Baraza la Kiislamu la Maadili lalaani kuzomewa Dk Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Kiislamu la Maadili lalaani kuzomewa Dk Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dudus, Jan 8, 2012.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 6,029
  Trophy Points: 280
  Baraza la Maadili la Kiislamu Tanzania, limelaani kitendo cha kuzomewa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kilichofanywa na baadhi ya wakazi wa Kigamboni, huku likiwaonya pia wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kumshambulia waziri huyo, kutokana na uamuzi wake wa kuongeza nauli ya huduma ya kivuko cha Magogoni-Kigamboni.

  Tamko hilo lilitolewa na Baraza hilo kupitia Mwenyekiti wake, Sheikh Athuman Mkambaku jana.

  Alisema hawana budi kutoa tamko kila wanapoonza maadili yanakiukwa na baadhi ya watu katika jamii, hivyo akasema wakazi hao hawakustahili kumfanyia kitendo hicho Waziri Magufuli kwani uamuzi wake wa kuongeza nauli ya huduma hiyo ulifanywa kwa kuzingatia sheria za nchi.

  "Hivyo, Baraza linalaani kitendo kilichofanywa na wakazi hao wa Kigamboni wasiostaarabika cha kumzomea Waziri Magufuli," alisema Sheikh Mkambaku.

  Alisema Baraza limeridhika na maelezo yaliyotolewa na waziri huyo kuhusu sababu zilizofanya kufikia uamuzi huo, ambazo ni kupanda kwa gharama za uendeshaji, ikiwamo bei ya mafuta.

  Sheikh huyo alisema sababu hizo haziwezi kupuuzwa na ndio maana vyombo vyote vya usafiri kuanzia ule wa anga, nchi kavu na majini, vimeongeza nauli na kuhoji iweje leo ionekeane ni ajabu kwa kivuko cha Kigamboni?

  Alisema kitendo cha wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam kuungana na kumshambulia Wazuiri Magufuli ni cha kinafiki na ajenda ya siri dhidi yake kwa kuwa kuna vitu vingi, ambavyo bei zake imependa Dar es Salaam, kama vile nauli za mabasi ya mikoani, daladala na umeme, lakini hawajaonekana wakiungana na kumshambulia waziri yeyote mwenye dhamana.

  "Ina maana vitu vyote vilivyopanda bei hapa Dar es Salaam ilikuwa ni sahihi kasoro nauli ya kivuko tu? Maandiko matakaifu yanasema unawezaje kutoa kibanzi katika jicho la mwezio na ile boriti iliyoko katika jicho lake usiitoe? Mnafiki wewe." Alisema Sheikh Mkambaku.

  Aliongeza: "Kwa mfano, wakazi wa Kiluvya walioko katika Jimbo la Ubungo wanalipa nauli Sh. 900 kutoka Kiluvya hadi Ubungo wakati wakazi wa Mbagala wanalipa Sh 450 kutoka Mbagala hadi Mwenge. Iweje Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akawatetee wakazi wa Kigamboni wanaolipa Sh. 200 badala wapigakura wake ambao hulipa Sh 1,200 kutoka Kiluvya hadi Posta. Je, huo sio unafiki?"

  Alimpongeza Waziri Magufuli kwa uchapakazi hodari unaodhihirisha kwa vitendo kwamba analipenda taifa na kusema laiti kama serikali ingelikuwa na mawaziri watano wachapakazi mfano wake, nchi isingetafunwa na mafisadi, hivyo akawataka Watanzania kumuunga mkono na kumtia moyo badala ya kumkatisha tamaa.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Naombeni kujua Waislam wana mabaraza mangapi? Je ni ya dhehebu moja au madhehebu tofauti?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Makubwa! Nilikuwa sijui nini kiko nyuma ya hili sakata. .Naanza kuona mwanga taratiiibu
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Kuna utitiri wa mabaraza, foundations, n.k ila linalotambulika kama wawakilishi wa waislamu ni BAKWATA.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo katika wabunge woote waliokuwepo wamemuona Mnyika tu?

  Kweli inadhihirisha kilichopo nyuma ya pazia!
   
 6. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hebu waache unafiki, lengo lao ni kumsema Mnyika tu.
   
 7. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  CCM ina matawi mengi sana tofauti na nilivyofikiria
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145


  strong point!
   
 9. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ukubwa wa jimbo la ubungo mpaka mbagara?
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni kama makanisa tu yalivyokuwa utitiri hasa mbeya kuna makanisa mengi sana!sheria inaruhusu mkiwa kumi tu mnaweza kuanzisha kanisa!
   
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,300
  Trophy Points: 280
  Hata nalo pia sio wote tunaolitambua,
  Wengine tunaliona kama la kizushi tu!!!
   
 12. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kwa mara ya kwanza naona taasisi ya kiislamu ikiongea cha maana! Na kwa upande mwingine wameonesha kuwa disappointed na Mnyika kwani waliexpect much from him.
   
 13. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanayo pointi juu ya hili. Nawapongeza kwa 100% Ukweli maisha ni magumu kila mahali kwa kila kitu, hata New York USA, muulizeni William Malecela atawafafanulia. Kikubwa tuwe creative ktk kutafuta na kuanziasha miradi.
   
 14. K

  Konya JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa sijui hata wanasimamia upande upi,inavyoonekana wanalao jambo ni mda tu nafikiri..
   
 15. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0


  Mkuu naulizia mabaraza ya Waislam silizii idadi ya makanisa......au makanisa ni mabaraza kama ya hao wazee wa matamko!
   
 16. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 6,029
  Trophy Points: 280
  Strong point? Sijui ni kigezo gani katumia huyo Shehe kulinganisha nauli ya Kiluvya na Ferry! Ni umbali? Ni aina ya usafiri? au ni kitu gani alichotumia kufikia conlusion yake?

  Kiluvya - Ubungo ni zaidi ya 30km wakati Kivukoni A - Kivukoni B haifiki 1km anyway let's assume its 1km.

  Hesabu rahisi (Nauli kwa kilometa):

  Kiluvya - Ubungo: 900/30 = T.Shs. 30/km.

  Kivukoni A - Kivukoni B: 200/1 = T.Shs. 200/km.

  Kwa akili yako na ya Shehe ni nauli ipi ghali? Kiluvya-Ubungo au Kivukoni? Jamani, just use common sense! Otherwise, tuambiwe ni kigezo kipi kimetumika. Naamini wananchi wakiambiwa kwa busara na ufafanuzi wa kueleweka hata kama itakuwa 10,000/= bado wataelewa na sio kwenda kuwatusi.
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  No wanahoji vitu vya msingi msiwadharau,mfano hiyo hoja ya mnyika kuacha kuwatetea wapiga kura wake wa kiluvya na nauli ya shs 900 mpaka ubungo tu hapo hatuhesabu watakayolipa kufika kariako au mwenge au posta,badala yake anaenda kupanda panton,ubungo kuna panton?pia kwanini mnyika hatujawahi kumsikia akipinga kiingilio cha pale ubungo bus terminal?kwanini anaonekana kuguswa zaidi na watu wa kigamboni?hapa kuna kitu kimejificha,nadhani ni uendeshaji wa kile kivuko ndio unawaumiza kichwa,kuna mtu anawasukuma wabunge wetu wampe kivuko akiendeshe!
   
 18. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ili hayo mabaraza lukuki yapate heshima yajishughulishe na issue za kitaia na yaache kutumiwa na magamba kuichafua chadema
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Naona unachanganya mambo kwa uvivu wa kusoma,sheikh hajalinganisha nauli ya kuvukoni A Tto kivukoni B na nauli kiluvya bali kalinganisha 450 inayolipwa kutoka mbagala kwenda mwenge na 900 inayolipwa kutoka kiluvya mpaka ubungo,tujenge tabia ya kusoma thread sawasawa kabla ya kukurupuka kuwatetea tunaowapenda!

   
 20. M

  Makupa JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hawa mashehe kama kweli wana uchungu na ufisadi basi watoe tamko la kulaani uporaji wa nyumba za serikali ulioasisiwa na Magufuli
   
Loading...