Baraza la MAWAZIRI kuwa dogo linapaswa kuwa na mwawaziri wangapi?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Yapo magazeti ambayo yamesifu sana uteuzi wa baraza la mawaziri kivuli la Chadema chini ya uongozi wa Kiongozi wa Kambi ya upinzani Mhe. Freeman Mbowe lakini mawziri wakiwa 29 hivi hilo baraza ni dogo kweli?

Kenya katiba yao yasema mawaziri wasizidi 24 na hakuna nafasi ya mawziri wasaidizi....................................Mbowe amesikika akiahidi kuongeza idadi ya mawaziri wengine labda kuwafurahisha CUF na wengineo........................................

Nionavyo amejibana kuiga baraza la mawaziri kimuundo la JK na hili linasababisha nihoji ubunifu wa Mhe. Mbowe uko wapi?
 
Mbowe atangaza baraza dogo


*Lina mawaziri 29 kutoka CHADEMA pekee
*Wapinzani wengine kufikiriwa baadaye


Na Kulwa Mzee, Dodoma

KIONGOZI wa Kambi ya Upinzania bungeni, Bw. Freeman Mbowe ameteua
Baraza la Mawaziri Kivuli lenye wabunge 29 kutoka CHADEMA ili kutekeleza dhamira ya chama hicho kuwa na baraza dogo.

Bw. Mbowe alitangaza baraza lake la mawaziri jana bungeni na kusema kwamba pamoja na serikali kuwa mawaziri ya manaibu 50, ameteua hao wachache ili waishi kwa vitendo kutokana na kilio chao cha kuwa na baraza dogo la mawaziri.

Alisema kwa kuwa CHADEMA ndiyo iliyotimiza yatokanayo na kanuni ya 14 fasili ya (4) ya kuchagua Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, hivyo ameamua kwa sasa kuunda baraza la mawaziri kivuli kutoka CHADEMA peke yake wakati mazungumzo na wapinzani wengine yakiendelea.

Mbali na yeye atakayeongoza Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Mbowe amemteua Bi. Raya Khamis, (Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu wa Bunge) na Bi. Esther Matiko (Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji). Manaibu waziri katika wizara hiyo ni Bw. Silinde Ernest (TAMISEMI-Utawala) na Bw. Vicent Nyerere (Elimu).

Mawaziri kivuli Ofisi ya Rais ni Bw. Said Arfi (Utawala bora), Mchungaji Israel Natse (Mahusiano na Uratibu), Bi. Suzan Lyimo(Menejimenti ya Utumishi wa Umma).

Bi. Pauline Gekul anakuwa Waziri Kivuli Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Bi. Grace Kiwelu (Mazingira) na Bw. Zitto Kabwe kateuliwa kuwa Waziri Kivuli Wizara ya Fedha na Naibu wake ni Bi. Christina Mughwai.

Wizara ya Mambo ya Ndani aliteuliwa Bw. Godbles Lema, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Tundu Lissu; Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Ezekia Wenje, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Joseph Selasini na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Silvester Kasulumbayi.

Wengine ni Profesa Kulikoyela Kahigi anayeshika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Halima Mdee, Maliasili na Utalii, Bw. Peter Msigwa, Wizara ya Nishati na Madini, Bw. John Mnyika,Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Salvatory Machemuli, Wizara ya Uchukuzi, Mhonga Ruhwanya, Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi. Lucy Owenya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Christowaja Mtinda na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Mbasa Gervas.

Wizara ya Kazi na Ajira, Bi. Regia Mtema, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Naomi Kaihula, Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Bw. Joseph Mbilinyi, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Mustapha Akunaay, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Opulukwa Meshack na Wizara ya Maji, Bw. Highness Kiwia.

Bw. Mbowe alisema pamoja na kutambua kuwa kanuni za bunge zimebadilishwa na kuwa wabunge wote wa upinzani wako chini yake, ameamua kuwateua wabunge wa CHADEMA pekee kwa kuwa bado mawasiliano hayajakamilika na vyama vingine na kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na baraza hilo kwa sasa.

"Ni matumaini yangu kuwa hapo siku za usoni na baada ya kuelewana na kuridhiana na wenzetu, nitaweza kuunda baraza litakaloshirikisha vyama vingine kutoka kambi rasmi ya upinzani bungeni," alisema.

Bw. Mbowe alitoa rai kwa serikali kwamba watendaji watoe ushirikiano kwa wasemaji ili waweze kutekeleza majukumu yao kuimarisha demokrasia.

"Uzoefu unaonesha kuwa wasemaji wa upinzani wamekuwa wakionekana wanoko, vizabizabina na wasio na uzalendo pindi wanapohoji na kukosoa, muono huu uondoke kwani lengo letu sote kujenga nchi iwe na uchumi imara na demokrasia ya kweli kwa ajili ya maendeleo ya watu," alisema.

Aliwapongeza wabunge wa upinzani waliochaguliwa kuongoza kamati za bunge za udhibiti wa fedha za umma na kuwahakikishia ushirikiano wake na baraza lake.

Alipomaliza kutangaza baraza hilo, Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda alisema alichofanya Bw. Mbowe ni kwa mujibu wa kanuni za bunge, na kuwataka wabunge kukubaliana na Kiongozi wa Upinzani na ahadi yake kuwa bado anayo nafasi ya kulibadili na kushirikisha wapinzani wengine kadri atakavyoona inafaa.

Wakati baraza hilo likitangazwa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod alikuwa bungeni kwenye eneo la wageni akisikiliza.

Akimtambulisha Dkt. Slaa, Spika Makinda alisema alikuwa mbunge shupavu na mchapakazi, akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu ya Serikali za Mitaa na kumalizia kuwa 'tutammisi sana kwenye kamati hiyo'.




2 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Chdema ubinafsi utakuwekenipabaya acheni uchu wa madaraka kwa kweli tunakudegemeeni kutuletea maendeleo lakini dalili ya mvua ni..............

sijui tutafikia wapi kwa hali hii kambi ya upinzani inaelekea wapi sasa heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. haya tutaonaaaa..........

February 14, 2011 8:40 PM
blank.gif

Anonymous said... Bora kambi ya upinzani hata iwe na mbunge mmoja kuliko kuwa na wabunge wengi halafu wengi wao ni mamluki, Chadema mko sahihi msije mkaingiza mamluki wakabeba na wengine kuwarudisha CCM, komaeni hivyo Chadema tuko nyuma yenu. Upinzani lazima uwe wa kweli sio wa kinafiki eti ilimradi wapinzani tu ndio wajumuishwe kwenye kambi ya upinzani.
February 14, 2011 9:01 PM
 
Mbowe amtosa Shibuda uwaziri
Tuesday, 15 February 2011 07:12

Israel Mgussi, Dodoma
KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe jana alitangaza Baraza la Mawaziri Kivuli likiwa na mawaziri 29 wote kutoka Chadema, huku akimtosa Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda.Shibuda ambaye aliyehamia Chadema baada ya kutoswa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, ameonekana kuwa na toifauti za kimtizamo dhidi ya chama chake cha sasa hali inayoweza kuwa ndiyo imechangia kutokuwamo kwenye Baraza la Mawaziri Kivuli.

Katika Baraza hilo, Mbowe amewateua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuwa Waziri Kivuli wa Fedha, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kuwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuwa Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Wizara ya Fedha na Uchumi inayoongozwa na Waziri Mustapha Mkullo, ndiyo muhimili wa uchumi wa nchi, ikishughulikia masuala yote yanayohusu mipango na bajeti, wakati Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na Waziri William Ngeleja inabeba uzito mkubwa kwa sasa kutokana na kuwapo kasoro kadhaa za kiuendeshaji ambazo zimekuwa zikigusa sekta zote muhimu za uchumi wa nchi na maendeleo.

Changamoto kubwa katika wizara hiyo ni matatizo makubwa ya uhaba wa nishati ya umeme, ambayo kwa sasa yamesababisha kuwapo kwa mgawo wa umeme wa muda mrefu, huku sekta ya madini ikilaumiwa kwa kutowanufaisha Watanzania na badala yake kuwanufaisha wageni kutokana na udhaifu wa sheria pia mikataba baina ya Serikali na wawekezaji.

Kwa upande wa Mdee, atakuwa ana kwa ana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye alianza kutekeleza wajibu wake katika wizara hiyo kwa kasi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Katika Bunge la Tisa, Mdee alikuwa miongoni mwa wabunge waliopigia kelele uozo katika sekta ya ardhi, kiasi cha kuwataja majina ya baadhi ya viongozi katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam kuwa ni mafisadi kutokana na tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.

Mbowe akitangaza Baraza lake Kivuli jana alisema, anaweza kulifanyia mabadiliko na kuhusisha wabunge wa
vyama vingine vya upinzani wakati wowote na kwamba mabadiliko yatafanyika baada ya wao (wapinzani) kuzungumza na kufikia muafaka.

Katika baraza hilo lililotangazwa baada kipindi cha maswali na majibu, Mbowe mwenyewe anakuwa Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi huku naibu wake akiwa Silinde David Ernest.

Idadi ya Mawaziri Kivuli
Mbowe alisema baraza lake halina mawaziri wengi ili kuonyesha mfano wa kukwepa matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa vitendo."Pamoja na idadi ya mawaziri na naibu mawaziri wa Serikali kuwa 50, uteuzi wangu umeteua wasemaji wakuu na manaibu wasiozidi 29 ili kuonyesha kwa kivitendo, kilio chetu cha muda mrefu cha kuwa na baraza dogo la mawaziri.

Aliwataka viongozi wa Serikali kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wasemaji hao wa Kambi ya Upinzani kwa lengo kujenga nchi na demokrasia ya kweli.

"Ikumbukwe kwamba watendaji wa Serikali hawana vyama na wanahudumia Serikali iliyopo na kuwa tayari kuhudumia Serikali ijayo bila kujali inaundwa na chama gani cha siasa. Uzoefu unaonyesha kuwa wasemaji wa upinzani wamekuwa wakionekana wanoko, vizabinazabina na wasio na uzalendo pindi wanapohoji au kukosoa, ni rai yetu kuwa muundo huo uondoke kwani lengo letu ni kujenga nchi," alisema Mbowe.

Mawaziri wengine kivuli
Kwa mujibu wa Mbowe, Waziri Kivuli katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), amekuwa Raya Ibrahim Khamis, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji amekuwa Esther Matiko huku naibu wake akiwa Vicent Nyerere.

Mbowe alimteua Said Amour Arfi kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mchungaji Israel Natse kuwa Waziri wa Mahusiano na Uratibu, huku Susan Lyimo akiteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Pauline Gekul ameteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Leticia Nyerere Waziri wa Ofisi hiyo akishughulikia mazingira ambapo Zitto Kabwe amekuwa Waziri wa Fedha huku naibu wake akiwa Christina Mughwai.

Godbless Lema amekuwa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Tundu Lissu, Katiba na Sheria, Ezekia Wenje akienda Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Joseph Selasini alipewa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Silvester Kasulumbai akiteuliwa kuongoza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Wengine walioteuliwa na wizara zao katika mabano ni Profesa Kulikoyela Kahigi (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Halima Mdee (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Mchungaji Peter Msigwa (Maliasili na Utalii).

Mhandisi Salvatory Machemuli ataongoza Wizara ya Ujenzi, Mhonga Ruhwanya (Wizara ya Uchukuzi), Lucy Owenya (Viwanda na Biashara), Christowaja Mtinda (Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Dk Gervas Mbasa (Afya na Ustawi wa Jamii).

Pia wamo Regia Mtema (Kazi na Ajira), Naomi Kaihula (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), Joseph Mbilinyi (Habari,Vijana na Michezo), Mustapha Akunaay (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Meshack Opulukwa (Kilimo, Chakula na Ushirika) na Highness Kiwia amekuwa Waziri Kivuli wa Maji.

Shibuda akabwa koo
Wakati Shibuda akitoswa katika Baraza Kivuli, wanachama wa Chadema walio katika Vyuo Vikuu mkoani Dodoma, wamepanga kwenda Ofisi za Bunge leo kwa lengo la kumzuia mbunge huyo kuingia bungeni wakidai ni msaliti.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika sanjari na uzinduzi wa tawi la chama hicho, Mipango, Kata ya Miyuji mkoani Dodoma, walisema kuwa awali walipanga kufanya hivyo jana, lakini kutokana na tukio la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutakiwa kutoa uthibitisho wa madai yake kuwa Waziri Mkuu kuidanganya jamii.

Mwenyekiti wa Tawi la Chadema Mipango, Leonard Toja alisema kuwa mbunge wao Shibuda amewasaliti kwa kuonyesha kuwa bado ana mapenzi na CCM huku akiutaka uongozi wa juu wa Chadema kumwajibisha.

"Tunalaani kauli za Shibuda, ni mamluki anayetimiza malengo yake kwa
kukivuruga chama, viongozi wa Chadema chukueni maamuzi magumu," alisema Toja ambaye pia ni kiongozi wa Baraza la Vijana wa Chadema katika Vyuo Vikuu vya Kanda ya Kati aliposoma risala yao.

Akichangia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita, Shibuda pamoja na
mambo mengine alinukuliwa akizungumzia kuhusu malezi ya vijana akisema vijana wa sasa wanahitaji mwongozo mzuri zaidi wa malezi na kwamba yeye atabaki na maadili aliyojifunza ndani ya CCM aliyosema pia atayapeleka Chadema.

Akizungumza baada ya mkutano wa uzinduzi wa Tawi la Chadema Mipango Kata ya Miyuji, Dodoma, Toju ambaye ni mwenyekiti wa tawi hilo alisema wao kama vijana wa Chadema hawana haja ya malezi anayotaka Shibuda kuyapeleka kwao.

"Yeye allisema anataka kuleta malezi aliyoyapata CCM alete Chadema, malezi ya CCM ayalete Chadema!, hapa hatutaki na sisi tutaandamana Jumanne(leo)
kwenda kumzuia Shibuda asiingie bungeni, " alisema Toju.

Hata hivyo, wakizungumza katika mkutano huo, Lema na Halima Mdee walionyesha mtazamo tofauti kuhusu Shibuda.Wakati Lema akisema kuwa suala hilo lipo ndani ya uwezo wa viongozi wa chama chao, Mdee alisema hakuna haja ya kumfuatilia mbunge huyo na kwamba kama hukumu atahukumiwa na jamii husika.

Hata hivyo, Shibuda mwenyewe hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.
 
"Yapo magazeti ambayo yamesifu sana uteuzi wa baraza la mawaziri kivuli la Chadema chini ya uongozi wa Kiongozi wa Kambi ya upinzani Mhe. Freeman Mbowe lakini mawziri wakiwa 29 hivi hilo baraza ni dogo kweli?

Kenya katiba yao yasema mawaziri wasizidi 24 na hakuna nafasi ya mawziri wasaidizi....................................Mbowe amesikika akiahidi kuongeza idadi ya mawaziri wengine labda kuwafurahisha CUF na wengineo........................................

Nionavyo amejibana kuiga baraza la mawaziri kimuundo la JK na hili linasababisha nihoji ubunifu wa Mhe. Mbowe uko wapi?"


Mh. Ruta:
Mi si mwanasiasa ila ni mfuatiliaji wa mambo ya kisiasa ya nchi kwa sababu ndo yanayofanya mwelekeo wa uchumi wetu. Baraza kivuli la CDM ni dogo kwa mtizamo wangu kwa sababu zifuatazo:
1. Mawaziri vivuli wakishachaguliwa wanakuwa wajumbe wa kamati husika za kudumu za bunge ambazo muundo wake kwa sasa unatakiwa kuendana na muundo wa wizara za JK. Hivyo CDM wamelazimishwa kuunda baraza kivuli lenye mawaziri 29 ili kufit kwenye muundo wa kamati za bunge na kuwa na wasemaji kila wizara.
2. Pia ukilinganisha na baraza la JK lenye mawaziri 50 hao 29 si kupunguza matumizi? Kenya wana katiba mpya na si tukiandika katiba mpya hili litaangaliwa upya ili kupunguza zaidi ukubwa wa baraza la mawaziri.
3. Suala la kuongeza baraza la mh. Mbowe ili kushirikisha vyama vingine nadhani inategemea kama muafaka utafikiwa, na vilevile kiutendaji inawezekana kumtoa mtu ukaweka mwingine na si kuongeza.
WFM.
 
Back
Top Bottom