Baraka za Wazazi

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
BARAKA ZA WAZAZI

Baraka zinazoachiliwa na wazazi wa kimwili baba yako na mama yako,ni nyingi kuliko zinazopatikana kwa wazazi wa kiroho.(manabii nk)

Umeshonea suti manabii na wachungaji,baba yako hujawahi kumfanyia hivyo

Ni mkarimu sana kwa nyumba ya mchungaji au manabii Nyumbani mara ya mwisho kumtumia mama yako ya vocha ilikuwa mwaka juzi.

Na wengine wazazi wenu ni ombaomba au wanaishi kwa Ndugu, halafu wewe unahudumia manabii

Wengine hamuendi hata nyumbani, bize mjini mnakanyaga mafuta.

Ukitelekeza wazazi wa kimwili ukawa bize na wazazi wa kiroho baraka utazisikia tu

Mungu anawatumia sana wazazi wako,lipo kusudi la wewe kukupitisha kwenye tumbo na kiuno hicho.USIWACHUKULIE POA ETI.

Look back to your parents INSTEAD of prophets
 
Hata mimi nawashangaa watu wanaotenga pesa kwa ajili ya manabii wao na mababa na mama wa upako wao.....wale jamaa ni wasanii tu hawana lolote zaidi ya kuwachezea waumini wao akili. Siamini kama kweli waumini wanakuwa na akili timamu kufanya wayafanyayo.
 
tena dada zetu siku hizi hawa manabii sijui wanawapa nn, unakuta mtu mda wote ni kumpost huyo mchungaji wao kwa caption ya daddy, mara cjui my father...kanisani kila mara hela wanazitoa kweli huko halafu unakuta home pagumu
 
Back
Top Bottom