Baraza la habari lakemea ukiukwaji maadili kwa waandishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la habari lakemea ukiukwaji maadili kwa waandishi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MzeePunch, Aug 27, 2010.

 1. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  KUJITOKEZA KWA UKIUKWAJI MKUBWA WA MAADILI YA TAALUMA YA UANDISHI WA HABARI KATIKA HABARI ZA UCHAGUZI MKUU


  Kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu 2010 kimefika na vyombo vya habari vinalo jukumu kubwa la kuwapa Watanzania taarifa sahihi kuhusu mchakato huu muhimu wa kidemokrasia.

  Baraza la Habari Tanzania (MCT) linapenda kuvipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ambayo vimekuwa vikifanya hata kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni kwa kuchapisha na kutangaza habari ambazo zililenga kuwasaidia wananchi kushiriki katika uchaguzi huku wakiwa na uelewa wa wagombea na sera za vyama vyao.

  Pamoja na pongezi hizi, Baraza lingependa kutoa tahadhari kuhusu hali ya uvunjwaji wa maadili ambayo imeanza kujitokeza na kuelekea kuenea kwa kasi. Baraza `linatambua kuwa matatizo haya yanachangiwa na uelewa mdogo wa maadili, ushabiki wa kisiasa, lakini pia vitendo vya makusudi vya wagombea na vyama vyao vinavyolenga kuwarubuni waandishi na wahariri kukiuka kanuni za taaluma yao kwa makusudi.

  Baraza linapenda kuwakumbusha wahariri na waandishi kwamba ushabiki wa vyama unaoingilia maadili ya taaluma haukubaliki kamwe. Wakati Baraza linafahamu na kuheshimu ukweli kuwa chombo cha habari kina uhuru wa kuunga mkono msimamo fulani wa kiitikadi au kisiasa, linapenda kukumbusha kuwa hiki si kisingizio cha kukiuka maadili ya kusema ukweli, kutoa haki ya mshutumiwa au mtuhumiwa kujibu, na kuzingatia uungwana katika uwasilishaji wa habari.

  Baraza limefurahishwa na matamko ya vyama vya siasa kuwa vitaendesha kampeni za kistaarabu, zisizokuwa za kutukanana na kupakana matope. Hadi sasa, Baraza linaona kuwa vyama vilivyoingia kilingeni, kwa kiasi kikubwa vinajitahidi kutimiza ahadi hii.

  Hata hivyo, kama msimamizi wa maadili ya wanataaluma ya habari, Baraza limeshtushwa na mwelekeo unaojitokeza unaoonyesha kwamba wakati wanasiasa wakionyesha kuendesha kampeni za kistaarabu majukwaani, baadhi ya vyombo vya habari vinaonekana kuendesha kampeni za maji taka kwa niaba ya wanasiasa.

  Jambo hili halikubaliki, na ni aibu kubwa kwa taaluma hii adhimu. Katika kampeni hizi, waandishi na wahariri waepuke kujaribu kuwa Wakatoliki kuliko Papa mwenyewe, yaani kuwa na ukereketwa na ushabiki kuliko ule unaoonyeshwa na wagombea na vyama vyenyewe! Vyombo vya habari viepuke kufanya kazi chafu kwa niaba ya baadhi ya wanasiasa.


  Baraza pia limezingatia kwa masikitiko mtindo unaochipuka wa wanahabari kuwa wakala wa vyama vya siasa wakati wakiwa kazini. Baraza linapenda kuwakumbusha wanahabari kuwa hawapashwi kushabikia rangi za vyama wawapo kazini, kuvaa mavazi yenye nembo, kauli mbiu au majina ya vyama na wagombea wa nafasi mbali mbali za uchaguzi.

  Jambo hili linawadharaulisha wanataaluma, linajenga mashaka juu ya uadilifu wao. Jambo hili sio tu ni kinyume cha maadili, bali pia ni jambo la hatari, kwani linamweka mwandishi katika nafasi ya kuonekana wakala wa chama au mgombea, na hivyo kuweza kudhuriwa na wapinzani wa mgombea huyo.

  Lakini pia, mwandishi akishajitambulisha kuwa anafanya kazi ya mgombea fulani, wagombea wengine na vyama vyao watawezaje kumwamini atakapokwenda kuandika habari zao?

  Baraza linapenda kuchukua nafasi hii kuviambia vyama vya siasa bayana kuwa ni makosa kuwapa waandishi fulana, skafu, makoti, kanga, kofia, au vazi jingine lolote lililoandaliwa kwa minajili ya kampeni.

  Baraza linawataka wahariri kuwaonya waandishi wao kuacha mara moja tabia hiyo. Kila mhariri makini ajiulize ikiwa kweli ana sababu ya kutumia habari inayoandikwa na mwandishi anayevaa nembo za chama katika kuandika habari za uchaguzi.


  Kumeanza pia kujitokeza mtindo wa baadhi ya vyombo vya habari kutoripoti kabisa habari za baadhi ya vyama na wagombea. Baraza linapenda kuwakumbusha wenye vyombo vya habari na wahariri wao kuwa kibali cha kuendesha gazeti au kituo cha radio au runinga ni mali ya umma.

  Leseni za vyombo vya habari hutolewa ili umma upewe taarifa; hili ndilo lengo la kwanza. Faida ya kifedha au mapenzi ya kisiasa sio sababu kuu inayofanya leseni ya chombo cha habari itolewe. Kwa hiyo wahariri wajitahidi kufanya kazi yao kwa uadilifu, na wamiliki wa vyombo wasiwashinikize kuacha kutangaza au kuandika habari muhimu katika kipindi hiki.


  Baraza la Habari Tanzania litaendelea kufuatilia utendaji kazi wa vyombo vya habari katika kipindi hiki na kushauriana na wahariri, ili Watanzania watendewe haki. Wakati huo huo, Baraza lingependa kuwahimiza wale wote waliopatiwa raslimali kwa ajili ya shughuli ya ufuatiliaji vyombo vya habari katika kipindi hiki, kufanya hivyo na kuwapatia wahariri na wadau wengine ripoti za ufuatiliaji huo, ili wahariri waweze kufanya marekebisho ya udhaifu wowote unapotokea.
  Tanzania yenye vyombo vya habari makini na vinavyowajibika kwa umma inawezekana.

  Kajubi D. Mukajanga
  Katibu Mtendaji
  Agosti 27, 2010
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wakiukwaji wakubwa wa maadili:

  1. Habari Corp

  2. IPP Media

  Hizi ndizo media houses zinazoongza katika uvunjaji wa maadili ambako waandishi wake wanashabikia vyama na nitasema kwa wawili hawa ni CCM tuuu. Pia kuna baadhi ya magazeti uchwara:

  Sauti Huru, Tazama, Hoja, Tafakari (silioni siku hizi), Taifa Tanzania, An Nur, Sauti ya Umma etc
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Magazeti ya Rostamu Azizi ndio kinara wa ushabiki na ushambuliaji wa mtu binafsi. Nina usongo sana nae jinsi alivyo na kiu ya kuchafua amani ya watanzania. Mwache tu aendelekee kwani siku ya siku hata nafasi ya kukimbilia kwao Iran hatutampatia.
  Big up baraza la habari kungamua tatizo la wanahabari.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Haiwezekani hivi hivi tu. haya magazeti (kwenye red) haya usomaji (readership) yoyote, yanatoka kwa kufadhiliwa na mafisadi tu wanaoiibia serikali ya CCM na baadaye kuichangia mapesa. Hilo jingine ni kutokana na ushabili wa kidini tu.
   
 5. m

  masasi Member

  #5
  Aug 27, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAIFA TANZANIA LEO HALIJATOKA NA YOTE HAYO NI KWAMBA GAZETI HALIUZIKI MTAANI TOKANA NA HABARI ZAO ZA KIDAKU:mad2::mad2::mad2::mad2::mad2:
   
Loading...