Baraka za ccm juu ya mgombea binafsi ni mbinu ya kupunguza wanaccm wanaokimbilia upinzani.

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Wimbi la wanaccm wanaohamia upinzani na hasa chadema limeelezwa kuwa ni mojawapo ya sababu za CCM kukubali mgombea binafsi.

Wanaccm ambao watakuwa wamekichoka chama hicho watapata fursa ya kugombea binafsi bila kulazimika kwenda chama cha upinzani.

My take: CCM wamepigana kufa na kupona mahakamani kumkataa mgombea binafsi na kesi bado inaendelea ni nini kimewafanya wageuke ghafla , kama kweli wanahitaji mgombea binafsi wangetangulia kufuta kesi iliyopo mahakama kuu.

Mwaka 2015 wagombea ambao wataondoka CCM watagombea kwa tiketi ya mgombea binafsi badala ya kwenda upinzani. Fursa hii itaipa CCM kuwa na wabunge wengi.

Chadema kuweni macho mnahitaji mkakati badala ya kushangilia.
 
Kuna uwezekano pia kuwa wale watakaotemwa na CCM kwa mizengwe wakakibomoa kabisa na hivyo mgombea wao wa urais akaambulia patupu!
 
Back
Top Bottom