Baraza la Iddi: Mahakama ya Kadhi ni suala la Waislamu wenyewe - Kikwete

THE GEEK

Member
Dec 10, 2010
90
32
[video=vimeo;28494538]http://vimeo.com/28494538[/video]

[video=vimeo;28494765]http://www.vimeo.com/28494765[/video]

[video=vimeo;28495126]http://www.vimeo.com/28495126[/video]

[video=vimeo;28495132]http://www.vimeo.com/28495132[/video]

[video=vimeo;28495463]http://www.vimeo.com/28495463[/video]

[video=vimeo;28495672]http://www.vimeo.com/28495672[/video]

[video=vimeo;28495799]http://www.vimeo.com/28495799[/video]
Nafuatilia hotuba ya mh raisi kikwete kwenye baraza la iddi kuoitia tbc 1.

Kwa kweli amejitahidi kuainisha ukweli wa mambo hususan katika sekta ya elimu,

japo naona kuna ma ustaadh wanamuangalia kwa roho mbaya kweli

hasa hasa anaposema baba wa taifa hili mwalimu nyerere alitaifisha

shule zote za dini na mashirika ziwe za serikali ili elimu itolewe bila ubaguzi.

Kudos j.k

n.b:

Mimi ni chadema, ila kiongozi wa ccm akisema jambo likanigusa hakika sitaacha kumfagilia.

Siasa sio uadui na kuona maovu ya mwenzako tu bila kuona mazuri wajameni.
 
Nimekaa nikimsikiliza JK katika baraza la Eid. Huyu bwana hana lugha ya kidiplomasia na sijui kwa nini Mkapa alimpa uwaziri wa mambo ya nchi za nje!!! Kimsingi ananiboa sana. Ukiangalia hata sura za mashehe wetu, wanaonekana wamekata tamaa kabisa. Anyway, binafsi ninajuta kumpigia kampeni kabisa ktk uchaguzi mkuu. Sasa ninakubaliana na statement ya jamaa mmoja inayosema, IF YOU THINK GADDAFI IS BAD, TRY JK
 
JK yuko hewani TBC katika baraza la idd, anaeleza wazi kwamba suala la kuanzishwa mahakama ya kadhi linawahusu waislamu wenyewe na serikali haitajihusisha wala kutoa rasilimali zake.

Kwa mara ya kwanza naona leo ****** akiwa serious na kuongea bila kutafuna maneno huku mashehe wakiwa kimya kama wamemwagiwa maji. Big up JK!!! Pamoja na udhaifu wake hapa jamaa kaongea point.
 
J.K amewathibitishia waislam kwamba mahakama ya kadhi ipo mbioni kuundwa.Lakini J.K ameeleza kwamba serikali haitohusika na uendeshaji wa mahakama hizo.Pia Rais kikwete amesema kwamba mahakama hiyo haitahusika na kesi za madai na jinai.Akieleza zaidi amesema kwamba mahakama hii hairuhusiwi kutoa adhabu ya kumvunja mtu mkono wala kumpiga mawe hadi kufa yule aliyefumaniwa.Mipaka ya mahakama hii ni kuhusika na kesi za Ndoa,Talaka na Mirathi tu.
 
Mimi mwenyewe sikuamini. Lakini nililazimika kumwamini baada ya kuona anaongea bila kuchekacheka na pia akitumia mifano ku JUSTIFY hoja zake, japo kajichanganya pale aliposema WAUZA unga watajulikana mahakamani, lakini hapohapo akasema wameonyeshwa bungeni. Generally, hotuba ilikuwa nzuri.
 
hao siku zote huisi mfumo wa kiraia unawabagua so ni kulalamika kwenda mbele. suala la serikali kutoingilia kati uendeshaji wa kadhi ni la kisheria zaidi kuliko matakwa ya mtu mmoja so kwa hilo ni sahihi maana nchi yetu haina dini japo watu wake wana dini. mwenye wazo la kwamba ipo siku dini itaongoza nchi asahau maana dini ni imani tu kati yako na unaemwamini. Hongereni lakini japo nahisi mmekwazika kutopigana mawe na kukatana mikono hahahaaaaaaa
 
Amefanya vyema. Kwa vizazi vipya msiwe na hofu wala shaka kihusu mahakama hii ya kadhi kwani ilikuwepo wakati tunapata uhuru na iliendelea mpaka mwaka 1963 ilipopigwa marufuku.
 
Hakika leo JK ametoa hotuba ambayo mi binafsi imenifurahisha kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Ila nina wasi wasi kuwa huenda haikupokelewa vizuri na viongozi wa dini ya kiislamu kwani hawakuonyesha sura za furaha.
 
Hivi kweli wataweza kuiendesha hii mahakama bila msaada wa pesa toka serikalini? Hapa kwanza italeta matatizo makubwa, kwani Bakwata watataka waikamte na kuiendesha na hawa wengine watakuja juu, ukweli italeta vurugu miongoni mwa waisilamu.

Uendeshaji wake, na si busara ipewe pesa na serikali.
 
J.K amewathibitishia waislam kwamba mahakama ya kadhi ipo mbioni kuundwa.Lakini J.K ameeleza kwamba serikali haitohusika na uendeshaji wa mahakama hizo.Pia Rais kikwete amesema kwamba mahakama hiyo haitahusika na kesi za madai na jinai.Akieleza zaidi amesema kwamba mahakama hii hairuhusiwi kutoa adhabu ya kumvunja mtu mkono wala kumpiga mawe hadi kufa yule aliyefumaniwa.Mipaka ya mahakama hii ni kuhusika na kesi za Ndoa,Talaka na Mirathi tu.
<br />
<br />
Kiukweli kikwete kazungumza kama raisi wa nchi. Nampongeza sana.
 
iti is very clear sasa kila mtu atajua watu wa hapa JF na chadema ni watu waaina gani.
ndo maana nilisema na narudia kusema kuwa uongozi wa JK umechukiwa kwa sababu ya hii mahakama ya kadhi, kujiunga na OIC na muafaka wa zenji. Sio hizi sababu zinazotolewa.
kabla ya hapo hamna hata mmoja anayeweza kunithibitishia kinyume chake. ona leo mlivyofurahi. Sitaki kuwa bias, bias kwangu mwiko.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom