Baraza jipya la Mawaziri kujulikana Feb 12

JK ni CCM damu na haamini katika Upinzani kwa undani ila kwa nje. Ana chuki mbaya na upinzani na hata imefikia sasa anaogopa kuwa na Mgombea binafsi. JK anasema yote ila chini kwa chini wanawanunua wapinzani. Makamba anafanya haina maana kwamba JK hajui haya. Wako wapi akina Tambwe and the likes. JK anaweza kufanya mabadiliko lakini si kuwapa wapinzani nafasi. Mimi wala siombei wapewe nafasi ila sheria ya Uchaguzi ziwe huru kabisa hapo utaona watakavyo washindwa CCM na kuichukua Nchi. Kazi ni kubwa hata donors wamegomea pesa zao hadi waone mwelekeo JK ana mengi moyoni .Anavyo penda safari kaacha kwenda Ulaya? Kweli yamemfika.

Kuna taarifa kwamba JK anafikiria kuwateua Mh. Zitto na Mh. Rashid Mohamed kuwa katika baraza jipya la mawaziri .... inasemekana ndiyo sababu halijatangazwa bado; akiamua hivyo atawaita leo (kama bado hajawaita); ili kuweka mambo sawa .... vinginevyo kesho baraza ni CCM watupu.
 
::::Mchungaji Rwakatare kupewa uwaziri??????
stay in tune masaaa 18 yajayo...kumeiva
:""""DODOMA""""
 
Kama ni kweli Chegeni anarudi,na nahisi ni jambo hili linaweza kumng'oa Diallo coz hawa ni wapinzani wa jadi.ila nina wasiwasi sana na hili
 
Hata mimi nimesikia habari za kuwasiliana na wapinzani. Nakumbuka JK alisema mwaka huu anataka aongeze ushirikiano na vyama pinzani, sijui ushirikiano to what extent!
 
Kati ya hawa wajumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi lazima watakuwapo katika baraza la mawaziri la kesho.ukimuondoa Lowassa,Chenge ila wengine wana nafasi swa kubaki ila kulinda maslahi ya chama

1.Andrew Chenge
2.Edward Lowassa.
3.Pindi Chana
4.Dk. Abdallah Kigoda
5.Abdulrahman Kinana
6.Anna Makinda
7.Zakia Meghji.
8.Yussuf Makamba
9.Saleh Ramadhan Ferouz rieti.
10.Kapteni George Mkuchika
11.John Chiligati
12.Bernard Membe
13.Pius Msekwa
14.Dk. Maua Daftari
15.Mohammed Gharib Bilal
16.Muhammed Seif Khatib
17.Omar Yussuf Mzee
18.Yussuf Mohammed Yussuf
19.Kidawa Hamid Salehe
20.Fatma Said Ali

hapa chini ni tathmini za kipindi kile.

Habari ambazo haziwezi kuthibitishwa kwa haraka zinaeleza kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwa wanasiasa hao wawili; Mwambi na Mwanri, kuingia katika Baraza la Mawaziri la Kikwete linalotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.


Je JK atamrudisha Rostam?
Aidha, baadhi ya wadadisi wa mambo wanampa pia Rostam ambaye kitaaluma ni mchumi, nafasi ya kuingia katika baraza hilo jipya la mawaziri akiwa na nafasi kubwa ya kuongoza Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko ambayo sasa inashikiliwa na mwanasiasa wa siku nyingi, Basil Mramba.
 
Hivi hawa mashujaa wapya kina anna kilango and some other guys from CCM camp pale bungeni wametoka wapi??? Mi naona wote mbofu mbofu tu!!! Wamemeza pini muda mrefu wakati ufisadi unaendelea ncini. Hivi mpaka mwakyembe atoe riport ndio wajifanye wazalendo??? Wabunge wa CCM walichofanya ni kama kutubia dhambi zao tu lakini hamna ushujaa wowote walioufanya.

Mtu akiniambia, Zitto, Slaa, Hamad Rashid and the likes ni mashujaa bungeni nitamuelewa, lakini kilango?? eti kwakuwa kamkoromea Lowassa!!! Hivi nyie, nani hakujua skendo la Richmond??? Walikuwapi muda wote huo??? Mbona hawakomai kuhusu BoT????

By nature, midomo ya wabunge wa CCM imefungwa, kukemea skendo za serikali!!! hawahitaji kupewa uwaziri kuiziba!!!!! kilichofanyika dodoma ni kama mchezo wa kina zembwela!!!!!

Hebu acheni kuwapa watu ushujaa wa bure, hicho ni cheo kitakatifu hakipewi mafisadi wa namna yoyote ile. Wezi, Marafiki wa Wezi na hata walezi wa wezi!!!!!
 
Kuna utashi kuwa kuna Mawaziri wa zamani watarudi na huo ni mtego kwani kuna ufisadi unawagusa hawa na ripoti zake bado hazijawakilishwa ,hivyo kuwaondoa kwa wakati huu ni kuwaruhusu wakimbie hivyo watabakishwa wakati Muungwana ameshajua watanasa katika raundi ya pili na hakuna isipokuwa watawajibika na ndio utakuwa mwisho wao ,kwa hivyo msije mkerusha mawe wakati bado mpira unachezwa na pambano la mwanzo limeanza walioanguka tumewaona.Na mtawajua tu kwani wamehusishwa moja kwa moja katika mechi zingine.
Aluta kontinyuwa ..viva Kikwete Viva Tanzania.
 
Baraza la Mawaziri: Moshi mweupe sasa kuonekana Jumanne
* Yadaiwa atapunguza mawaziri 20
* Tetesi za kuteua Zitto, Mdee zaenea

* Wapinzani wasema hawana habari


Na Muhibu Said


RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzima shauku kubwa na ya muda mrefu ya Watanzania kwa kutangaza Baraza jipya la Mawaziri, mjini Dodoma Jumanne baada ya kuahirishwa Jumatatu


Shughuli hiyo ambayo awali ilitarajiwa kufanyika saa 11:00 jioni, itafanyika Jumanne saa 4:00 asubuhi, katika Ikulu Ndogo ya Chamwino, mjini hapa.


Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premy Kibanga amethibitisha suala hilo kupitia taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana.


"Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kutangaza Baraza la Mawaziri kesho (leo) Jumanne

(12/02/2008) saa 4.00 asubuhi katika Ikulu Ndogo ya Chamwino, Dodoma," alisema Kibanga na kuwataka wahariri, waandishi, wapiga picha kuwasili katika eneo hilo saa 3.00 asubuhi, ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda.


Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Rais kuvunja Baraza la Mawaziri wiki iliyopita kutokana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa huo kufuatia kuhusishwa kwenye kashfa ya upendeleo katika zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond Development ya Marekani.


Kutokana na hatua hiyo, Alhamisi wiki iliyopita, Rais Kikwete alimteua aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu mpya.


Pinda ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mashariki (CCM), aliapishwa kushika wadhifa huo siku iliyofuatia.


Ijumaa wiki iliyopita, Spika wa Bunge, Samwel Sitta aliliambia Bunge kuwa alikuwa na fununu kwamba, Rais Kikwete angetangaza baraza hilo jana.


Taarifa hiyo ambayo jana ilitawaliwa karibu vyombo vyote vya habari, iliwafanya Watanzania kusubiri suala hilo kwa hamu na shauku kubwa, kabla ya Ikulu kutoa taarifa rasmi jana mchana kuuarifu umma kwamba, shughuli hiyo itafanyika leo.


Hata hivyo, Sitta alikaririwa na kipindi cha Harakati kinachorushwa hewani na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) jana jioni akisisitiza kuwa taarifa za kutangazwa kwa Baraza jipya la Mawaziri jana, zilitolewa na Ikulu na kwamba uamuzi wa kuahirisha hadi leo, uko nje ya mamlaka yake.


"Ni Ikulu ndio waliosema, sasa kama kuna kuahirishwa, jambo hilo si letu, na mimi sina uwezo wa kumpangia Rais siku ya kutangaza," alisema Sitta kupitia kipindi hicho.


Hata hivyo habari zilizopatikana jana zinadai kuwa, awali, Baraza jipya la Mawaziri lilitarajiwa kutangazwa jana.


Lakini shughuli hiyo ikaahirishwa baada ya Kambi ya Upinzani kukataa uteuzi wa baadhi ya wabunge wao kuingizwa katika baraza hilo kwa madai kwamba hawakushirikishwa katika mchakato huo.


Baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani wanaodaiwa kuingizwa katika baraza hilo, ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Halima Mdee, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.


Zitto alipoulizwa na mwandishi wa Mwananchi jana, alikiri kupigiwa simu na watu wa kada mbalimbali za kumpongeza kwa kuteuliwa kuwamo katika Baraza jipya la Mawaziri, lakini akasema hajapata taarifa za uteuzi huo.


Nao Mdee na Hamad walipoulizwa kwa nyakati tofauti jana, walisema hawajapata taarifa zozote kuhusiana na uvumi huo.


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, alipoulizwa alisema hajapata taarifa za kuteuliwa kwa mbunge wao yeyote, lakini akasisitiza msimamo wa chama chake kwamba, hawatakubaliana na uteuzi huo.


"Lazima kuwapo na majadiliano na makubaliano kabla ya kuamua uteuzi huo na siyo jambo hilo zito lifanywe kwa mtu mmoja mmoja pekee, ndivyo inavyofanyika duniani kote," alisema Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema).


Habari zilizopatikana jana zinafahamisha kuwa, Baraza jipya la Mawaziri limefanyiwa mabadiliko makubwa kwa kupunguza idadi ya mawaziri na manaibu wake.


Imeelezwa kuwa, katika mabadiliko hayo, idadi ya mawaziri imepunguzwa kutoka mawaziri 29 waliokuwapo zamani hadi kufikia mawaziri 25 wa sasa.


Pia, idadi ya manaibu mawaziri imepunguzwa kutoka 31 wa zamani hadi kufikia manaibu mawaziri 15 wa sasa.
 
Akipunguza mawaziri 20 litakuwa jambo zuri sana. Manaibu wengi ni kama wanakuwa hawana kazi zaidi ya kujibu maswali bungeni.

Pale panapokuwa na naibu ni vizuri apewe majukumu ya kushughulikia na sio
kukaimu pale tu waziri anapokuwa safarini.

Kama ni kweli manaibu kupungua kutoka 31 mpaka 15, ina maana kuna watu wengi sana watalia.

Wapinzani, kubalini kuchukua hizo nafasi, ni nafasi ya kujifunza. Vyama havitabanwa kuitetea serikali na badala yake ni hao mawazili tu ndio watatakiwa kuwajibika kwa pamoja na serikali.

JK akifanya hivyo atabeba sifa nyingi toka kwa Watanzania.

Nakumbuka PM Brown alifanya hivyo hapa UK na wananchi wengi walifurahia, I hope itakuwa hivyo kwa TZ pia.
 
Akipunguza mawaziri 20 litakuwa jambo zuri sana. Manaibu wengi ni kama wanakuwa hawana kazi zaidi ya kujibu maswali bungeni.

Pale panapokuwa na naibu ni vizuri apewe majukumu ya kushughulikia na sio
kukaimu pale tu waziri anapokuwa safarini.

Kama ni kweli manaibu kupungua kutoka 31 mpaka 15, ina maana kuna watu wengi sana watalia.

Wapinzani, kubalini kuchukua hizo nafasi, ni nafasi ya kujifunza. Vyama havitabanwa kuitetea serikali na badala yake ni hao mawazili tu ndio watatakiwa kuwajibika kwa pamoja na serikali.

JK akifanya hivyo atabeba sifa nyingi toka kwa Watanzania.

Nakumbuka PM Brown alifanya hivyo hapa UK na wananchi wengi walifurahia, I hope itakuwa hivyo kwa TZ pia.



Maneno mazito haya wacha tuone itakuwaje kwa kweli .
 
Kuna tatizo mbona kunakuwa na habari tofauti...wengine wanadai ni leo saa 4.00 asubuhi na kwamba wahandishi wa habari wanatakiwa wawe wamefika Ikulu ndogo ifikapo saa 3.00 asubuhi...sasa tushike lipi...


:(:confused:
 
Ha ha haaa..... Unajua wakati mwingine mtu unajiuliza kuna maana gani kutangaza kwamba utachelewesha kutangaza baraza la mawaziri (such a sensitive issue) na kuahirisha mara 2???@#$?%

Mi nadhani Muungwana yeye ajipumzikie huko Chamwino kisha akiwa tayari alirushe tu manake inachosha hii kiu ya kutumia muda wa hewani (radio) kutuletea habari za kuahirishwa!!!!

Kwa mwendo huu sijui kama tutafika.....
 
Kuna tatizo mbona kunakuwa na habari tofauti...wengine wanadai ni leo saa 4.00 asubuhi na kwamba wahandishi wa habari wanatakiwa wawe wamefika Ikulu ndogo ifikapo saa 3.00 asubuhi...sasa tushike lipi...


:(:confused:

Wamesema ni saa tisa mchana na ukumbi ni Tamisemi

Source TVT
 
Ratiba imebadiliswa badala ya Saa nne asubuhi ,,,ni Mchana

TUAMINI TAARIFA IPI???

taarifa toka ikulu ndogo ya chamwino
Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kutangaza Baraza la Mawaziri kesho - Jumanne (12/02/2008) saa 4.00 asubuhi katika Ikulu Ndogo ya Chamwino, Dodoma.

Wahariri/Waandishi/Wapiga picha wawe wamewasili ifikapo saa 3.00 asubuhi, na wale wenye waandishi wao Dodoma wawaelekeze vyema ili wazingatie muda.

Vyombo vya Televisheni vinavyohitaji kutafuta signals na kuweka vyombo vyao sawa wanaweza kuja kuviweka leo jioni au kesho mapema asubuhi pale Chamwino. Tafadhali TVs ziweke scrolling message ili wananchi waelewe pia.

Wale wote watakaochelewa kufika hawataruhusiwa kuingia pindi Rais akishaingia.

Tunaomba tushirikiane kufanikisha kazi.

Ahsante na karibuni.


P. Kibanga
MHRM
Ikulu, Chamwino
DODOMA.
11/02/2008

© Michuzi Tarehe: 11.2.08 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3

Hapa kuna kitu si bure......
 
Back
Top Bottom