Baraza la Madiwani (CCM) lakumbwa na kashfa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kahama. Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya ya Msalala wilayani Kahama, limekumbwa na kashfa baada ya wananchi kulituhumu kwa rushwa.

Wakazi hao wa kata 10 kati ya 18 zinazounda Halmashauri hiyo, wameiomba ofisi ya Rais (TAMISEMI) kulivunja.

Wanadia kuwa rushwa imeshamiri hasa katika mgogoro wa ujenzi wa makao makuu yaliyoidhinishwa na Serikali yajengwe eneo la Busangi.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, John Mongella, walisema makao hayo yaliyojengwa katika Kata ya Ntobo hayakuwa makubaliano na kwamba, yalitakiwa kujengwa Kata ya Busangi.

Walimtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kulivunja kwa madai limejaa rushwa iliyokwamisha ujenzi wa makao hayo katika eneo walilokubaliana awali.

Mgogoro wa kupinga ujenzi huo ulianza tangu mwaka 2012 na hakukuwa na msimamo maalumu wa kata husika itakayojengwa makao hayo na mara ya mwisho walikubaliana yajengwe Kata ya Ntobo.
 
Kumbe mgogoro ni wa kugombania makao makuu ya wilaya! Sasa hapo tuhuma za rushwa ziko wapi?
 
mkuu,nadhani kuna eneo makao makuu ya wilaya ilibidi yajengwe,ila kuna watu wakawa tembezea fedha madiwani wapindishe maazimio,na hivyo ujenzi wa makao makuu ukaenda kwengine
 
wanashangaa CCM kula rushwa?! watakuwa wageni nchi hii hao. CCM na rushwa ni kama kichwa na nywele hata ukinyoa kipara zitaota tu, hata wakibadilisha wana CCM tabia zao ni zilezile tu. Wawakatae waishi kwa amani.
 
wanashangaa ccm kula rushwa?! watakuwa wageni nchi hii hao. ccm na rushwa ni kama kichwa na nywele hata ukinyoa kipara zitaota tu, hata wakibadilisha wana ccm tabia zao ni zilezile tu. Wawakatae waishi kwa amani.
Yale yale ya Nzi na KINYESI
 
Kahama. Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya ya Msalala wilayani Kahama, limekumbwa na kashfa baada ya wananchi kulituhumu kwa rushwa.

Wakazi hao wa kata 10 kati ya 18 zinazounda Halmashauri hiyo, wameiomba ofisi ya Rais (TAMISEMI) kulivunja.

Wanadia kuwa rushwa imeshamiri hasa katika mgogoro wa ujenzi wa makao makuu yaliyoidhinishwa na Serikali yajengwe eneo la Busangi.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, John Mongella, walisema makao hayo yaliyojengwa katika Kata ya Ntobo hayakuwa makubaliano na kwamba, yalitakiwa kujengwa Kata ya Busangi.

Walimtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kulivunja kwa madai limejaa rushwa iliyokwamisha ujenzi wa makao hayo katika eneo walilokubaliana awali.

Mgogoro wa kupinga ujenzi huo ulianza tangu mwaka 2012 na hakukuwa na msimamo maalumu wa kata husika itakayojengwa makao hayo na mara ya mwisho walikubaliana yajengwe Kata ya Ntobo.
Jana na leo naona unato vichwa vinatofautiana na habari yenyewe. Kichwa kinakadia CCM habari inaeleza mafanikio na misimamo imara ya viongozi wa CCM kuchagiza maendeleo.
Kweli CHADEMA mmechoka na sasa mnaleta viroja. Hapa mnanikumbusha zile nyimbo za Omary Mkali pale shoga analia konda kamtukana. Alipoambiwa naye atukane unajua alisemaje, likonda hiloo!! Ndio haya mwanachadema huyu anatuletea
 
Kumbe mgogoro ni wa kugombania makao makuu ya wilaya! Sasa hapo tuhuma za rushwa ziko wapi?
Utaonaje mzee wa buku 7? kumbe hujui manufaa ya eneo likijengwa makao makuu ya wilaya?? Haya kosoa tena uongezewe buku 7 ingine
 
Back
Top Bottom