Baraza jipya la Mawaziri: Geofrey Mwambe na Dkt. Philip Mpango turufu mpya za ukuaji wa uchumi katika awamu hii ya mwisho ya Rais John Magufuli

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
1,000
BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI:MH GEOFREY MWAMBE NA DKT PHILIP MPANGO TURUFU MPYA ZA UKUAJI WA UCHUMI KATIKA AWAMU HII YA MWISHO YA RAIS JOHN MAGUFULI.

Leo 13:25hrs 06/12/2020

TIC ndio mzizi uliosimikwa chini kwa Maendeleo ya Taifa la Tanzania,TIC ina wajibu wa kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora kwa wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali,hii ni kutokana na kuwapo kwa uchumi imara sambamba na mazingira bora ya uwekezaji,uwepo wa ardhi, watu, nishati, masoko na sera bora,kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC ndio jicho au sura ya Taifa la Tanzania mbele yawawekezaji kuja kuwekeza kwenye miradi ya viwanda, kilimo, uzalishaji wa mafuta ya kula, uzalishaji wa sukari, uongezaji thamani mazao ya uvuvi, uunganishaji wa magari, uzalishaji wa madawa na vifaa tiba, ujenzi wa hospitali na utalii,haya yatafanya Uchumi wa Tanzania kukua na kuendelea kukua kwa kasi katika siku zijazo,ili kuifanya ndoto hii kuwa kweli Mh Rais John Magufuli amemteua Mh Geofrey Mwambe aliyekuwa Mkurugenzi wa TIC kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara,

Mh Geofrey Mwambe akiwa Tic amekuwa nguzo kubwa ya ukuaji wa kiuchumi hasa kwa kusimamia multiplier effects ambayo ndiyo inazaa mazingira wezeshi ya kibiashara,tunapoona TRA inakusanya kodi kubwa basi sifa za kwanza zilistahili kwenda TIC kwa Mh Geofrey Mwambe ambaye amefanya mazingira bora na kuiwezesha TRA kukusanya kodi kwa siku,kwa wiki,kwa mwezi na kwa Mwaka, Mazingira wezeshi ya kibiashara ndiyo yanayofanya tra kuvuka malengo na kuvunja rekodi ya ukusanyaji mapato,tunapoelekea kwenye Mapinduzi ya nne ya kiviwanda kama yalivyoandikwa kwenye andiko la Profesa Mathew Luhanga,Tanzania haitabaki nyuma,Tanzania inaingia kwenye Mapinduzi ya kiviwanda awamu ya nne,na Wizara ya Viwanda na Biashara itakwenda kushika hatamu na kutegemewa katika Uwekezaji wa Viwanda na Biashara kuleta matokeo chanya kwenye Pato la Taifa na Uchumi wa nchi kwa ujumla.

Waziri wa Fedha na Mipango,Daktari Philip Mpango ambaye anasimamia fedha na mipango ya Serikali ataungana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Geofrey Mwambe,wakitumia taaluma mbili,taaluma ya Uchumi(Economics)na taaluma ya uhasibu(Accounting) wakisimamiwa na taaluma ya Uongozi (Management) wakitekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu,maadili,Sheria,kanuni na taratibu za utumishi wa Umma,kwa ushirikiano wao kufanya kazi kwa weledi,bidii na kushirikiana na kila mmoja katika nafasi yake ili kuboresha Utendaji kazi daima wataongeza mapato ya Serikali,kwa uchambuzi na usimamizi wa sera za Taifa na bajeti kuu ya Serikali itatosha,Nina imani kama sasa tunakusanya trioni 1.2 kwa mwezi basi miradi mikubwa itakapoisha Mwaka 2025,Taifa letu la Tanzania litakuwa linakusanya kodi ya trillioni 4 kwa mwaka.

-Taaluma ya Uchumi,Taaluma ya Uhasibu,Taaluma ya Uongozi,Taaluma ya Sheria.

Hizi ni taaluma nne ambazo daima zinasimamia Utendaji wetu katika shughuli zetu za kila siku,taaluma ya Uchumi,Uhasibu,Uongozi na Sheria,mfano Mfanyakazi wa Serikali kapewa Millioni tano katumwa kwenye semina Arusha,baada ya kufika Arusha stendi akaibiwa hela zote,kwa taaluma ya Uongozi,huu ni Uzembe,kwa taaluma Uhasibu hii ni audit query,kwa taaluma ya sheria hii ni criminal offence na kwa taaluma ya Uchumi hii ni Hongera kwa mwizi maana atachukua zile hela atapanda taksi,ataenda dukani kuoga atanunua nguo begi zima,ataenda kwa Mromboo ataagiza mbuzi mzima,baada ya hapo ataenda kulala Singita,kule Serengeti,huo ni Mzunguko wa hela ambao utauchukulia kama msaada mkubwa wa ukuaji pato la mtu mmoja mmoja,

Taaluma ya Uchumi ndio inakwenda kuzaa Taaluma ya Uhasibu na katikati yao zinaunganishwa na Taaluma ya Management kama ethics na code of conduct,Waziri Mpya wa Viwanda na Biashara,Mh Geofrey Mwambe ambaye alikuwa Mkurugenzi wa TIC hapo kabla akihusika na multiplier effects,uwekaji wa mazingira bora ya Uwekezaji,mfano kutoa msamaha wa dola millioni 10 kwa Hotel kubwa labda Ngurudoto na baada ya msamaha huo,kutegemea kurudisha pesa hiyo kutoka kwenye bill ya Umeme itakayotumia hotel hiyo,billi ya maji itakayotumia hotel hiyo,ajira itakayotengenezwa na hotel hiyo,sasa Mh Geofrey Mwambe anakwenda kuprove multiplier effects,mazingira bora ya Uwekezaji yalete tija katika Wizara yake Mpya ya Viwanda na Biashara.

Taaluma ya uchumi ni sayansi ya kijamii ambayo utafiti uzalishaji, usambazaji, na matumizi ya bidhaa na huduma pia hushughulija na kuanguka kwa masoko mfano Uchumi wa Sekta ya umma,iwapo masoko uanguka basi aina fulani ya uthibiti ufanyika,hapa ndipo Mh Geofrey Mwambe kama Waziri wa Viwanda na Biashara atakwenda kushughulika nako,uchambuzi wa gharama,uchambuzi wa faida, kuangalia multiplier effects iwapo kampuni itafungiwa biashara nini kitatokea na iwapo Kampuni itapewa msamaha wa kodi faida gani itapatikana kwa kukusanya kutokana na ulipaji wake wa billi za maji,Umeme na ajira atakazozalisha,Je viashiria vya kukua kwa Uchumi kulinganisha Pato la Taifa kati ya Mwaka uliopo na ulioisha na pia kulinganisha kipato cha mtu kati ya Mwaka uliopo na Mwaka ulioisha,iangaliwe kukua kwa Uchumi ajira imeongezeka au imetoweka,Je ubora wa maisha umeongezeka,je usawa wa kipato baina ya mtu na mtu,na kuwa na mazingira endelevu.

Nimalizie kwa kusema,hakuna nchi bila kodi,tusiendekeze wahuni na kuleta siasa,kukwepa kodi ni asili ya Mwanadamu ndio maana zimewekwa Sheria kuhakikisha Serikali inapata kodi yake,Ulaya wanakamatwa akina Messi na Ronaldo kwa kukwepa kodi na wanapelekwa Mahakamani,huku uswahilini tunaleta siasa!? Je mnataka TRA ivunjwe kodi isiwepo ili tutumie siasa badala ya kodi kuendesha nchi yetu!? Niipongeze Serikali makini ya awamu ya tano,nimpongeze Rais John Magufuli kwa kutafuta watu wazuri kwa ajili ya nafasi za Uwaziri,watu wazuri kwenye Principles na Practice of Leadership,Innovative,Creative,result oriented, problem solvers, analytical minded and critical thinkers,kwa hakika ukiwa na sifa hizi bila kutafuta sifa mitandaoni au kwenye Vyombo vya habari,siku isiyo na jina,state machineries za mamlaka ya uteuzi zilizosambaa nchi nzima zitakupendekeza upewe nafasi inayoendana na uwezo wako ili ukatoe mchango mkubwa zaidi kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania,kwa ufupi uwe na sifa za kocha ili upate nafasi Uwanjani ya kocha mchezaji.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,703
2,000
Mwekezaji gani mpumbavu atakuja kuwekeza pesa yake jehanamu?

sifa mbaya za nchi hii Kwa wawekezaji ni ngumu Sana kumshawishi kuja Tanzania....miaka 5 ya magufuli imepita bure bila wawekezaji sembuse miaka hii mingine ya jasho na damu!!!
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
14,597
2,000
Masisiemu Sasa ndio yamejua kiasi ambacho magufuli hawaamini.

Yaani kawapa Watoto wake, Na mbuzi za chadema alizonunua mnadani na zile ng'ombe za jalalani udsm pale bila kusahau lakezonelization, watu wa Kanda ya ziwa.

Masisiemu yamepigwa na butwaa
 

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
10,360
2,000
Ukimsifu mgema tembo hulitia maji uadilifu na uchapaka kazi wao ndio silaha kuu ya maendeleo!
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,721
2,000
Mwekezaji gani mpumbavu atakuja kuwekeza pesa yake jehanamu?
sifa mbaya za nchi hii Kwa wawekezaji ni ngumu Sana kumshawishi kuja Tanzania....miaka 5 ya magufuli imepita bure bila wawekezaji sembuse miaka hii mingine ya jasho na damu!!!
Acha hofu mkuu,chapa kazi,kufika uchumi wa kati ni pamoja na kubanana wenyewe kwa wenyewe,there is always no easy task,ni kweli inauma ila vumilia kidogo, hii ni kwa ajili ya watoto wetu na wajukuu zetu...
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,084
2,000
Chini ya Utawala huu hakuna waziri yeyote atatumia akili zake kwenye swala lolote hata kama ni kwa manufaa ya Taifa , Waziri ni yule aliyewateua tu, ukitaka kuthibitisha hili waite chemba mawaziri waliopita wa awamu ya 5
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom