BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI - Spika, Waziri Mkuu wamuonya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI - Spika, Waziri Mkuu wamuonya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 3, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

  Spika, Waziri Mkuu wamuonya Kikwete

  Mwandishi Wetu

  Toleo la 237
  2 May 2012

  [​IMG]

  UJUMBE maalumu umewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kutoka kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambao kwa pamoja wamekiri kuwa baadhi ya mawaziri wana uwezo mdogo wa kukabili changamoto za hoja za wabunge na wamependekeza uteuzi mpya uzingatie zaidi umakini na uwezo binafsi wa mtu, sambamba na uadilifu, Raia Mwema, limeelezwa.

  Kwa upande mwingine katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni Rais Kikwete kukubaliana na ujumbe huo na ushauri wa wabunge, pamoja na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, kwa mara ya kwanza tangu wito wa kuwawajibisha mawaziri utolewe, ameweka wazi kuwa atachukua hatua.

  Kikwete aliweka bayana msimamo wake huo wakati wa hotuba yake ya Mei Mosi, mjini Tanga, Jumanne wiki hii, akikumbusha kuwa yeye ndiye aliyeruhusu ripoti za ufisadi zinazotokana na ukaguzi wa hesabu za Serikali zijadiliwe kwa uwazi bungeni na sasa, ni wakati wa kuwachukulia hatua kwa watu aliowaita "mchwa."


  Kwa mujibu wa Kikwete, hatua kali zitawagusa watendaji waliohusika na wizi ulioripotiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Hata hivyo, hakufafanua ni hatua zipi zikazochukuliwa dhidi ya wahusika ingawa pia alieleza kufadhaishwa na ufisadi huo.


  Kikwete anaungana na kauli iliyowahi kutolewa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwamba, mjadala mkali miongoni mwa wabunge kuhusu ripoti za CAG kutaja ufisadi kila mwaka zitakuwa zinabeba sasa heshima na uzito unaostahili.


  Kwa upande mwingine, taarifa kuhusu ujumbe wa Makinda na Pinda waliouwasilisha kwa Kikwete unatajwa kutolewa kwa kuzingatia uwezo mdogo walioonyesha baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri, kiasi cha kuzidisha malalamiko ya wabunge wanaodai maswali yao bungeni kutojibiwa ipasavyo.


  Mifano kadhaa imetolewa, ambayo ni pamoja na baadhi ya wabunge kuwahi kulalamika kwa maandishi kwa Spika wakieleza maswali yao kwa baadhi ya mawaziri kujibiwa kwa misingi ya ubabaishaji.


  Katika kuwasilisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete, Spika na Waziri Mkuu Pinda wamekaririwa kumweleza Kikwete kwamba wapo mawaziri ambao ni butu katika kujibu maswali bungeni au kukabili hoja zenye changamoto zinazopaswa kupata majawabu kutoka kwenye wizara zao, wakitaja mawaziri kadhaa.


  Kutokana na ushauri huo maalumu kwa Kikwete, Spika na Pinda wametaka mawaziri wapya wateuliwe kwa kigezo cha umakini wao, sambamba na vigezo vingine, huku vyanzo vyetu vya habari vikieleza kuwa Kikwete ameahidi kuzingatia ushauri huo.


  "Kuna ujumbe maalumu amepewa Rais Kikwete na viongozi waandamizi. Ni ushauri ambao unazingatia hali halisi na changamoto zinazoikumba Serikali ndani ya Bunge. Wameeleza kusikitishwa na mwenendo wa baadhi ya mawaziri na kwa kweli wamewataja kwa majina na kutoa mifano ya vitendo vyao ndani ya Bunge vinavyoashiria ama kuwa na uwezo mdogo katika kujibu hoja zinazoonekana kuishambulia Serikali au si wafuatiliaji wa masuala yanayohusu sekta zao.


  "Spika ndiye kiongozi wa Bunge na Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, wanayo nafasi kubwa sana ya kuwapima mawaziri na naibu mawaziri, mapendekezo au ushauri wao ni muhimu sana na Rais ameonyesha kukubaliana nao," kinaeleza chanzo chetu cha habari.


  Lakini wakati Spika na Pinda wakiwasilisha ujumbe huo maalumu kwa Rais Kikwete, vyanzo mbalimbali vya habari kutoka CCM vinabainisha kuwa, wito wa kuvunja baraza la mawaziri umemsaidia kwa kiasi kikubwa Kikwete ambaye anatajwa awali kuwa katika namna ya kutafuta njia ya kufanya mabadiliko hayo.


  "Rais alikuwa na mpango wa kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri sasa ni kama vile shinikizo hili limesaidia kufanikisha nia yake bila lawama kutoka kwa mtu yeyote wakiwamo hao mawaziri watakaoenguliwa," anaeleza mtoa habari wetu.


  Shinikizo la mabadiliko ya Baraza la Mawaziri msingi wake ni pamoja na ufisadi mkubwa kufichuliwa na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) wa Hesabu za Serikali, ufisadi ambao umekuwa ukijirudia karibu kila mwaka sasa.


  Ni ufisadi huo kujirudia kila mwaka ndiko kulikomfanya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zitto, kutoa wito kwa wabunge kutia saini fomu kwa ajili ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


  Zitto alifanikiwa kupata saini za wabunge 73 waliokuwa tayari kutaka Waziri Mkuu apigiwe kura ya kutokuwa na imani, hata hivyo, baadaye Kamati ya Uongozi ya wabunge wa CCM ilikutana na kuazimia baadhi ya mawaziri kujiuzulu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa mwenendo usioridhisha kiutendaji.


  Baadaye Kamati Kuu ya CCM ilikutana na kuridhia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambayo yanatarajiwa kufanywa na Rais Kikwete wakati wowote.


  Ni katika baraza hilo jipya, kumekuwa na wito wa kutaka ukubwa wake uzidi kupunguzwa kutoka idadi ya sasa ya mawaziri 31 pamoja na Waziri Mkuu.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ina maana wamepeleka majina ya Mawaziri au Wabunge Mbumbumbu hawafai kuwa mawaziri?

  "BINADAMU lazima awe tayari kufa kwa ajili ya kutetea haki. Kifo ni ukweli ambao hauepukiki. Kila siku watu hufa, lakini matendo mema ya mtu huishi milele"
   
 3. s

  slufay JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwacheni mteuliwa wa wananchi yeye ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho: Viva CCM Viva Kikwete chaguo la Watanzania na mlezi wa Taifa letu, HAKUNA RAIS KAMA KIKWETE AFRICA, CCM IMARA TAIFA IMARA.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kwa mwaka ulioishia June 2010 ilikabidhiwa serikali mwezi April 2011; leo yapata mwaka hizo hatua zitachukuliwa lini; kwanza pengine kwa mwaka ulioishia June 2011 hao watendaji watakuwa wameharibu zaidi maana hawakuona hatua yoyote dhidi yao
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kituko kingine hiki. Makinda anahoji uwezo wa mawaziri? Vipi tukihoji uwezo wake.
   
 6. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh sasa kama Pinda legelege na Makinda wamewasilisha ushauri kwa Rais kwamba mawaziri wengine ni Butu sasa sijui wao ni wakina nani aiseee.

  Pinda acha kupindisha mambo yasiyopindika..Makinda acha kufanya watu makinda.

  tuna akili zetu timamu kwamba mnajikosha tu hamna lolote
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sasa PInda naye anaonya kuhusu uwezo... mbona hata yeye hana huo uwezo wa kuhimili???
   
 8. b

  big niga Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ..mbona mnarudia yaliyoandikwa kwenye magazeti, toa hoja hapa
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  nincompoop!!!
   
 10. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,696
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Sasa kuna haja ya wabunge nao kupeleka hoja kwa Rais kuhusu Ubutu wa PM na Spika..maana hata wao ni Gamba na ndio chanzo cha yote haya.
   
 11. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Always remember:- "Procastination is thief of time."
   
 12. s

  santesandy JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  slufay unavuka mipaka ya ujinga, Unaingia kwenye upumbavu! angekua raisi bora Africa kusingekuwa na kelele za kuvunjwa baraza la sasa la "mafisadi"!
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wengine sisi hatuishi Tanzania, Tunahitaji habari nzima kuliko hoja ili tuelewa yanayoendelea; kama nyie mko Nyumbani Msiwe wachoyo wa habari, mnatakiwa mtupe habari yote halafu mtoe hoja kuhusu hiyo habari

  Hapo ndio kutaonyesha Ushirikiano wa kuelimishana kuhusu kupeana habari toka Nyumbani - Sio Hoja
   
 14. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135


  Na hii ndiyo hoja ya Zito ya sahihi70 - Kwamba vote of no confidence inamlenga rais kuwa ni legelege au butu mkipenda kusema. Hivyo si aliyepinda au makinda ya kuku bali hata mpangaji wa nyumba yetu pale magogoni.
   
 15. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Blah bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla bla fuc shit bla bla bla bla bla bla!
   
 16. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slufay una roho ya paka kuweza kutoa maneno hayo wakati huu poole Mwee!!
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yeye si anajulikna kawekwa pale na siyo uwezo wake ulomfanya awe pale?!
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hiyo ulobold
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hiyo statement ulobold!?
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  siyo yeye pinda na makinda pekee ambao uwezo wao ni mdogo bali hata jk mwenyewe uwezo wao ni mdogo na ni legelege!
   
Loading...