Elections 2010 Baraza La Mawaziri La Dr. W.P. Slaa Hili Hapa

Katika hizo 10: moja ampe Lipumba nyingine Magufuli.

Hapo vipi?

Kutoka moyoni, natamani Dr. John Pombe Magufuli apewe ukiranja mkuu! Japo yuko chama cha mafisadi. lakini kama katiba itabdilika, akaachia ubunge, afaa sana kuwa PM, naamini combination ya Slaa na JPM Tanzania itazaliwa upya!
 
Hiyo nayo ni hoja nzito!
 
WanaJF;

Si vibaya tukaanza kutoa maoni na mapendekezo yetu hata kuota ni nani ambao wanaweza kufanya team nzuri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mh. W.P. Slaa endapo atashinda uchaguzi mkuu.

Napenda nianze kutoa mapendekezo hayo:

Rais: Mh. Wilbroad P. Slaa

Makamu wa Rais: Said Mzee Said

Waziri Mkuu: Mh. Freeman Mbowe

Mwanasheria Mkuu: Mabere Marando

Waziri Wa Sheria na Katiba: Tundu Lisu

Waziri wa Fedha; Mipango na Uchumi: Mh. Ndesamburo

Waziri wa Miundombinu: Mh. Zitto Kabwe

Waziri wa Ajira; Vijana; Michezo na Utamadubi: Mh. Halima Mdee

Waziri wa Afya; Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto:

Wizara ya Ulinzi; Mambo ya Ndani; JKT na Usalama wa Taifa:

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi:

Wizara ya Kilimo; Chakula; Ushirika; Mifugo; Maji na Umwagiliaji

Wizara ya Ardhi; Makazi; Misitu; Mazingira na Utalii

Wizara ya Mambo ya Nje; Biashara na Masoko:

. . . . .

Naomba sasa wadau muendelee . . . .

Freeman Mbowe apewe wizara ya starehe, na burudani.
 
Hakuna haja ya kuwa na Mwanasheria Mkuu, ambaye ni mbunge kwa nafasi yake, halafu ukawa na Waziri wa Sheria. Mwanasheria Mkuu anatosha na hiyo Wizara ifutwe. Ila sikubaliani na Mabere Marando kuwa Mwanasheria Mkuu. Atafutwe kijana atakayeleta mabadiliko ya maana.
 
naona mmesahau kuwa kwa mujibu wa katiba iliopo Rais wa Jamuhuri ya Tanzania anahaki ya kuteua wabunge Kumi kama ataona inafaa, kama ataona anakosa watu makini na wajuzi wakuendesha serikali anauwezo wakumteua yoyote awe Mbunge, yeye sio Kikwete anaetumia nafasi kumi za Ubunge kuwapa wapuuzi nafasi za uongozi wa kitaifa....rejea Uteuzi wa Kingunge kisha leta hoja yoyote aliyowahi kuijenga Bungeni kwa miaka 5.
Sio kingunge pekee,mbunge mwingine wa kuteuliwa ni Yusufu Makamba ambaye mchango wake katika Bunge ni nini?
 
Siwezi kuendelea mimi labda kama ni la muda! maana Dr Slaa keshasema anabadili katiba na atachagua mawaziri wasio wabunge. Anyway, napenda kuona Nishat na Madini Mh Zitto Kabwe.

Ila alisema kabla ya kubadili katiba atatumia katiba ya zamani, maana yake ni utaratibu ule wa kuteua mawaziri.
 
Aisee...

hili litakuwa moja ya baraza la mawaziri bovu kusikia maisha yangu yote!!! Naona watu wasiozidi watano wanaostahili hapo!

Specifically Mdee, Zitto, Mnyika na yule binti mwingine wa Kigoma.... the rest mmmmhhhh.... Lisu kama mwanasheria siku ile kwenye kampeni anaongea mbele ya waTanzania anamkejeli Waziri Mkuu kwa jina alilopewa na Wazazi wake.... hapana CHADEMA itakuwa chama cha kibabe sana!

Ingawa inasikitisha watu wengine hawajui katiba inasema je kuhusu kuunda baraza la mawaziri specifically kuteua na kupitisha waziri mkuu...

Ni hivi ukishinda urais bila kuwa na wabunge wakutosha utakuwa rais wa muda mfupi sana....

In short ili CHADEMA iunde serikali italazimika kuteua waziri mkuu kutokan CCM. na hii ni mpaka CCM wakubali.
 
Katika hizo 10: moja ampe Lipumba nyingine Magufuli.

Hapo vipi?
Magufuli atambae zake kule atatubania nafasi bure, kiukweli utendaji wake ulitukuka lakini huko aliko kuchafu. Ni sawa na Mrema Lyatonga pamoja na kuwa alifanya kazi nzuri wakati wake lakini sasa hivi huwezi kumdhamini. Kuhusu Mbowe siyo rahisi kuwa PM, mi naona atafaa zaidi kwenye viwanda na biashara, PM atakuwa mtu flani ambaye siyo famous kivile.
 
Aisee...

hili litakuwa moja ya baraza la mawaziri bovu kusikia maisha yangu yote!!! Naona watu wasiozidi watano wanaostahili hapo!

Specifically Mdee, Zitto, Mnyika na yule binti mwingine wa Kigoma.... the rest mmmmhhhh.... Lisu kama mwanasheria siku ile kwenye kampeni anaongea mbele ya waTanzania anamkejeli Waziri Mkuu kwa jina alilopewa na Wazazi wake.... hapana CHADEMA itakuwa chama cha kibabe sana!

Ingawa inasikitisha watu wengine hawajui katiba inasema je kuhusu kuunda baraza la mawaziri specifically kuteua na kupitisha waziri mkuu...

Ni hivi ukishinda urais bila kuwa na wabunge wakutosha utakuwa rais wa muda mfupi sana....

In short ili CHADEMA iunde serikali italazimika kuteua waziri mkuu kutokan CCM. na hii ni mpaka CCM wakubali.

na Tanzania yenye mafisadi Lukuki bila ubabe na umwamba mambo hayaendi, utawala wanchi sio kuchekea wezi, kuwakumbatia, ni upuuzi.
 
Siwezi hata ku-guess. Naweza kufanya hivyo siku moja baada ya Slaa kutangazwa kuwa Rais mteule.
 
Oooh! You are right Mkuu!

In 100 days . . . . ngoja tuendelee kuota tu!

Basi, Mipango, Fedha na Uchumi namweka: Professor Ibrahimu Lipumba . . . .

Hapo mkuu nimecheka sana!!!

Si kuota lazima kieleweke.
 
Back
Top Bottom