Baraza jipya la mawaziri litakuwa ni la manufaa nchini iwapo tu haki itatendeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza jipya la mawaziri litakuwa ni la manufaa nchini iwapo tu haki itatendeka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JF-MBUNGE, May 1, 2012.

 1. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa takribani wiki sasa watanzania maofisini,vijiweni na hata mabarabarani kwenye vyombo vya usafiri wamekuWa wakimsifu na kumshukuru Mh. Rais kwa usikivu wake juu ya vilio vya wabunge na wananchi kwa ujumla khs utendaji mbovu wa baraza lake la mawaziri. Hii inaashiria kuwa watanzania wanamatarajio makubwa na baraza jipya la mawaziri litakalo tangazwa hv karibuni. Hivyo basi, hii ni fursa nzuri sana kwa JK na wasaidizi wake kuteua mawaziri wachapakazi ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao na chama tawala kwa ujumla.


  Wananchi wengi wamekua wanazungumza haki kwa maana ya kuwajibisha mawaziri wote ambao hawajafanya vzr ktk wizara zao na kutumia uwaziri kujilimbikizia mali. Haki itendeke kwa maana gani? Itakua si haki kwa mfano kumtoa waziri wa serikali za mitaa MH. Mkuchika eti tu kwa makosa yalivyoongelewa kwenye wizara yake kwenye bunge lililopita na kumrudisha waziri C. Kombani ambaye ndiye aliyekuwa waziri wa TAMISEMI kabla ya MH. Mkuchika, hasa ukizingatia madudu mengi yaliyoongelewa ya ubadhirifu katika wizara hiyo yalitendeka kipindi cha Mh. C. Kombani na Mh. Mkuchika kuyakuta. Kwa maana hiyo mawaziri wenye record mbaya zamani na sasa pia wawajibishwe hata kama wizara wanazoziongoza sasa hazikutaja sana kwa ubadhirifu ktk kikao cha bunge kilichopita.


  Mfano mwingine ni kuwa kumekuwepo na hoja kuwa mawaziri wanaotakiwa kuondolewa ni wale tu waliotajwa kushindwa kusimamia wizara zao ipasavyo kwenye kikao cha mbunge kilichopita hata kama makosa hayakutendeka kwenye uongozzi wao. La-hasha, huku mtaanii na wantanzania walio wengi hawazungumzi hivyo tu, bali kwa ujumla wao wanahitaji hata wale mawaziri ambao wizara zao zilifanya vibaya kipindi cha nyuma na kuliletea taifa hasara nao waondolewe…hapa **** mfano wa waziri wa ulinzi tukumbuke mabomu ya gongola mboto wengi walihitaji political responsibility ktk hili lkn haikutokea hilo halikutokea…,hivyo basi ni fursa nzuri ya kuwapumzisha wahusika wizara hii pia….si haki kuwarudisha kwenye baraza wachache walioshindwa kuendesha wizara zao kiufanisi, na kufukuza wengine.


  Haki ikitendeka jamii itaielewa serikari na kurudihsa imani kwake.


  Source:MIMI-mwakilishi wa wananchi JF
   
 2. r

  raffiki Senior Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwatoa kwenye baraza la mawaziri tu haitoshi....inatakiwa warudishe na fedha za umma walizovuja na na maharamia wa nchi hii..ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
   
Loading...