Baraza la Habari Tanzania (MCT) limemchagua kwa mara nyingine Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Rais wake

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
pic+mctt.jpg


Baraza la Habari Tanzania (MCT) limemchagua kwa mara nyingine Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Rais wake kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Jaji mstaafu Mihayo amekitetea kiti chake hicho leo huku akiwa hana mshindani na kuibuka na ushindi wa kura 59 za ndiyo na mbili za hapana katika uchaguzi huo uliowashirikisha wajumbe 61 wa baraza hilo jijini Dar es Salaam.

Akitangaza matokeo hayo, Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Deogratias Nsokolo amewataja wengine waliochaguliwa kuwa ni wajumbe wa bodi akiwamo Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Lts (MCL) Bakari Machumu, Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Eda Sanga, Dinna Chahali na Wallance Maugo.

Amesema nafasi ya uwakilishi wa wananchi kwenye baraza hilo, aliyechaguliwa ni Jaji Mstaafu Juxon Mlay, Anna Hengan na Edmund Mdolwa.

Pia baraza hilo limesema litaanza kuwashtaki watakaovunja uhuru wa Habari ikiwamo kuwazuia waandishi wa Habari kupata taarifa, vipigo na matukio yote ya udhalilishaji dhidi yao.


Mwananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom