Baraza la Madiwani Bukoba, lamtoa jasho Waziri Kagasheki

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Katika kikao cha madiwani leo mjini Bukoba, Balozi Kagasheki (Mbunge Bukoba Mjini) amejikuta hana diwani anayemuunga mkono alipotaka mpango wa kubomoa soko kuu la Bukoba ucheleweshwe. Madiwani wote wamesema soko libomolewe lawama baadaye.

HOFU YA KAGASHEKI NI KUWA ENDAPO SOKO LIKIBOMOLEWA NA KUMALIZIKA KWA WAKATI LITAPANDISHA CHATI YA MEYA WA MANISPAA DOKTA ANATORY AMAN AMBAYE ANAWEZA KUWA TISHIO KWAKE KTK UCHAGUZI MKUU UJAO.

attachment.php
 

Attachments

  • KAGA.jpg
    KAGA.jpg
    16.9 KB · Views: 435
Mshenzi tu huyo ..tena yule dr. ni wa ukweli sana mpeni huyo kazi
 
Nilitarajia Bkb mjini chini ya Kagasheki wangekwisha jenga soko jipya,stand kuu ya mabasi na kuimarisha miundombinu kumbe kinyume chake Kagasheki amegeuka kikwazo cha maendeleo kama alivyokuwa Meya wa zamani mzee Luhangisa.
 
Kagasheki kamjenga sana Amani uchaguzi uliopita na hii ni kwa sabbu Amani alikuwa na kundi lake lenye nguvu ndani ya ccm ili kwa pamoja wapambane na chadema na Rwakatare ambaye ana ushawishi mzito kwenye siasa bkb

Ukiangalia kwa wakati huo ilikuwa sahihi kwasabbu Rwakatare na Chadema yake alikuwa anawapumulia shingoni, na kibaya zaidi siasa za bkb 2010 ziliharibiwa na udini toka CUF baada ya Rwakatare kuhamia cdm, kwahyo baadhi ya waislam hasa viongozi wa CUF wakapiga kampeni mbaya dhidi ya Rwakatare kwamba amehama CUF kwasbbu ya udini ili aongeze nguvu kampeni za dr slaa mkristo na kuamua kumuunga mkono mgombea wa ccm ambaye ni mwislam mwenzao.

Amani ni mkristo kwahyo ili kubalance kagasheki akakubaliana na amani wawe karibu akiahidi kumsapoti umeya wa bkb mjini. Lakini sasa ni dhahiri wataingia kwenye vita maana wote ni wapenda sifa, na kila mmoja atataka aonekane ni mchapa kazi kuliko mwenzake, hasa ukizingatia amani ana kiu ya muda mrefu ya ubunge..hofu yangu siasa za udini zilizoingizwa na kushadadiwa sana 2010 bkb mjini zinaweza zikatoa matunda machungu 2015! wacha tusubiri muda utasema mengi!
 
huyu kagasheki ni mpuuzi wa kutupwa,ona anahujumu maendeleo kwa sababu za kisiasa,hii mipango ni ya kitambo sana mkuu
 
Ivi kagasheki yupo nchini.,kama nlimuona akikwea pipa KIA juzi kwenda Unyamwezini
 
KAUDO vipi kuhusu stand kuu wanasemaje ama ndo ishu za kagasheki anaendelea na siasa zake za kifara ...tupe nyuzi mkuu.
 
Mimi siasa za bukoba uwa sizpend, ziko complicated sana, kuna unafiki pia majungu pale bkb, nadhani chadema ijipange vizuri ituokoe kwani mji wetu unabaki nyuma kila kukicha.kisa kuendekeza majungu, chonde chonde, tnaitaji damu mpya maana rwangisa bado anapamezea mate na uzee wote ule
 
kweli vijana tuna wajibu wa kutimiza wajibu kwa ajiri yetu na watoto wetu,hawa wazee wachawi wanatuharibia mkoa wetu
 
Katika kikao cha madiwani leo mjini Bukoba, Balozi Kagasheki (Mbunge Bukoba Mjini) amejikuta hana diwani anayemuunga mkono alipotaka mpango wa kubomoa soko kuu la Bukoba ucheleweshwe. Madiwani wote wamesema soko libomolewe lawama baadaye.

HOFU YA KAGASHEKI NI KUWA ENDAPO SOKO LIKIBOMOLEWA NA KUMALIZIKA KWA WAKATI LITAPANDISHA CHATI YA MEYA WA MANISPAA DOKTA ANATORY AMAN AMBAYE ANAWEZA KUWA TISHIO KWAKE KTK UCHAGUZI MKUU UJAO.

attachment.php

Wa Tz tusivyokuwa na kawaida ya kuona mbali - soko kuu litavunjwa kabla ya kuhakikisha biashara iendeshwayo hapo itahamia wapi - hata kama ni kwa muda wa wakati wa ujenzi. Hao madiwani wangekuwa ni kweli wanajua wajibu wao na wana uwezo kuona mbele wangeanzia na ujenzi wa masoko yafuatayo Kashai/Mafumbo, Rwamishenye/Kiteyagwa na Kibeta/Ibura. Hayo masoko matatu yangepunguza pressure kwenye soko kuu na kusogeza shughuri/huduma za soko karibu na walaji.
Ilivyo sasa soko kuu la bukoba haliwezi kupanuliwa - tukiangalia mazingira ya afya lilitakiwa lipunguzwe ukubwa wake.
 
barumuna bange kiki bojo ntujurangana emyenda omumbaga? Ntushaira owa,abanyamahanga? Akawe kawe kajunda nokara banyakutura,ebyaitu tubimalire bukoba.
 
Ndo ubovu wa wabunge wetu,wanajua kucheza na siasa za sifa,wanasahau matatizo ya wananchi wake! BIG up kwa MAGUFULI PALE CHATO!
 
Juzi nilibahatika kupita Bukoba lakini nilishangaa kuambiwa kuwa halmashauri ina mpangomwa kulibomoa soko kuu la mjini Bukoba na kujenga soko jipya mahali pale pale.
Kwa jinsi mji unavyoendelea kupanuka lile eneo la soko ni finyu sana halifai na haliwezi kupanuliwa zaidi,halina hata sehemu yakutosha kwa ajili ya maegesho ya magari ya wateja achilia mbali magari yanayoleta nafaka.
Sijui kwa nini madiwani hawakutafuta sehemu nyingine inayoendana na ukuaji wa mji husika lakini kama ilivyoelezwa hapo juu mipango inafanyika kuwanufaisha watu kisiasa hapo hakuna mipango miji inayofuatwa maana hata upanuzi wa uwanja wa ndege uliamliwa kisiasa ukiangalia uwanja ulivyopanuliwa unaenda sambamba na shule za msingi mbili ni bahati kuwa ndege zinazotua hapo si nyingi lakini pamoja na uchache wake wanafunzi wanadhilika na kelele za ndege.
Kwa ufupi uwanja wa ndege soko kuu na stendi ya mabasi vinapashwa viamishiwe sehemu inayojitosheleza nje ya mji.
 
Back
Top Bottom