Baraza la Kiislamu la Maadili lalaani kuzomewa Dk Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Kiislamu la Maadili lalaani kuzomewa Dk Magufuli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jan 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  [h=2][/h]












  [​IMG]
  Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli


  Baraza la Maadili la Kiislamu Tanzania, limelaani kitendo cha kuzomewa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kilichofanywa na baadhi ya wakazi wa Kigamboni, huku likiwaonya pia wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kumshambulia waziri huyo, kutokana na uamuzi wake wa kuongeza nauli ya huduma ya kivuko cha Magogoni-Kigamboni.

  Tamko hilo lilitolewa na Baraza hilo kupitia Mwenyekiti wake, Sheikh Athuman Mkambaku jana.

  Alisema hawana budi kutoa tamko kila wanapoonza maadili yanakiukwa na baadhi ya watu katika jamii, hivyo akasema wakazi hao hawakustahili kumfanyia kitendo hicho Waziri Magufuli kwani uamuzi wake wa kuongeza nauli ya huduma hiyo ulifanywa kwa kuzingatia sheria za nchi.

  “Hivyo, Baraza linalaani kitendo kilichofanywa na wakazi hao wa Kigamboni wasiostaarabika cha kumzomea Waziri Magufuli,” alisema Sheikh Mkambaku.

  Alisema Baraza limeridhika na maelezo yaliyotolewa na waziri huyo kuhusu sababu zilizofanya kufikia uamuzi huo, ambazo ni kupanda kwa gharama za uendeshaji, ikiwamo bei ya mafuta.

  Sheikh huyo alisema sababu hizo haziwezi kupuuzwa na ndio maana vyombo vyote vya usafiri kuanzia ule wa anga, nchi kavu na majini, vimeongeza nauli na kuhoji iweje leo ionekeane ni ajabu kwa kivuko cha Kigamboni?

  Alisema kitendo cha wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam kuungana na kumshambulia Wazuiri Magufuli ni cha kinafiki na ajenda ya siri dhidi yake kwa kuwa kuna vitu vingi, ambavyo bei zake imependa Dar es Salaam, kama vile nauli za mabasi ya mikoani, daladala na umeme, lakini hawajaonekana wakiungana na kumshambulia waziri yeyote mwenye dhamana.

  “Ina maana vitu vyote vilivyopanda bei hapa Dar es Salaam ilikuwa ni sahihi kasoro nauli ya kivuko tu? Maandiko matakaifu yanasema unawezaje kutoa kibanzi katika jicho la mwezio na ile boriti iliyoko katika jicho lake usiitoe? Mnafiki wewe.” Alisema Sheikh Mkambaku.

  Aliongeza: “Kwa mfano, wakazi wa Kiluvya walioko katika Jimbo la Ubungo wanalipa nauli Sh. 900 kutoka Kiluvya hadi Ubungo wakati wakazi wa Mbagala wanalipa Sh 450 kutoka Mbagala hadi Mwenge. Iweje Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akawatetee wakazi wa Kigamboni wanaolipa Sh. 200 badala wapigakura wake ambao hulipa Sh 1,200 kutoka Kiluvya hadi Posta. Je, huo sio unafiki?”

  Alimpongeza Waziri Magufuli kwa uchapakazi hodari unaodhihirisha kwa vitendo kwamba analipenda taifa na kusema laiti kama serikali ingelikuwa na mawaziri watano wachapakazi mfano wake, nchi isingetafunwa na mafisadi, hivyo akawataka Watanzania kumuunga mkono na kumtia moyo badala ya kumkatisha tamaa.



  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata sheikh Mkambaku na baraza lake nao ni wanafiki. Unaposuluhisha mgogoro basi na utazame pande zote. Kama wakazi wa kigamboni walikosea kumzomea Magufuli, je ilikuwa sahihi kwa Magufuli kuwaambia kuwa kama hawawezi kulipa 200 wapige mbizi? Au hayo ni maadili? Kuzungumzia kosa la wanakigamboni bila kusema la Magufuli ni unafiki na kujipendekeza kwa serikali.
   
 3. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ungekua karibu yangu ungepata zawagi. Nilikuja haraka kwa nia ya kusema kama ulivo sema hapo bold.
   
 4. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,714
  Likes Received: 3,121
  Trophy Points: 280
  Magufuli alikuwa sahihi kuwaambia kama hawawezi kulipa 200 wapige mbizi. Watanzania tunahitaji mtu kama huyu wacha tupelekwe kijeshijeshi. Hiyo 200 ndio iwafanye watu wafanye upumbavu wa kuogelea. Atakayeogelea amependa mwenyewe. Lipeni hiyo 200 bana mbona Ubungo Bus Terminal watu tunalipa itakuwa kuvuka mto ooops bahari ya Hindi! Mh. Magufuli ulikuwa sahihi 100%
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Tena kwa gharama zilivyopanda,mimi naona kule ilitakiwa walipe 1,000
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,276
  Trophy Points: 280
  Unampomnyooshea mwenzio kidole kimoja kumkanya, basi vitatu vyote vinakurudia wewe kua una makosa vilevile.
  Hawa jamaa ni unafiki wao tu wa kujipendekeza kea Serikali, sijui waislamu gani wanaowakilishwa na haya mabaraza Uchwara!!!
  Wanakuja na references za ajabu za Kiluvya mpaka Ubungo na Mbagala mpaka Posta, wapi na wapi???
  Wanajua umbali halisi wa Mbagala-Posta V/s Kilivya-Ubungo??
  Na kama wao waliliona hilo la nauli ni tatizo, walichukua hatua gani tangu mwanzo kabla ya kumnyooshea kidole Mh. Mnyika???
   
 7. m

  mams JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2012
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono, naamini hao wabunge wanaomwandama Magufuri ndiyo walihamasisha wananchi wa Kigamboni wamzomee Magufuri.
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,276
  Trophy Points: 280
  Unakosea mams,
  Hao wabunge walikutana wote kwa pamoja lini,
  Na maghufuli alizomewa lini?
  Mbona kama tukio la wabunge kukutana limekuja BAADA ya maghufuli kuzomewa??
  Kabla ya hapo lilikua ni individual issue tu ya Ndugulile peke yake!!
   
 9. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Dada hilo sio jibu la kijeshi bali ni jibu la kijeuri. Yawezekana limekufurahisha leo kwa kuwa hukai kigamboni lkn nikutahadharishe kuwa kushabikia udhalimu ni jambo baya kwani ipo siku itakuwa zamu yako.

  Shida sio kiwango cha uchangiaji mama angu ila ni sababu za kupandishwa kwake. Madai ya Magufuli ni kuwa gharama zimepanda, lkn ameangalia na mianya ya ufujaji wa mapato? Wao wanalalamika kuwa mapato yanaishia mifukoni mwa watumishi wa TEMESA jambo ambalo ni kweli. Jaribu kuchunguza utaona kuwa hawachani tiketi zote badala yake wanazirudisha dirishani kuuza tena. Sasa kama fedha nyingi hivi zinaibiwa, kwa nini wasidhibiti mapato badala ya kupandisha nauli?
  Kujulikana kwa kosa la zamani hakuhalalishi kosa la leo. Kama unaamini serikali inawabana wananchi kwa kuwa tu gharama za uendeshaji zimepanda, je pale Ubungo stendi tunalipa kwa huduma gani? Nikukumbushe kuwa choo kinalipiwa mule sasa napo kuna mafuta mule? Halafu nikukumbushe kuwa hakuna mtu anayeenda stendi kila siku kama ambavyo wakazi wa kigamboni wanaenda kazini na kurudi kila siku.

  Sasa turudi kwenye source: Ukitaka kujua tatizo lilipo ondoka kwenye ushabiki kwanza. Hebu tuangalie hili jambo kwa ujuml wake. Gari ndogo imepandishwa gharama kutoka 800 hadi 1,500 na GUTA (baiskeli ya miguu mitatu) imepandishwa toka 200 hadi 1800, kabla hujamsifia Magufuli hebu fanya ulinganifu wa hivi vyombo viwili na matumizi. Kama kiongozi hajui effect za kupandisha gharama za usafirishaji wa bidhaa (kama usivyojua wewe) basi mtaua watu. Bidhaa za magengeni kule kigamboni zinakwenda kwa GUTA, sasa kama GUTA linapandishwa nauli kwa 1,600 unategemea bei ya nyanya na vitunguu itabaki vile vile?
  Je, kuna uwiano gani wa GUTA na Gari ndogo mpk GUTA ambalo kwangu mimi naweza kuliita ni Public Service lipandishwe zaidi ya gari?

  Hilo neno PUMBAVU ni uonevu kwa watu wa Kigamboni. Kuhoji sio upumbavu (kama ulivyoamua kuwaita kwa sbb ambazo unazijua mwenyewe), kutokuhoji ndio upumbavu. Kwa maoni yangu, watu wa kigamboni wapo sahihi, tulio wapumbavu ni sisi tunaochangishwa stendi ya mkoa na bado hatuhoji juu ya nini tunachanga ikiwa mabasi yanalipa ushuru na vyoo mule ndani ni vya kulipia. Magufuli kuwa waziri sio maaana yake kuwa ndio ana akili kuliko Watanzania woote. Alitakiwa asikilize maoni yao. Kama ana akili sana, mbona wizi unafanyika pale na yeye asibaini? Wale wafanyakazi wamezihujumu zile mashine za tiketi mpk zimekufa ili wakatishe tiketi na mikono waendelee kuiba, mbona hilo halizingatiwi?

  Magufuli na wewe mmekosea (kwa maoni yangu), vigezo na masharti havikuzingatiwa.
   
 10. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama serikali inajua gharama zimepanda, umeshahoji kwa n ini mishahara haijapandishwa? Unaleta ushabiki usio na manufaa ili kutafuta sifa. Ndio namna unayoonyesha jinsi ulivyo mtu wa imani kama unavyojinadi au?
   
 11. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  FF, please nambia huyu sheikhe Mkambaku..!?? anapendelea kuswali mskiti gani ili nikamzomee?
   
 12. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo ndio atajua nini maana ya kuonesha hisia. Kwa kifupi, ni mjipendekeza. (Sasa unapoenda niambie nikuongezee kundi la madogolasi wakusapoti, ukiwa mwenyewe haitanoga, lazima tuwe na watoto wa kukodi)
   
 13. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii zomeazomea ya kuzomea viongoz na kudharau mamlaka zilizowekwa imeasisiwa na chama fulani cha siasa ambacho chenyewe kinajiona kipo juu ya sheria na hudai haki yake kwa kutumia nguvu bila kufuata sheria. Ni tabia mbaya na utamaduni ambao utakuja uliingine taifa mahara pabaya sana , inapaswa ikomeshwe maana ikikomaa watu watafikia kuchukua ama kupelelekea kuchukua sheria mkononi. Tumekuwa taifa la watu wahuni tusiokuwa na maadili kbs kiongozi anakuja kufafanua jambo anaanza kuzomewa hii inatupeleka wapi? au Mnajidanganya ni kukua kwa demokrasia? Kama ndvy bs svyo. Tuwe na staha ukimuacha mtoto wako amtusi jirani au adui yako kesho atakutusi wewe mwenyewe.
   
 14. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naona hapa waTanzania wenzangu mmechemsha. Sbabu zenu zote mnazotoa hazija fikira chanzo chake ni nini? Formula ya kupandisha nauli ya kivuko ilikuwa ni nini. Lazima tuishi katika dunia ya leo. Thamani ya huduma iwe ni sawa na thamani ya malipo. Minus mapungufu. Mwisho ingiza factor ya collection inaelekea wapi.

  Insanity: doing the same thing over and over again and expecting different results.
   
 15. LUPITUKO

  LUPITUKO JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Wewe huibi kazini kwako? Acheni unafiki bwana asitaka nauli mpya aogelee tu
   
 16. LUPITUKO

  LUPITUKO JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Mkubwa hebu pasua kichwa kidogo acha jazba kama wananchi wanaozomea huku hawajui tofauti ya saloon car na guta au baiskeli ya miguu 3
  Unataka kuniambia hata wewe mwenye uelewa mpaka wa kupost thread humu hujui guta na baiskeli hizo ni za biashara na zinaingiza hela nyingi kwa cku wakati saloon car ni huduma tu ya kumtoa mtu point A to B! Sasa kwanini guta asilipe zaidi? Au hujui bajaji zinaingiza hela nyingi kuliko saloon car tax?
  Wacheni kumlaumu Magufuli huyo ni moja ya kiongozi wachapakazi hapa bongo hata kama anamapungufu kama binadam.
   
 17. magilu

  magilu Member

  #17
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i can not belv in this issue yaani all about is ongezeko la sh 100 daaaaah kweli siasa nimchezo mchafu,wanainch tutaendele kuwamadaraja ya waheshimiwa !!!!!!!!
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hawa wabunge badala ya kufanya kazi wamekalia majungu,..hiyo 200 wanapiga kelele weee hizo posho walizojiongezea wao wanaona ni sawa .......myuzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
   
 19. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  nyie wabunge kumbe nyie wanafiki plus, kelele zenu mpka kwa waziri mkuu , mbona hamjaenda kumshitaki Anna Makinda na posho feki zilizopitishwa kinyemela, au kwa kuwa zinawahusu, wewe tambe kaa kimya au msaada kabisa kwa jimbo lako, kazi majungu kama GUNINITA
   
 20. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sawa mimi sina akili, lkn ngoja nikuulize swali. Ukiongeza 1600 kwenye huduma ya guta, umemuongezea mwenye guta au na yeye anaihamishia kwa mwenye mzigo ambaye naye anaihamishia kwa mlaji wa nyanya gengeni kwake?

  Unaweza ukajifanya una dharau lkn ukakosa akili vile vile. Halafu nikukumbushe kuwa wizi sio sifa. Kuniambia kama mimi siibi ofisini kwangu huo ndio UPUMBAVU unaotufanya tuwe maskini mpk leo. Unaiba fedha ya kivuko kwa miaka na miaka kwa manufaa ya familia yako. Kauli zako zinaonesha wewe ndio una jazba. Yawezekana mzazi wako ni mmoja wa wauza tiketi na wewe umelelewa kwa fedha za wizi unaofanyika pale. Tafakari, muogope Mungu.
   
Loading...