Baraza la Madiwani Arusha lamjibu RC Gambo

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
BARAZA la Madiwani wa halmshauri ya Jiji la Arusha linalomaliza muda wake limesema kuwa halikuwa na mgogoro wowote na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, katika kutekeleza majukumu yake na halina uwezo wa kutokutekeleza maagizo yanayotolewa na mkuu huyo wa mkoa kwa kuwa ndie mlezi wa halmashauri zote za mkoa .

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji wa halmashauri hiyo ambae pia ni mjumbe wa kamati ya fedha,Diwani Ally Bananga, alipokuwa akitoa ufafanuzi kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika ukumbi wa shule ya msingi Arusha.

Ameliambia baraza hilo kwamba wiki iliyopita mkuu wa mkoa alitoa maelekezo kwenye maeneo manne kwa halmashauri hiyo ikiwemo kumaliza mgogoro ulioibuka katika msikiti mkuu wa Ijumaa mkoa wa Arusha, na kushughulikia mgogoro wa kanisa na shule ya msingi Terati, pamoja na migogoro mingine ya ardhi .

Bananga,amesema maagizo hayo yalikuwa yanaendelea kufanyiwa kazi na halmashauri ambapo kwa sasa yamefikia kwa ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya utekelezaji.

Diwani huyo amesema kuwa baraza linapokea maelekezo ya mkuu wa mkoa na kuyapeleka kwenye vikao vya baraza hilo kwa ajili ya maamuzi na utekelezaji hivyo wao hawampingi na wala hakuna ushindani.

Amesema kauli iliyotolewa na mkuu wa mkoa kwamba kuna viongozi wanatunishiana misuri na hivyo halmashauri kushindwa kutekeleza maagizo anyoyatoa,Bananga amesema hizo ni chuki binafsi kati ya mkuu wa mkoa na wateule wa rais kwenye ngazi ya halmashauri na wilaya lakini baraza halina msuguano wowote hivyo kama ni mgogoro binafsi asiihusishe halmashauri .

Amesema anamshangaa mkuu huyo wa mkoa kuituhumu halmashauri na kusema kuwa tuhuma hizo hazina msingim,na tatizo ni mkuu wa mkoa ambe mawasiliano kati yake na halmashauri yamekatika na ameshindwa kuhudhuria mara kwa mara vikao vya baraza hilo

Katika hatua nyingine,baraza hilo limempongeza Gambo kwa kusaidia ujenzi wa shule ya bweni ya Mrisho Gambo,iliyopo kata ya Olasti badala ya shule hiyo kuwa ya kutwa kama ilivyokuwa imekadiriwa hapo awali.

Kwa upande wake Diwani Ephata Nanyaro, Amesema kauli ya mkuu wa mkoa ni maelekezo na kama lipo jambo lina masilahi binafsi sio ajumuishe watu wote bali anapaswa kulitatua kiubinafsi na kamwe asiwahusishe wote kwa kuwa linazorotesha maendeleo

Ametolea mfano soko la NMC lilipoungua mwezi uliopita halmashauri ilitenga bajeti kwa ajili ya kulijenga liwe la kisasa lakini mkuu wa mkoa alikataa na akaamuru wafanyabiashara kurejea na kuendelea na shughuli zao
 
Back
Top Bottom