barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limeanza kikao chake cha kawaida cha siku mbili mjini Zanzibar leo hii chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama, Mhe. Twaha Taslima anayeonekana hapa akikifungua kikao hicho.
Picha nyengine inamuonesha Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa taarifa kuhusu mahudhurio ya wajumbe na kumkaribisha Mwenyekiti kufungua kikao.
Na picha ya mwisho inaonesha sehemu ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa wakiwa kwenye kikao hicho.
Pamoja na mambo mengine, kikao hichi cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kinatarajiwa kutoa mwelekeo wa CUF kuhusu hali ya kisiasa nchini.