Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania lamtaka Prof. Bisanda aombe radhi kuhusu waraka wa Corona alioutoa

Mnavyopiga kelele mtasema huwa hamuendi makazini shubamiti zenu! Huna ata uweze wakujilockdown lakini unashadadia kama hela yakuishi ata mwezi unayo..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona wajifanya headless chicken? Wapi na nani kasema ishu ya kuji lockdown? So wew ukiambiwa uchukue tahadhali unawaza kujilockdown? Watu wengine sijui huwa mnafikiri kwa kutumia kiungo gani...
 
Baada ya kumshawidhi aukane waraka wake kushindikana sasa wameamua kumuamuru kuomba radhi.

Huyo hawezi kuomba radhi. Atakachofanya ni kuwabidhi resignation letter usiku huu. Barua hiyo wataikataa na badala yake kutangazwa kwamba ametenguliwa.
Naomba usiku na mchana hii kitu ikapige pale kwa huyo mtu nadhani akili ndipo zitaturudia.
 
Huenda ni kwa sababu unapenda kusoma na kuandika mambo ya namna fulani, hivyo unadhahi wote tuko hivyo. Uliisoma thread hii niliyoanzisha mwezi uliopita, na watu wa aina yako wakanishambulia tena?


Au ulisoma post yangu hii? Tunanadika mambo objective huwa hatuangalii yanamhusu nani; Magufuli akifanya vizuri tutamsifia, na akifanya vibaya tutamkosoa pia. Sio kama wewe unaoyeonekana kupenda kukososa tu hata pale pasipohusika.

Asante. Nimekupata!
 
Atafanya jambo jema machoni pa Mungu wa Mbinguni na Malaika wake ikiwa ataamua kujiuzulu kuliko kuomba radhi kwa kusema UKWELI wenye KUIPONYA Nchi.
Atakuwa mmojawapo wa Viongozi Watanzania wachache wenye Maadili ya kweli.
 
Baraza la Chuo Kikuu Huria, limekaa kikao cha dharura na kuagiza Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Elifas Tozo Bisanda aombe radhi kwa Wizara ya Elimu, Chuo Kikuu Huria na Umma kwa waraka wa tahadhari ya #CORONAVIRUS alioutoa Februari 8, 2021.

Prof. Bisanda alitoa waraka kuwatahadharisha wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho kuhusu ugonjwa wa Corona. Baraza limebaini kuwa yalikuwa maoni binafsi na alikosea kutumia nembo za Serikali.

Aidha imedaiwa taarifa ya Prof. Bisanda imeonekana kukinzana na Sera ya Serikali juu ya tahadhari dhidi ya #COVID19 pia haikuwa na takwimu za kuthibitisha uhalali wa baadhi ya taarifa hizo.

Baraza limeagiza wanafunzi na wafanyakazi wa chuo waendelee na kazi na masomo kama kawaida. Pia limeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Pia soma

- Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT) Chatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID19 NA COVID21

- Corona: Wizara ya Elimu yaukana waraka wa Prof. Elifas Tozo Bisanda Makamu wa Chuo Kikuu Huria (OUT)
1. Natamani kufahamu kama Prof alishaomba radhi.
2. Je, kichwa cha Prof bado kinaonekana kuwa ni kidogo kama walivyomdhania na kumtaka kuomba radhi?
3. Je, waliomtaka aombe radhi kwa madai kuwa waraka ulikuwa wake binafsi na sio wa chuo bado wanasimamia kauli zao?
 
Back
Top Bottom