Baraza jipya la mawaziri, nimehuzunika pia nimesikitika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza jipya la mawaziri, nimehuzunika pia nimesikitika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAZETI, May 4, 2012.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Nakosa maneno ya kuongea juu ya uchungu ninaousikia kwa Ndugu Rais kumrudisha tena G. MKUCHIKA. Nimesikitika mno na masikitiko haya si yangu peke yangu, ni masikitiko kwa wakulima wote wa korosho.

  Tunajua yeye ni miongoni mwa watu waliosababisha bei ya korosho kuwa ndogo.

  Nitafafanua hili siku nyingine lakini nieleze wazi tu kuwa kurudi kwa mkuchika ni MSIBA kwa wana MTWARA kwani ni mtu mbaya sana huyo!

  INASIKITISHA.
   
 2. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tupo palepale.
   
 3. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumefanyiwa danganya toto,watu ni wale wale ofisi tofauti,panaponukia kufa ni pale utumishi kwa Kombani
   
 4. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kama kawaida yake kamtoa wizara moja then anampeleka kwingine badala ya kubadili kabisa
   
 5. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade kwa nini umesema baraza jipya la mawaziri? kuna upya hapo? "kiraka kipya juu ya vazi kuukuu"
   
 6. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi mkuu, lile sio baraza jipya. Nimeteleza hapo
   
 7. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  sio huyo tu mi nna wawili ndugu b.mahenge naibu waziri wa maji na p. Mulugo nw elimu hawa gurudumu la maendeleo watalisukuma kuludi nyuma.
  Mfano b. Mahenge jimbo lake ni 1 kati ya majimbo maskini kuliko yote tz mfano halisi ktk jimbo hilo kuna watu wazima hawajawahi kuona gali so unaweza ukapata picha hali ya miundo mbinu sasa kama jimbo limemshnda anaongezewa mzigo hivi sijui itakuaje .
  Huyu mulugo alihusika na wizi wa mitihani ya 4m 4 ktk shule yake hadi ikafungiwa southen highland.
   
 8. i

  isoko Senior Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  katika sehemu aliyochemka ni pale utumishi katoa kiroba kaweka gunia kazi kubwa ipo
   
 9. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani Mkuchika anahusika vipi na kilimo badala ya kusikitika kwa ajili ya Prof Maghembe aliyekuwa Waziri wa Kilimo na kuendelea kurudishwa? Mimi nashangaa zaidi Adam Malima kubaki. Pia naona Mkuu ameteua Madokta na Maprofessa sijajua kama PHD zina msada sana katika kuongoza Wizara.
   
 10. E

  Elai Senior Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mheshimiwa umenena. Mulugo ni janga la taifa.
   
 11. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mimi bado naamini tunaweza kuwachambua mawaziri wa sasa kwa mtazamo wa kiutendaji ili tusaidie hata uongozi ujao utambua wananchi nao wanaonana wanelewa kuliko kulalamika bila kutoa mwelekeo au nini tulidhani ni cha kimaendeleo zaidi. Kwa mfano katika wizara ya afya ameweka madaktari na mabingwa wa public heath je kwingine amefanya kulingana nu uwezo, uelewa na ujuzi wa mtu au basi tuu? tujulize!! mfano mwingi ni Dunia ya sasa ni ya Nuclear hivyo ni sawa kumuweka Prof. Muhungo katika wizara ya nishati na madini? Dunia ya sasa ni ya sayansi na technolojia hasa ICT je Makamba ataweza kufanya kazi na Prof. Mbarawa katika wiza aliyopewa, anao uwezo, ujuzi na uelewa wa mabo hayo au amepewa tu? Nadhani hapa ni kazi yetu kufanya uchambuzi wa kila mtu na namna tunavyoona ataweza kufanya kazi. Wapo watu wengi tu ambao ni kero katika baraza la mawaziri tunaweza kusema wamebebwa tu na siyo kuwa na uwezo labda kwa kuwa wanasimamia sera ila ha hivyo sera bila utambuzi hi bure.

  Mimi ni ushauri tu hasa kwetu sis tunaopenda kulaumu na kulalamika bila kutoa what we think is the best solution kwa matatizo yetu.
   
 12. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,053
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Si kaomba chama chake idhini ya kufanya hayo aliyofanya? Eti rais mzima hawezi kuamua mpaka aamuliwe na Chama baada ya kutumia fedha chungu nzima kodi za Watanzania! Huyu jamaa hana uchungu wala huruma na Watanzania. Afadhali hata ya Mkoloni.
   
 13. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,896
  Likes Received: 2,315
  Trophy Points: 280
  Mkuu hisia zako zibaki kuwa hisia zako.
  Kama humpendi mtu kwa sababu humpendi tu, basi hapa si mahali pake.
  TOA sababu za kutompenda Mkuchika bila kumung'unya maneno, ama sivo utahesabika kama mpiga majungu.

  Huyu jamaa (Mkuchika) hajamuibia mtu, kama mmegongana kona hilo liwe lenu.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,798
  Trophy Points: 280
  mkuchika ana nyodo yaani anapoongea hasa bungeni ni kanakwamba wengine ni mapimbi tu! hafai hata kwa kulumagia.
   
 15. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Hivi hakuwemo katika wale 8 waliotakiwa kujiuzulu?
   
 16. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Siku nyingi kulikuwa na tetesi kuwa naye ananufaika katika zao la korosho
  kupitia vyama vya ushirika. Wakulima walipoanzisha umoja wao na kuamua
  kuuza wenyewe ghalani, Kupitia TAMISEMI wakazuiwa hamna kufanya mauzo
  wao wenyewe bila kutumia mfumo huo.
  Wakulima wakaamua kuonana na waziri mkuu DODOMA ili kufikisha malalamiko
  yao, badala yake akajitokeza mkuchika na kudai kuwa waziri mkuu ana kazi nyingi
  badala yake kama wana matatizo yoyote wayafikishe kwake.
  Sijui wanakula wote na mkuu wa Kaya?
   
 17. m

  maingu z Senior Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu solution katika matatizo yetu ni sisi watanzania wenyewe ambao hao waliomo humo ndo tuliowachagu, ni kweli sasa kama tumechagua vibaya mnategemea maendeleo yatoke wapi. Nakuunga mkona kabisa hakuna sababu ya kulalamika, wakati wa upigaji kura tulikuwa na choice nzuri ya kufanya badala yake mkawaweka hao tena kwa ushabiki tu wa kisiasa wala hatukuangalia kama wako commited. Huu ni mzigo wetu wenyewe tutulie chamoto tukione, na mjifunze kufanya mabadiliko. Ili noa wajue kuwa mnaweza kufanya chochote, lakini tangu uhuru mpaka leo, angalieni ni sisi tu watanzania ndo bado tumeng'ang'ania chama kilichopigania uhuru mpaka sasa wenzetu karibuni wotu wameshafanya mabadiliko.
   
 18. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii nchi ni inatokana na wasanii na itaendeshwa kisanii tu,watu(mawaziri)wameiba/wamekula rushwa hawajaguswa na yeyote unatazamia hawa wa sasa wataiga nini zaidi ya kula ukizingatia hakuna binaadamu anaechukia kula?Hii ndio nchi yetu hali ikibana vizuri watu ndio wataamka Kama sio kustuka Ila kwa sasa ukiwapa somo hawakielewi kabisaa
   
 19. m

  maingu z Senior Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si mkuchika wala mawaziri, tatizo ni rais, hayuko sirious na matatizo ya wananchi, ndo maana anaendelea kuteua utumbo, kwa hiyo kwa mheshimimiwa huyu watz msitegemee la maana, tulichagua mzigo si mchezo. Ingawa si vema kuzungumzia ukabila lakini wakati mwingine historia inatushitaki tangu lini wacheza mdundiko wakawa na sifa ya uongozi, hata machifu hawakuwepo, hapo anakotoka ndo ilikuwa njia ya watumwa, ina maana hakukuwa na ukinzani, kazi ilikuwa ni kucheza ngoma tu.
  So natumaini tumepata somo, wakati wa uchaguzi sio lele mama, kwani watz tunachukuli suala la viongozi ni ushabiki tu, wanasahau kuwa tunawakabidhi dhamana ya mali zetu na utu wetu hao tunaowachagua,
   
 20. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mbaya ni kwamba katika biashara ya mazao wanasiasa wamekwisha kuwa madalali na makuwadi wa wafanyibiashara wakubwa,siyo rahis kwa mtu kama Mkuchika kutokuwa na maslahi kwenye biashara ya korosho au ufuta mazao yanayostawi vizuri huko kusini au kunuliwa na wahindi wanaofanya biashara hiyo ya mazao ili wakidhi maslahi yao.Kumbuka pia vizuri kanuni nyingi za manunuzi ya mazao zinatungwa na Halmashauri ambazo Mkuchika alikuwa anasimamia.Ni kama hivi sasa zao la pamba lilikwisha vurugwa na wanasiasa makuwadi kama Kigwangalah na kamapuni yake ya MSK, hawa hawawezi kuwa rafiki wa mkulima hata siku mmoja maana wanajua ndiye chakula yake.
   
Loading...