Baraza la mawaziri chaka la mafisadi?

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Tumeendelea kushuhudia sakata la ufisadi likilitafuna baraza la mawaziri la rais Kikwete tena ndani ya kipindi kifupi kisichozidi miezi miwili.

Baada ya Waziri mkuu Lowassa,waziri Karamagi na waziri Msabaha kuachia ngazi juzi usiku ilikuwa ni zamu ya waziri Andrew Chenge.

Chenge amejiuzulu kutokana na tuhuma za kuhusika katika sakata la ununuzi wa rada ya mabilioni huko uingereza,ununuzi ulioelezewa kuwa ulikuwa umegubikwa na faulu nyingi.

Matukio haya yote yanatuacha na maswali kibao kuhusu hatma ya siasa za Tanzania.Wakati Kikwete anaingia madarakani tulijua tatizo la rushwa litapungua lakini tumeshuhudia katika nusu ya kipindi chake cha uongozi mawaziri na watendaji wengine wengi wakituhumiwa kwa ufisadi.

Hata baraza lililopo sasa bado lina watu ambao wananchi na wachunguzi wa mambo wanadai siyo safi.Mengi yalisemwa kuhusu chenge lakini Kikwete akaziba masikio,matokeo yake ndiyo haya.

Ukichunguza kwa undani utagundua kuwa mawaziri wengi waliopo sasa ni wafanyabiashara wakubwa lakini biashara zao haziko wazi.Kuna uwezekano mkubwa kuwa wapo wengine ambao kwa njia moja ama nyingine wanahusika na matatizo haya kwa kuwa wamekuwepo serikalini tangu awamu ya tatu ambapo ndipo mikataba mingi mibovu na ufisadi uliokithiri ulitendeka.

Hakukuwa na haja kwa Kikwete kurejesha sura hizo katika baraza hasa kwa kuwa wengi walionesha kutokuunga mkono.

Naona ipo haja sasa ya kuwa wakweli na kuanika peupe ukweli kuhusu baraza letu.Tumsaidie rais kwa kumwonesha kama kweli baraza la mawaziri ni kichaka cha mafisadi kwa kuendelea kuwaumbua watafuna nchi.

Naye JK anatakiwa kusoma alama za nyakati,wananchi wamechoka na wanataka kuona uongozi ukiheshimiwa hivyo asikie sauti ya wengi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom