dakika 30, aliahidi kujenga mnara wa kumbukumbu katika eneo hilo.

  “Tumelia sana lakini tumwambie Mungu asante… ndugu zetu wamekufa kifo kibaya sana; naomba Mungu anisaidie nijenge mnara wa kumbukumbu tuandike majina yao, alisema.

  Mbunge huyo, mbali na kupeleka misaada mbalimbali kwa wananchi hao, aliamua kupiga kambi eneo hilo kwa siku nne kuwafariji wananchi wake na kuzungumza nao kwa karibu.

  Kilango alipeleka msaada wa chakula, mafuta ya kupikia, sukari na ng’ombe huku mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya akitoa Sh100,000 na Kimaro aliyetoa kiasi kikubwa cha maharage.
  Habari hii imendaliwa na Daniel Mjema, Same, Salim Said na Fidelis Butahe.
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  "Babu Duni" I concur with you here....ni sawa na kusema ufisadi ni system nzima...au kama samaki susuni vile, akioza mmoja basi wote mushkel...kwa hiyo CCM yote imeoza hakuna msafi.
   
Loading...