baraza awaasa wachezaji wa Africa

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,501
183
MSHAMBULIAJI wa timu taifa ya Kenya 'Harambee Stars' John Baraza ametoa usia kwa wachezaji wenzake wanaoshiriki michuano ya Cecafa kwa kusema kama wanataka kucheza soka kipindi kirefu basi waachane na tabia zisizofaa nje ya uwanja.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam, Baraza ambaye anaichezea pia klabu ya Sofapaka alisema kuwa nidhamu mbovu nje ya uwanja ndio sababu iliyofanya mastaa wengi wapotee katika ramani ya soka wakati umri wao bado unaruhusu.

Baraza ambaye amewahi kuichezea Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000 alisema kuwa wachezaji wengi hasa wa Kiafrika wameshindwa kudumisha nidhamu zao nje ya uwanja pale wanapopata umaarufu kidogo hali ilinayowapelekea wasidumu katika soka.

"Uwezi kufanya vizuri katika soka na mchezo wowote ule kama utakuwa na tabia zisizofaa nje ya uwanja, utakuta mchezaji amepata umaarufu kidogo tu anaanza tabia za ajabu ikiwemo utumiaji wa madawa ya kulenya na umalaya sasa hapo unategemea atacheza kwa mafanikio muda mrefu kweli,"alisema Baraza.

Baraza ambaye ameendelea kuwa moto wa kuotea mbali kwa kufumania nyavu amemaliza msimu wa ligi kuu ya Kenya akiwa mfungaji bora kwa mabao 15. Pia katika msimu wa mwaka jana Baraza alifungana na mshambuliaji wa klabu ya KCB, Ezekiel Odera.
 
Karibuni sana kwenye forum ya michezo tunaomba msilete sihasa huku
 
Nilianza kumsikia Barasa nikiwa primary school,nilimsikia kabla hata ya Kuwasikia kina Ulimboka,Pawasa,Costa,lakini ajabu huyu Barasa bado anapeta wakati hawa wenzetu sasa ni maveterani wa soka la bonanza.Si Barasa tu,kuna Mark Sirengo,Sunguti na Musa Otieno hawa bado wanacheza wakati sisi wachezaji wa Kitanzania wenye umri wao tulishawasahau zamani.
 
Baraz amekuwa mzee wa hekima now dayss ameacha bangi au???????
 
Hivi kauli hiyo inawahusu wachezaji wa timu zote zinazoshiriki (i.e., Ivory coast, Malawi, na Zambia?)... Baraza fafanua.....:target:
 
Back
Top Bottom