Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), muda umefika sasa

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,918
1,993
Wakati klabu ya AS Roma inatoa salamu za pole kwa Watanzania kwa kutumia lugha ya Kiswahili, Wabongo wengi tulikuwa na hamu ya kujua ni Mtanzania gani mwenzetu alopewa hilo shavu uko Rome Italy.

Ajabu wadukuaji wakatudukulia; Mkenya ndio amekamatia hiyo nafasi, mimi kama mimi nikaanza kuwaza kwanini Wakenya kila tunda analotakiwa kula Mmbongo wao wanatupiga gepu? Nkaona baraza nina jambo nao la kuteta na sina uwanja mwengine zaidi ya huu.

Baraza la Kiswahili mna maeneo mengi ya kujifunzia, mfano tu wenzenu wa madini walishaamka na Tanzanite leo inajulikana inatoka Tanzania. Bodi ya utalii nayo ni mojawapo ya mfano bora, ndugu zetu hawa waliudanganya ulimwengu miaka mingi kuhusu mlima Killimanjaro, leo hii bodi imesimama kidete ulimwengu umeanza kujua huu mlima upo kwetu.

Na nyie basi nawaomba shirikianeni au kama mnashirikiana basi zidisheni juhudi kupitia balozi zetu zote ulimwenguni kukamata hizi tenda za ualimu wa Kiswahili. Ni muda wa Wakenya kuwaonyeshea kuwa sasa watanzania tumechoka kuchezewa, tusake hizo nafasi kwa udi na uvumba.

Binafsi nina ndugu yangu ana miaka zaidi ya 3 au 5 yuko mtaani na anayo shahada ya mambo hayo ya lugha; ameipatia pale Chuo Kikuu Dodoma lakini nani wa kumpa connection kama sio nyie kuwatafutia masoko huko nje.

TFF wamekuza soka la bongo
BASATA nao wanalo la kujisifia maana wasanii wako chini yao
Bodi ya Utalii naipigia saluti kama Brother K
Vyama vya ngumi pia saluti
Riadha pia saluti kwao kiaina

Nyie ndugu zangu mna kazi kubwa bado sio tu kuishia Radio One japo sio vibaya inasaidia lakini naona bado kama kweli tumepania kuikuza lugha hii kimataifa. Jukumu letu la kwanza liwe kuwapoka hawa jamaa fursa zote za kufundisha Kiswahili ulimwenguni. Sisi hatuna ugomvi nao kuja kutufundisha Kingereza nchini kwetu lakini Kiswahili watuachie wenyewe wajuvi.

Mamalka ya anga nawapa big up kwa kuonyesha tunahitaji heshima yetu pia.
 
Hilo Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) linapaswa liundwe upya ama lifanyiwe maboresho makubwa katika rasilimali watu, kimuundo, kimajukumu, kisera, kimtazamo na mengineyo mengi. Vinginevyo tutaendelea kunung'unika tu.
 
SAUTI YAKO,

Suala sio kuongea tu naomba uulize Bakita kwenye bajeti ya taifa inatengewa shilling ngapi kwa mwaka? Kuuza au kupromote lugha kimaitafa kunahitaji pesa sio maneno au utashi, Wakenya wataendelea kutupiga katika utalii kiswahili riadha nk kwasababu wavipa kipaumbele na wanatenga pesa kwelikweli. Sisi pesa yetu nyingi tunaiweka kwenye kujenga flyover nk.
 
Walisema watu waliosoma kiswahili ngazi ya shahada watu majina yao, miaka inakatika kimya, hawana wanachokinyafa hao.
 
Mkuu, kwani inabidi wafanye nini hasa. Mimi ninaona unajambo nzuri la kujenga lakini haujalitoa. Ni vema ukasema sasa hilo baraza lifanye nini ili tutoboe, yaan uwaeleze mbinu gani wazitumie ili tutoboe na kuwafunika Wakenya.
 
SAUTI YAKO,

Hivi hujui? Kuna msemo unasema: ''Kiswahili kilizaliwa Tanzania, kikakulia Kenya na kikafia Uganda''. Huu msemo mimi nakubali upo sahihi: Kenya sasa hivi wanajitahidi sana kuongea kiswahili fasaha kulinganisha na Tanzania. Tanzania kiswahili kimeshaharibiwa na wengi hata kuandika hawawezi bali ni kukariri makosa. Mfano ni wewe hapo umeandika ''Mimi kama mimi.....'' Hivi kama siyo kukariri haya maneno yana maana gani? Kwani kuna ''Wewe kama siyo wewe'' na wewe kama wewe''?
 
Mkuu, kwani inabidi wafanye nini hasa. Mimi ninaona unajambo nzuri la kujenga lakini haujalitoa. Ni vema ukasema sasa hilo baraza lifanye nini ili tutoboe, yaan uwaeleze mbinu gani wazitumie ili tutoboe na kuwafunika Wakenya.
Nadhani Cha kufanya wanakijua,Mimi nawasitizia tu,Kama kweli mkuu wa nchi alitumia Kiswahili alivyoketi na wakuu wa nchi sadc,sidhani Kama atashindwa kuwatengea fungu bakita kuikuza lugha yetu.Mi nadhani wao ndio waombe Rais awasaidiaje
 
Back
Top Bottom