Baraza kubwa la mawaziri ni mbwembwe na fadhila

Said Bagaile

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
686
256
Tumekuwa tukishuhudia matumizi mengi yasiyo na lazima yakiwamo ya safari za nje za rais, huku Serikali ikiwa inashindwa kugharamia sekta muhimu ikiwapo kuwalipa mishahara yenye hadhi stahiki Ma-Dr.

Kwa kutokuwepo ofisini kwa zaidi ya miezi mitatu, Naibu Waziri wa Miundombinu, Dr. Mwakyembe na Waziri wa Maji, Prof. Mwandosya na kazi zinaendelea bila kuonekana mapengo ya kutokuwepo kwao (Maana kama kungekuwa na mapengo, rais asingesita kuwateua watu wengine kukaimu au kuchukua nafasi zao ili kazi zisilale nayo iweze kutekeleza Ilani yake ya Miaka 5).

Kutokana na kutokuonekana kwa upungufu wowote wa kiutendaji hata kama hawapo, je serikali haioni kwamba imefika mahali pa kupunguza baraza lake la Mawaziri kwa kufanya Wizara ziwe na Mawaziri badala ya kuwa na watu wawili kwenye wizara moja?

Na hapa nimezungumzia Wizara mbili tu ambazo tumeaminishwa kwamba ni moja ya Wizara nyeti, bado sijaja Kazi na Maendeleo ya Vijana, Jinsi n.k.
 
Kama ufanisi ni mdogo, Serikali haioni kwamba haitaweza kutekeleza ilani ya Uchaguzi ambayo inadumu kwa muda wa miaka mitano tu? Au ndio wanakiri kwamba Ahadi zoote za Ba M'asha zilikuwa ni Magumashi matupu? Hivi sisi wabongo tutaendelea kufanywa Ma.fa. la mpaka lini na hawa wanaotaka kutumia migongo yetu kupata vyeo vya kisiasa!
 
Back
Top Bottom