Baraza la Habari Tanzania(MCT) wamlaumu RC Makonda kwa uvamizi wa Clouds Media

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,584
2,000
Baraza la Vyombo vya Habari Tanzania(Media Council of Tanzania-MCT) Likiongea na Wanahabari mapema leo limesema kuwa tukio la Uvamizi wa Clouds Media limeongelewa kwa kirefu, hivyo waliamua kulifanyia utafiti huru ili kuelewa kilichotokea haswa.

Tukio liko live hivyo updates zaja......

======


=> Ripoti imeandaliwa kutoka maeneo mawili ya Tanzania Bara na Visiwani.

=> Methodology: Kusoma machapisho na maandiko pia kuhoji watu mbalimbali.

=> Kuna mahusiano makubwa kati ya mfumo wa kisheria na masuala ya kisiasa. Mfano kupitishwa kwa sheria mbili zinazohusu sekta ya habari.

=> Kinyume na matarajio ya wengi sheria hizi mbili zimeonekana kuwa haziwezi kukidhi nahitaji katika sekta ya habari. Ingawa zilipokelewa kwa Shangwe na wengi lakini matokeo yake ni kuwepo kwa vifingu vinavyominya Uhuru wa habari.

=> Pia zuio la kurushwa kwa matangazo ya Bunge hili pia tumeliangazia katika utafiti wetu. Wananchi wengi wamekiri kuwa usitishwaji huo umewanyima haki ya kujua nini Wawakilishi wao wanafanya ndani ya Bunge.

=> Mwaka 2016 taasisi nyingi za Print Media zilikuwa katika hali mbaya kutokana na matukio mbalimbali ya kufungiwa kwa magazeti.

=> Kupungua kwa matangazo kwenye magazeti hii imepelekea kuathiri sana shughuli za Taasisi hizo.

=> Kushuka kwa usambazaji wa magazeti kutokana na kuingia kwa mitandao ya kijamii pamoja na miundo mbinu.

=> Pia miundombinu ya usambazaji imekuwa mibovu.

=> Kutoka na sheria zisizo rafiki imekuwa pia chanzo cha mauzo ya magazeti kushuka. Pia ukosefu wa teknolojia ya hali ya juu umekuwa ni changamoto.

MAFANIKIO
=> Print media zimeendelea sana katika habari za kiutafiti.

=> Redio imeendelea kuwa chombo kinachotegemewa na watu wengi na idadi ya redio pia imeongezeka.

ZANZIBAR
=> Kwa Zanzibar kulikuwa na matukio mengi ikiwemo waandishi kunyimwa ushirikiano.

=> Baadhi yao walipewa vitisho na kulazimika kujilinda bila kujali kwamba wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya jamii.

=> Hakukuwa na muongozo wowote wa kuwaeleza waandishi kuwa habari hii weka au hii iache.

=> Tumebaini Zanzibar mpaka leo hakuna sheria ya Right to information.

=> Waandishi wengi hawajiendelezi kielimu na baadhi ya waandishi wanafanya kazi bila kuwa na elimu ya kutosha kuhusu taaluma

=> Zanzibar kuna Vituo vya redio 25 na runinga 22.

MAPENDEKEZO
=> Kuna haja ya kutungwa kwa sheria ya Right to information

=> Kuna haja ya specialization kwenye news room

=> Pia traning kwa waandishi hasa kuhusu maslahi yao maana wengi wanajua kutetea maslahi ya jamii lakini ya kwao hawayajui.

RIPOTI YA CLOUDS
=> Baraza la habari lilitupa jukumu la kuchunguza kilichotokea kituo cha CloudsMedia Group 17 March, 2017 ambapo mkuu wa mkoa alienda studio usiku akiwa na askari.

=> Timu yetu ilikuwa na wanachama wanne.

=> Kwa mujibu wa katiba ya habari kifungu cha tatu [E] ndicho tulichokisimamia katika uchunguzi wetu.

Hadidu za rejea zilizotumika.
1. Kwanza kuchunguza kilichotokea
2. Kubaini askari walioambatana na mkuu wa mkoa
3. Kutoa mapendekezo kutokana na uchunguzi
4. Kuandika ripoti
5. Kuwasilisha kwa wananchi

=> Timu ilitembelea ofisi za Clouds na kuongea na baadhi ya wafanyakazi, ilifanya mahojiano na wafanyakazi wa TRA, Ilifanya mahojiano maafisa wa haki za bianadamu.

=> Juhudi za timu kuonana na mkuu wa mkoa hazikuzaa matunda yoyote.

=> Tulipitia sheria kuona kama kuna sheria yoyote inayomruhusu mkuu wa mkoa kufanya hicho alichokifanya.

TULICHOBAINI

=> Tarehe 17/3 mkuu wa mkoa wa Dsm akiwa na askari alienda kwenye kituo cha Clouds usiku lakini afisa wa ulinzi alisema mkuu wa mkoa huwa anaenda mara kwa mara na alishazoeleka.

=> Sio vibaya kwa vyombo vya habari kushirikiana na wanasiasa lakini Urafiki uliojengwa kati ya mkuu wa mkoa na Clouds ndio uliopelekea akawa na ujasiri wa kuingia ofisi kwa namna ile.

=> TCRA ilisema haina wajibu wa kumuadhibu mtu aliyekikosea kituo cha habari kwahiyo yunaona iwepo sheria itakayoruhusu TCRA kuweza kufanya hivyo.

 

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
MCT: Tukio la Uvamizi wa Clouds Media limeongelewa kwa kirefu, tuliamua kufanya utafiti huru ili kuelewa kilichotokea haswa...

=======UPDATES
LIVE: Tazama Baraza la Habari Tanzania MCT wanazindua Ripoti ya Uchunguzi wa uvamizi wa Clouds TV>>>https://youtu.be/Bt_NzkdTANA


=> Mwaka 2016 kwa print media haukuwa mwaka mzuri kwasababu kulikuwa na tukio la kufutwa kwa magazeti mengi sana zaidi ya 400.

=> Kulikuwa na kushuka sana kwa matangazo kwasababu mbalimbali.

=> Kushuka kwa usambazaji wa habari. Sababu mojawapo ni ongezeko la mitandao ya kijamii imechangia sana katika kushusha soko la magazeti. Sasa hivi magazeti sio chanzo pekee cha habari kama zamani
 

Lawrich

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
589
1,000
o_O Hakuna jipya hapo... Kila mtu anajua nani alikuwa Muhusika mkuu [HASHTAG]#DAB[/HASHTAG] :(! Hii nchi daaaah... [HASHTAG]#NAKWENDA[/HASHTAG] ZIMBABWE
 

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
MCT: Katika utafiti wetu, tumebaini kuwa Sheria ya [HASHTAG]#CybercrimesAct[/HASHTAG] utekelezaji wake hauko sawasawa; tumependekeza iangaliwe upya...
 

Kocha Mkuu

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
1,798
2,000
What is she talking about?

Who wants to hear those shits she is telling.

She should go straight to Bashite's issue.
 

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
MCT: Mwaka 2016, hakuna Mwandishi wa Habari alofungiwa wala Gazeti lililofungiwa visiwani [HASHTAG]#Zanzibar[/HASHTAG]
- There was no critical analysis
 

Victor wa happy

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
11,675
2,000
Sjasoma content

Lkn km lengo ni kuendelea kumfinya Bashite ni furaha sana kwetu vwapenda democrasia

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,433
2,000
o_O Hakuna jipya hapo... Kila mtu anajua nani alikuwa Muhusika mkuu [HASHTAG]#DAB[/HASHTAG] :(! Hii nchi daaaah... [HASHTAG]#NAKWENDA[/HASHTAG] ZIMBABWE
Zimbabwe tulienda kuwaondosha walowezi, ili Zimbabwe iwe huru. Sasa wewe na mwenzio mnaacha matatizo yaliyopo kwenu mnaenda kutatua ya wengine? Hajawaalika, pambana na hali zenu
 

kambonde

Member
Sep 6, 2013
48
95
MCT: Tukio la Uvamizi wa Clouds Media limeongelewa kwa kirefu, tuliamua kufanya utafiti huru ili kuelewa kilichotokea haswa...

=======UPDATES
LIVE: Tazama Baraza la Habari Tanzania MCT wanazindua Ripoti ya Uchunguzi wa uvamizi wa Clouds TV>>>https://youtu.be/Bt_NzkdTANA


=> Mwaka 2016 kwa print media haukuwa mwaka mzuri kwasababu kulikuwa na tukio la kufutwa kwa magazeti mengi sana zaidi ya 400.

=> Kulikuwa na kushuka sana kwa matangazo kwasababu mbalimbali.

=> Kushuka kwa usambazaji wa habari. Sababu mojawapo ni ongezeko la mitandao ya kijamii imechangia sana katika kushusha soko la magazeti. Sasa hivi magazeti sio chanzo pekee cha habari kama zamani
Mkuu MBNA ripoti emechukua mdaa mlefuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,501
2,000
TULICHOBAINI
=> Tarehe 17/3 mkuu wa mkoa wa Dsm akiwa na askari alienda kwenye kituo cha Clouds usiku lakini afisa wa ulinzi alisema mkuu wa mkoa huwa anaenda mara kwa mara na alishazoeleka.

=> Sio vibaya kwa vyombo vya habari kushirikiana na wanasiasa lakini Urafiki uliojengwa kati ya mkuu wa mkoa na Clouds ndio uliopelekea akawa na ujasiri wa kuingia ofisi kwa namna ile.
Hi statement hakika sijaielewa, kuna kitu wanataka kusema but ni kama wamefungwa either mdomo au mikono; kama walikua hawana uhuru wa kusema walicho kibaini better wangekaa kimya kuliko kusema maneno nusu nusu.
 

lolo123

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
454
500
Hawa ndo wanafiki wenyewe.....siku zote walikua wapi ?.... Wameona waingilie kwa gia zilizo wakukutanisha Ruge na Makonda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom