Baraza jipya: Watu wale wale, wao Hawajiajiri?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Pana haja ya kumpongeza Mama Samia kwa spana zake hadi tukae sawa. Hakuna namna, maana wajinga ni wengi mno!

Eti nyoyo za watu zaonekana kuwa na maduku duku. Kwani tulitegemea dodo chini ya mnazi?

Kwamba nyuso za watu haziakisi furaha na baraza jipya? Kwamba baraza zima halikuvunjwa kuanza na timu mpya? Kwamba kina Riz moko, Nape, na kina January wako ndani ya nyumba?

Kwamba pascal pamoja na yote angali kijiweni?

Kwani hao wa kila siku si ndiyo wanayo mitaji minono tayari na hata fursa za connection kibao kuweza kujiajiri kwa tija? Kwani wao kujiajiri haiwahusu?

Hata hivyo mama endelea kupiga spana hadi ijulikane hii nchi ni mali ya nani.

IMG_20220108_210128_527.jpg

Kabla ya kuelewana kuwa maadui na marafiki si wa kudumu bali agenda, mama na aendelee kuupiga mwingi tu.

Ila angalizo:

Tanzania ijayo (Mungu mkubwa, ikitupendeza) ajira zote zitakuwa ni za mkataba miaka mitatu mitatu, renewable mara moja tu. Mtu mmoja hatakuwa kwenye ajira ya umma (na kama vipi, ikitupendeza zaidi, hata binafsi) kwa miaka sita.

Hii itakuwa kwa watu wote across the board isipokuwa rais na wabunge watakao kuwapo ofisini kwa miaka minne minne renewable once.
 
Bado tuna safari ndefu sana kama taifa, CCM baada ya kututawala kwa miaka 60 wanaonesha dhahiri jinsi akili zao zilivyofika mwisho wa kufikiri. Sasa wanashindwa hata jambo dogo tu la kutafuta sura mpya zenye weledi zije kufanya kazi ya wananchi licha ya wasomi wengi waliopo.

Ni aibu kwa taifa la watu zaidi ya milioni 60 kuongozwa na sura zile zile kila awamu, huu mchezo wa kurithishana madaraka unatengeneza taifa la watawala na watawaliwa. Nawashangaa zaidi wale jamaa zangu wanaoitwa ikulu wakaimbe mipasho wakati hata wao keki ya taifa haiwahusu, hawa ndio watumwa haswa.
 
Bado tuna safari ndefu sana kama taifa, CCM baada ya kututawala kwa miaka 60 wanaonesha dhahiri jinsi akili zao zilivyofika mwisho wa kufikiri, Sasa wanashindwa hata jambo dogo tu la kutafuta sura mpya zenye weledi zije kufanya kazi ya wananchi.

Mkuu wanayo hata haja ya kujipanga kiushindani? Kwa kitisho kipi tunachowapa?

IMG_20211211_115457_124.jpg

Tumeshindwa hata kuwa infiltrate?

Kama wa jalalani, Ndugai na wengine walikuwa ni Sukuma genge kwenye kumuondosha Jobo usupika, kusingezaliwa mambo hapo?

Mshindani asiyekuwa na mkakati ya ushindi ana kitisho gani?
 
Bado tuna safari ndefu sana kama taifa, CCM baada ya kututawala kwa miaka 60 wanaonesha dhahiri jinsi akili zao zilivyofika mwisho wa kufikiri. Sasa wanashindwa hata jambo dogo tu la kutafuta sura mpya zenye weledi zije kufanya kazi ya wananchi licha ya wasomi wengi waliopo.

Ni aibu kwa taifa la watu zaidi ya milioni 60 kuongozwa na sura zile zile kila awamu, huu mchezo wa kurithishana madaraka unatengeneza taifa la watawala na watawaliwa. Nawashangaa zaidi wale jamaa zangu wanaoitwa ikulu wakaimbe mipasho wakati hata wao keki ya taifa haiwahusu, hawa ndio watumwa haswa.
Anko Magu Ndo aliwathaminisha wasomi lakin siyo hii mburutu
 
Wasomi wenyewe ni hawa wa majalalani?

Prof. Mwanazuoni Nguli wa mambo ya sheria aliyeipigia chapua katiba mpya akiwa nje hadi alipoteuliwa uwaziri.

Akawa waziri wa sheria na katiba, mshauri mkuu wa mwendazake kama W NJ. Leo anatolewa uwaziri unceremoniously bila kuipa nchi hii katiba mpya?!

Kitila Mkumbo, Prof mwanazuoni Nguli wa mambo ya uchumi aliyepigia chapua katiba mpya akiwa nje hadi alipoteuliwa waziri.

What a disgrace?!

Hawa jamaa na wenzao wa namna hii bora warejee walikotoka.

Ama kweli majalalani (kama mavumbini) na warejee!
 
Na wana mitaji na hata kama hawana kuipata sio tatizo

Ila bado wamengangania tu kutuongoza akina sie wana wa wakulima.
 
Bwana Stroke kwa mara ya kwanza maishani nimekupa "like" yangu.

Yote haya tunayo yaona ni kwa sababu ujinga wetu uliopitiliza. Ninadhani wacha tuendelee kuwahudumia hadi pale akili vichwani zitakapotukaa sawa.

Tumeshindwa kumwunga mkono Ndugai kwenye hoja yenye mashiko. Tukashindwa kuzuia asifurushwe yeye kama mkuu wa mhimili.

Timu yote inayoitwa sukuma genge, sisi na ninyi tumeshindwa kusikilizana kuirejesha nchi hii mikononi mwetu?

Tukawa na katiba mpya yenye kushinikiza uhuru kamili wa mihimili yote pia haki, uhuru na usawa kwetu sote?

Hatutaki demokrasia? Halafu tunalia lia?

Kwani hata tunaye nani wa kumlaumu kwenye ujinga wetu huu uliopitiliza?
 
Mzalendo yeyote hawezi furahishwa na mambo yanayoendelea kwa sasa.

Vizazi vijavyo vitatushangaa mno kuwa sisi ni watu wa aina gani tukiendelea kuzembea katika mambo ya msingi.
 
Nimekupa "like" nyingine bwana Stroke tafadhali usinirejeshe tulikokuwa. Ni nia yangu kuendelea kukutunuku kama mzalendo mwenzangu na kama ninavyo watunuku wakiwamo kina denooJ .

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi na yaliyopita si ndwele.

Tunakubaliana kuanza mwanzo mpya wenye maridhiano ya kweli kuirejesha nchi hii mikononi mwa umma (wananchi)?
 
Nilikuwa nimejipa nadhiri kuwa nisi discuss suala lolote la siasa lakini nimeshindwa,siku nchi tukiirudisha mikononi mwa wananchi kuamua hatma yao tungekuwa na maendeleo kama USA ila tumewakabidhi wanasiasa ambao wanajipatia umaarufu na maisha mazuri kupitia matatizo yetu,wanarithishana madaraka na kujipatia maisha mazuri kwa kigezo cha kutuongoza lakini baada ya miaka 5 au 10 tunatengeneza wanasiasa matajiri ambalo linakuwa kundi maalum la wachache wenye nacho huku wakiliacha kundi kubwa likiwa kwenye ufukara wa kutisha
 
Pana haja ya kumpongeza Mama Samia kwa spana zake hadi tukae sawa. Hakuna namna, maana wajinga ni wengi mno!

Eti nyoyo za watu zaonekana kuwa na maduku duku. Kwani tulitegemea dodo chini ya mnazi?

Kwamba nyuso za watu haziakisi furaha na baraza jipya? Kwamba baraza zima halikuvunjwa kuanza na timu mpya? Kwamba kina Riz moko, Nape, na kina January wako ndani ya nyumba?

Kwamba pascal pamoja na yote angali kijiweni?

Kwani hao wa kila siku si ndiyo wanayo mitaji minono tayari na hata fursa za connection kibao kuweza kujiajiri kwa tija? Kwani wao kujiajiri haiwahusu? Au?!

Hata hivyo mama endelea kupiga spana hadi ijulikane hii nchi ni mali ya nani.

View attachment 2073914

Kabla ya kuelewana kuwa maadui na marafiki si wa kudumu bali agenda, mama na aendelee kuupiga mwingi tu.

Ila angalizo:

Tanzania ijayo (Mungu mkubwa, ikitupendeza) ajira zote zitakuwa ni za mkataba miaka mitatu mitatu, renewable mara moja tu. Mtu mmoja hatakuwa kwenye ajira ya umma (na kama vipi, ikitupendeza zaidi, hata binafsi) kwa miaka sita.

Hii itakuwa kwa watu wote across the board isipokuwa rais na wabunge watakao kuwapo ofisini kwa miaka minne minne renewable once.
hiyo picha sasa uliyoambatanisha🤣🤣
 
Nilikuwa nimejipa nadhiri kuwa nisi discuss suala lolote la siasa lakini nimeshindwa,siku nchi tukiirudisha mikononi mwa wananchi kuamua hatma yao tungekuwa na maendeleo kama USA ila tumewakabidhi wanasiasa ambao wanajipatia umaarufu na maisha mazuri kupitia matatizo yetu,wanarithishana madaraka na kujipatia maisha mazuri kwa kigezo cha kutuongoza lakini baada ya miaka 5 au 10 tunatengeneza wanasiasa matajiri ambalo linakuwa kundi maalum la wachache wenye nacho huku wakiliacha kundi kubwa likiwa kwenye ufukara wa kutisha

Hakuna mwenye akili zake mwenye muda wa kupoteza kuandika andika mitandaoni.

Ieleweke kuacha kuandika au kuacha kufanya lolote ni kuwasabiria fisi bucha.

Tunaweza kushinikiza mabadiliko kwa namna tunayoona inafaa.

Kwa kuanzia tunaweza kushinikiza Ndugai abakie pale kama Spika.

Tunaweza kufikia maridhiano na wadau wengine.

Hii nchi ni yetu sote. Tufike mahali tutoe kauli:

"Inatosha!"
 
Back
Top Bottom