Baraza kuu UVCCM wailaani CHADEMA kwa siasa za fujo na mauaji; Je, ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza kuu UVCCM wailaani CHADEMA kwa siasa za fujo na mauaji; Je, ni sawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Sep 14, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Na Suleyman Mwenda,
  UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wamemaliza kikao cha baraza la umoja huo ambapo wamejadili ajenda mbalimbali za msingi kuhusu Uchaguzi na pia wamejadili juu ya hali ya siasa nchini na mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa amani na mauaji, ambapo wamekinyooshea kidole Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwa vinara wa matukio ya mauaji, kitu ambacho ni hatari kwa Taifa.

  Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya Katibu Mkuu, jengo la Mikutano (whitehouse) katika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi, Dodoma.

  Alisema kuwa, kumekuwa na matukio ya mauaji kwenye mikutano ya chama hicho katika mikoa ya Singida, Igunga, Tabora, Morogoro na Iringa hali ambayo imekuwa ikitishia Usalama na Amani ya Nchi.
  "Tunalaani Chadema kuwa vinara wa vurugu zinazosababisha mauaji na kila tukio linapotokea viongozi wa Chadema wanakuwepo, hali inayoonyesha kuwa siasa wanazoendesha si za kistaarabu" alisema.
  Alisema kuwa Chadema wanachojenga ni hatari kwa Taifa na pia hatari kwa Umoja wa Vijana pia na kama wana mapenzi ya kweli na watanzania waache siasa zinazasababisha mauaji mara kwa mara.

  source hakingowiblog
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CDM ikifungua matawi yake hapo ndo fujo!! Polisi waliotumwa na CCM wakipiga CDM wanaofungua matawi inakuwa CDM wamefanya fujo.. CCM kunavilaza sana!!
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama CHADEMA ndio waliosababisha vifo, kwa nini Jamhuri imepeeka mahakamani askri wa Jeshi la polisi? Shigella amesoma press release ya waziri wa mambo ya ndani? If this so call kiongozi wa vijana wa CCM cannot understand something as basic as this atawezaje kuongoza huo umoja wa madalali?
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  "Hongera" Shigela kwa kuonyesha ni jinsi gani chama chako kilivyoishiwa na mambo ya msingi ya kujadili. Badala ya kujadili ni jinsi gani chama chako kifanye ili kutekeleza ilani ya uchaguzi na kuondoa kero za watu, nyie mnajadili siasa za maji taka kwa kujaribu kusukuma lawama za mauaji kwa Chadema. Chadema ina polisi na FFU wanao ua watu?

  Pambaf!!!!!


  Tiba
   
 5. L

  Leodgard Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hawajaanza kujilaani wao kwa kuwatumia polisi ccm KUUA raia???
   
 6. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wanaunga mkono vitendo vya polisi?
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ningependa sana kuona vijana nchi hii tunakuwa kitu kimoja badala ya kuwatumikia wanasiasa.

  sikubaliani na mauaji na fujo zinazotokea kwenye mikutano na maandamano ya vyama vya siasa lakini pia sikubaliani na baadhi ya wanasiasa vijana kutumia vifo hivyo kama mtaji wa kisiasa
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo ndio utajua CCM hamna viongozi wenye uelewa tofauti na alivyokuwa anajigamba yule waziri mchovu wa Afrika mashariki
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wapo kwa ajili ya maslahi yao hata ikibidi kutetea uovu
  huyo bwana nadhani hata tumbili ana akili zaidi yake
  picha zote, press release ya waziri na magazeti hajaona
  hebu athibitishe ni wapi chadema iringa walitumia fujo?walirusha hata jiwe?
  je morogoro nako walifanya fujo? wasitake kututia chuki tukaanza kuwatwanga virungu mitaani
   
 10. m

  manucho JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kumbe askari nao ni Chadema nilikuwa sijajua hilo
   
 11. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  huyo shigela anatumia masaburi kufikiri. wanaoua ni police waliotumwa na CCM au ni wafuasi wa Cdm. ingekuwa Cdm ndo wangekuwa wanaua watu mbona hizo tume zinazoundwa zikigundua ni magamba yamehusika hazitoi majibu mpaka leo. hii ya Iringa imewaumbua mungu yu pamoja na Cdm sio mafisadi.
   
 12. saronga

  saronga JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 909
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hawa ndo walewale kina Kibabaji na Mchemba, wanasingizia kutumiwa msg za kutishiwa kuuwawa na wabunge wa CDM ili kupunguza ukali wa hoja za CDM, kumbe wanajitumia wenyewe hizo sms. Wamechoka, hawaoni tena mbele, kuna giza totoro mbele yao. Mfa maji haishi kutapatapa, wanatafuta pa kuponea lakini hawatapona. Wamekwisha. Magamba yao yameshakuwa mizigo isiyobebeka, kuyavua ndo haiwezekani kwasababu yameng'ang'aniana na minofu yao.Sasa wameamua kutumia Policcm kuuwa raia wasiokuwa na hatia. Watajuta kutuibia rasilimali zetu. M4C 4REVER
   
 13. m

  manucho JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kumbe askari nao ni Chadema nilikuwa sijajua hilo
   
 14. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Kama Shigela ndo anaonekana ana akili kubwa na kuongoza vijana wa CCM hao wanaoongozwa wakoje? TAFAKARI
   
 15. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Akina Shigela ndo wale vijana tuliokuwa tunawajadili jana ITV ambao wanatumiwa na wanasiasa bila kujijua.

  Kama hajaambiwa akawaulize wanausalama wa ccm watamwambia kwa nini vifo vinatokea ktk mikutano ya Chadema - (sisi tunajua) na lengo lilikuwa ni nini ambalo liliharibikia Iringa kwa bahati mbaya. Kama hajui basi bado hawajamwamini kumwambia vitu vizito. Let him to his home work.
   
 16. m

  mossad Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ............Kwa propaganda hizi zisizo na ubunifu za CCM, nina uhakika hata babu yangu tuliyemzika miaka 28 iliyopita akiwa na umri wa miaka 102 kama akifufuka leo hawezi kukubaliana wala kuipenda CCM
   
 17. saronga

  saronga JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 909
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kama si tukio la Nyololo kurushwa LIVE na wanahabari, leo hii tume/kamati hii waliyoiunda kujichunguza wenyewe ingekuja na stori nyingine kama ile ya Morogoro. Sasa hivi wangekuja na propaganda kuwa CDM wanamiliki Mabomu (vitu vizito vinavyonyofoa uhai wa watanzania kikatili). Kwasababu Mungu yupo upande wa Watanzania ameamua kuweka mambo hadharani kwa kuanza kuwafunga ufahamu majangili (Chama twawala). Ndo maana wanafanya mambo ambayo hata watoto wadogo tena kutoka vijijini ambako magazeti na TV ni chache watambue udhalimu wao. HAWADANGANYIKI TENA na propaganda majitaka, wanaona na kusikia kwa macho na masikio yao. MBINU zao zimefikia ukomo. wajiandae kutinga ICC 2015.
   
 18. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Yani kweli UVCCM ndiyo wanadhihirisha ni jinsi gani tulivyokuwa na serikali DHAIFU. Inakuwaje wanasema CDM wanafanya mauaji, wakati tunaona waliokamatwa na kutuhumiwa kwa mauaji hayo ni mapolisi? Mpaka sasa Polisi mmoja wa Iringa ameshafikishwa mahakamani kwa mauwaji ya kikatili ya mwandishi Daud Mwangosi, na wengine nane wametuhumiwa kwa mauaji ya Ally Zona Morogoro. Jinsi walivyolaani matukio ya mauaji haya, inaonekana basi POLISI ni chama cha kisiasa nacho kinaitwa CHADEMA.
   
 19. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Huyu she_jela hajui anenalo.IVI UVCCM umri vp? Shegela =45
   
 20. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Poleni vijana wa ccm mnaoongozwa na huyu Shigela aliyejaa Wasifu wa Bi Kirembwe kiongozi mkuu wa nchi ya Giningi kwa waliosoma kitabu cha Tamthiliya "Kivuli kinaishi" { Advance Kiswahili}wanamfamu vizuri. Kitu unakifahamu kina rangi nyeusi lakini Bi Kirembwe anakuambia hiyo ni rangi nyeupe kisha wanashangilia kama mazuzu.
   
Loading...