Baraza la mawaziri! Hata serikali ya mafisadi inapaswa kuwa na kanuni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la mawaziri! Hata serikali ya mafisadi inapaswa kuwa na kanuni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Mar 13, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Sijui hawa mawaziri wanasumbuliwa na nini?
  Ninavyojua, serikali hata iwe ya kifisadi namna gani, mawaziri huendelea kuwajibika kwa pamoja hata kama wanatofautiana vyama.
  Leo hii unawasikia mawaziri wanaisema serikali kwa kauli zinazopingana mfano Babu wa Loliondo anapigwa stop na waziri wa Afya kisha waziri mwingine anasema haiwezekani kumzuia. Halafu ujue mwana JF, wote wana sababu nzuri tu za kumsaidia mtanzania waliyemfilisi kwa ufisadi.
  Mwingine anaisemea serikali eti wamegundua kuna balozi zinawafadhili CDM kuleta machafuko nchini. Kwa manufaa ya nani? Nchi gani hizo? Haijulikani.
  Kwa nini serikali iliyo makini kiasi cha kugundua yote hayo haijamchukulia hatua hata mhusika mmoja? Mbona inakuwa vigumu kuzitaja nchi?
  Kauli nyingi za binafsi na zinazotofautiana hazitakiwi under serikali moja. Hii ni bila kujali ni serikali ya kifisadi kama yetu au ni ile inayowajibika. Ndiyo maana nasema; Mawaziri wa JK acheni mikurupuko!
   
 2. H

  HAM Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani lazima kwenye ukweli tuseme ukweli, hivi ikibainika zile dawa zinazotolewa na mzee kule Longido zina madhara baada ya miaka mitatu kwa binadamu tutasemaje mbele ya umati, ni vema ikachunguzwa kama haina madhara yoyote ya kiafya siku za baadaye. Na hapa ndio tunasema kila wizara inamsemaji wake kwa maana ya waziri anayeshughulika na Wizara hiyo.

  Kabla utafiti haujafanyika si vema kuwaacha watu wakiendelea kunywa, lamsingi utafiti na vipimo viharakishwe.
   
 3. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wewe! Ninacholaumu ni wao kukosa kauli moja na kuifanya serikali kuwa na mapande mapande kama kifusi cha bomoa bomoa.
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  nafkiri kwa sasa kila waziri ni independent hawawajibiki kokote thats why kila mmoja anaropoka tuu hovyo hovyo tena wakiongozwa na pinda issue za utendaji anaamua kisiasa. Where is collective respondibility? Yani ni kama timu ambayo haichezi kitimu kila mchezaji anadrible kivyake na kukaba kivyake no pasi wala nini kweli itashinda? JK ur cabinet will lead you to destruction
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Waganga wote wa jadi Tanzania wanatoa mitishamba yao bila miti hiyo kuchunguzwa kwanza ubora.
  Wanachanja chale na kuweka dawa zao bila dawa hizo kuchunguzwa.
  Nyembe zao hazichunguzwi.
  hata mikono yao wengine hawanawi.
  Pamoja na yote hayo sijawahi kusikia serikali ikitaka kuanzisha zoezi la kupima dawa za waganga hawa wa jadi.

  Kwa nini Ghafla inakuwa Noma kwa Babu kutoa Dawa??
  Kwa vile kasema anatibu Ukimwi??
  Angesema anatibu Nguvu za kiume serikali ingeaagiza dawa zipimwe??

  DOUBLE STD? KUJIKANYAGA? AU NINI?
   
 6. J

  Joblube JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tatizo lao ni waongo na hawajui kanuni za uongo. Kanuni ya uongo ni kuwa ukiwa muongo usiwe msahaulifu utakutaunajipinga mwenyewe.
   
Loading...