Baraza jipya la mawaziri

Rational

Member
Feb 27, 2012
10
4
Heshima kwa wote. Ujanja wa JK. J.K anampango wa kubadilisha baraza la mawaziri na siyo kuwawajibisha mawaziri waliyofuja mali za umma. Ujanja anaotaka kuutumia J.K si kuwawajibisha ila atabadili baraza zima na kuwaacha wale waliyo husika ili ionekane kuwa hawajawajibishwa bali ni timua timua ya wengi. Kwa hiyo msahau kuhusu wao kupelekwa mahakamani. Kwani akiwawajibisha mawaziri hao pekee atalazimika kupambana na upepo wa kuwapeleka mahakamani.
 
kikwete ni vampire kwa hapa tz, yaani sifuri, uozo, yaani huyu mtu anakera sana, nchi inaelekea kubaya sana kwa ajili ya huyu jamaa, shime wa tz inatakiwa tuchukue maamuzi magumu.
 
Inasikititisha sana kuona watanzania wanakosa mang'amuzi juu ya jambo hili! Wengi wametega masikio yao ili kusikia tu uteuzi wa baraza jipya la mawaziri. Ingekuwa katika nchi nyingine kabla ya jambo lolote, ajenda kuu hapo ingekuwa wahujumu uchumi kupelekwa mahakamani; tena kwa maandamano ya hali ya juu na hata fujo! Hili ndilo jambo la kwanza ambalo lingesubiliwa kwa hamu na kila mtu. Lakini kwa Tanzania ni kinyume chake! Kinachosubiriwa kwa hamu ni uteuzi wa mawaziri wapya! Baada ya uteuzi tuendelee kudumisha amani na utulivu! Haya nayo ni mazingaombwe mengine! Bado tuna safari ndefu!
 
Tulikuwa na imani sana na mkulu wetu alipochukua nchi lakini bahati mbaya imekuwa kinyume
 
Atasubiri apigiwe kelele zingine ndipo aamue kuwashtaki wachache kwa kesi ambaya anajua watashinda. SWALI; Hivi hao mawaziri wakiondolewa kwa ajili ya WIZI, je,watafaa kuendelea kuwa wabunge?
 
Kwa Tanzania watafaa.Mfano mzuri,Chenge,Lowasa,Meghji etc
 
Inasikititisha sana kuona watanzania wanakosa mang'amuzi juu ya jambo hili! Wengi wametega masikio yao ili kusikia tu uteuzi wa baraza jipya la mawaziri. Ingekuwa katika nchi nyingine kabla ya jambo lolote, ajenda kuu hapo ingekuwa wahujumu uchumi kupelekwa mahakamani; tena kwa maandamano ya hali ya juu na hata fujo! Hili ndilo jambo la kwanza ambalo lingesubiliwa kwa hamu na kila mtu. Lakini kwa Tanzania ni kinyume chake! Kinachosubiriwa kwa hamu ni uteuzi wa mawaziri wapya! Baada ya uteuzi tuendelee kudumisha amani na utulivu! Haya nayo ni mazingaombwe mengine! Bado tuna safari ndefu!

You read my mind. Very well said.
 
Heshima kwa wote. Ujanja wa JK. J.K anampango wa kubadilisha baraza la mawaziri na siyo kuwawajibisha mawaziri waliyofuja mali za umma. Ujanja anaotaka kuutumia J.K si kuwawajibisha ila atabadili baraza zima na kuwaacha wale waliyo husika ili ionekane kuwa hawajawajibishwa bali ni timua timua ya wengi. Kwa hiyo msahau kuhusu wao kupelekwa mahakamani. Kwani akiwawajibisha mawaziri hao pekee atalazimika kupambana na upepo wa kuwapeleka mahakamani.

Kwa kuongezea kuwawajibisha hao mawaziri ni sawa na kujiwajibisha yeye mwenyewe kwani haiwezekani dege litue, tena nasikia la kijeshi, na kubeba twiga bila TPDF, TISS kujua. Pia JK lazima amekuwa akipata mgao! Tatu watoto wanaiga mambo ya baba!!
 
Salama ya Jk ni kuwafukuza hao wezi wenzake na kuwapeleka mahakamani. Tofauti na hapo umma tutatoa azimio la kumwajibisha yeye mwenyewe.
 
Tusubili tuone nni kitatokea,vipo vyombo vyasheria vyenye wajbu wakuwashugulikia waalifu.na ucshangae kusikia ma'mkwe waziri tena.
 
Kuwawajibisha ndio nini? unaweza kumwajibisha mtu asiyewajibika? Kaa fikiri kabla hujajibu, unaonesha huielewi maana ya uwajibikaji.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom