Baraza la Mawaziri Kenya laundwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Mawaziri Kenya laundwa!

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Indume Yene, Apr 13, 2008.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hatimaye yale mazungumzo kati ya Kibaki na Odinga ya kuunda baraza la mawaziri yamefikia kileleni baada ya kutangazwa kwa baraza la mawaziri. Rais Kibaki akiongozana na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na Waziri Mkuu Mteule Raila Odinga alitangaza baraza hilo kupitia vyombo vya habari akiwa IKULU mjini Nairobi.
  Baraza la Mawaziri ni kama ifuatavyo hapo chini:-

  President: Mwai Kibaki

  Vice President and Minster for Home Affairs: Kalonzo Musyoka

  Prime Minister: Raila Odinga
  Deputy PM and Minster for Trade: Uhuru Kenyatta
  Deputy PM and Minister for Local Governmet: Musalia Mudavadi

  Minister for Internal Security and Provincial Adminstration: Prof George Saitoti
  Asst. Ministers: Orwa Ojode
  Simeon Lesrima

  Minister for Roads: Kiplaya Kones
  Asst. Ministers: Machage, Lee Kinyanjui

  Minister for Public Works: Chris Obure
  Asst. Minister: Dick Wathika

  Minister for Transport: Chirau Mwakere
  Asst. Minister: John Mwau

  Minister for Lands: James Orengo
  Asst. Minister: Sylvester Wakoli and Samuel Rae

  Minister for Energy: Kiraitu Murungi
  Asst. Ministers: Charles Keter and Mohammed Maalim


  Minister for Roads: Kiplaya Kones
  Asst. Minister: Wilfred Machage

  Minister for Special Programmes: Naomi Shaban
  Asst. Minister: Mohammed Ali

  Minister for Gender and Children: Esther Mathenge
  Asst. Minister: Athanus Keya

  Minister for Public Health and Sanitation: Beth Mugo
  Asst. Minister: J Ondicho

  Minister for Medical Services: Prof Anyang’ Nyong’o
  Asst. Minister: Danson Mungatana

  Haya sasa baraza ndilo hilo, mnakaribishwa kutoa maoni.
   
 2. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  At last Wakenya watapona sasa kutoka kwenye vurugu.
  Unaweza pia uka-andika na vyama walivyotoka?
  Lakini hii nayo ni hatua nzuri.
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni progress nzuri!

  Vipi wanakubalika kwa wananchi? Makubaliano ya msingi kati ya vyama vingine...etc yapo..! tusubiri tuone mambo yatakavyoendelea!!
   
 4. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hili baraza bado halieleweki, na ninashangaa jinsi Odinga alivyolikubali. Hivi kiitifaki, nani mkubwa kati ya waziri mkuu na makamu wa rais? Walivyoorodhesha hapo inaonesha makamu wa rais ndiye anayemfuatia rais kimadaraka, lakini huyohuyo makamu wa rais ati ni waziri wa mambo ya ndani! Sasa katika wizara hiyo anayoongoza atawajibika vipi kwa waziri mkuu? Halafu wame-duplicate wizara, mfano "public health and sanitation" na hiyo ya "medical services" zina faida gani kutenganishwa? Labda wenzetu ni matajiri wanazo pesa nyingi za kuhudumia mawaziri wasiokuwa na umuhimu!
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kithuku;

  Fananisha kidogo na Tanzania, Makamu wa Rais ni Makamu kweli wa Rais kwa maana anakuwa active zaidi pale Rais akiwa hayupo! Kwa hakika yupo Juu ya Waziri Mkuu pale Rais anapokuwepo... lakini akiwa hayupo ndio hivyo tena... Lakini ki-protocol Makamu wa Rais yuko juu ya Waziri Mkuu... lakini ki-majukumu I don't see it, Waziri Mkuu wa Kenya ni mtu mzito...


  Kuhusu makamu wa Rais kuwa na wizara anamaanisha kwamba he has to be busy doing something wakati Rais akiwa hana tatizo lolote... Hata kwetu Makamu wa Rais ana wizara ya Mazingira, na Wizara ya Muungano; wale mawaziri wa nchi wanaitwa wasaidizi lakini yeye mwenyewe makamu ndiye waziri wa hizo wizara.

  Lakini Lingine ni kwamba Wale Manaibu waziri wakuu wamepewa pia wizara... hii haina tofauti sana na Tanzania... Tofauti ninayoiona sisi tunasema Waziri wa nchi ofisi ya Waziru Mkuu Tawala za TAMISEMI; kwa maana nyingine kwa system ya Kenya Mzee. Wetu Taisoni ni Naibu Waziri Mkuu...

  Mimi nawapongeza kwa ku-introduce wizara hizi:-:

  Wizara ya Industrilization " wenzetu wanaangalia mbali"

  Wizara ya Nairobi Metropolitan "Majiji kweli yanahitaji kuangaliwa kwa karibu sana kama hili letu linalojengwa kama mtoto anayejifunza kufinyanga vyungu"

  Wizara ya mipango na vision 2030:"Hili pia nimelipenda" at least mpango wa maendeleo wa muda mrefu uko na ownership, una mtu wa kuulizwa... sio unaingiza kwa watu ambao wanafanya operations; eventually wanasahau kabisa mambo ya muda mrefu.


  Zaidi nawasubiri wale wasiopenda wizara nyingi... kwa kuwa Kenya sasa iko na Mawaziri 40 na Manaibu 52. Kazi kwenu watu wa tarakimu... mnaopenda kujadili mambo kwa namba...
   
 6. T

  Tabata-Kisiwani Member

  #6
  Apr 13, 2008
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona Foreign Minister hakuna?
   
 7. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #7
  Apr 13, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Apr 13, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kuna minister wa health, halafu kuna mwingine wa medical services. Halafu minister for home affairs, na mwingine hapohapo for internal security. Ama kweli wenzetu kwa madaraka hamjambo! Nawaona kwa mbali mawaziri watakapokuwa wanakanyagana!
   
 9. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  wale vibaraka walioamua kuviunganisha vyama vyao ndani ya PNU mbona hawajapewa hata wizara fofofo?
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Apr 14, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona Odinga kakubali mwenzake Willium Ruto aliyesota nae pamoja na Najib Balala kukaa nje ya team?

  Halafu nimefagilia Mudavadi kupewa U-deputy na Local governments.

  Sasa hapa mimi sioni Ministry za Finance na pia Tourism.Pia za Culture na pia Justice and constitution.
   
 11. H

  Hume JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Minister for Justice ni Martha Karua,

  Najib Balala ni waziri, nimesahau kidogo wizara yake.
  Nilimuona kwenye list iliyokuwa inaonyeshwa na The CitizenTV!
   
 12. H

  Hume JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Waziri wa Fedha - Amos Kimunya, ameendelea na nafasi yake

  waziri wa Kilimo - William Ruto.
   
 13. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sasa wote wako kwenye serikali, nani atakayekuwa anaihoji serikali?
   
Loading...