Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,800
Wakati anaingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude Kili Stars ilikua imezidiwa kabsa eneoa lote la kiungo. Mzamiru alikua kapotea vibaya. Mkude alikua hoi kachoka hali iliyopelekea kufanya faulo nyingi. Ili kukwepa kadi nyekundu ilibidi Mgunda afanye sub. ya lazma na hapo ndipo Matogolo alipoingia. Kwa kweli jamaa aliwapoteza Wakenya kabsa. Ndani ya dk kama 12 eneo lote la kiungo akalichukua hali iliyopelekea Kili. Stars kuzinduka na kuanza kuishambulia Kenya kwa nguvu na kupelekea kupata penalt iliyofungwa Gadiel Maiko.
Niliangalia uchezaji wa Matogolo nikajiuliza hv Simba na Yanga siku zote hawamuoni huyu jamaa mpaka kwenda nje kununua wachezaji wa gharama kubwa wenye viwango vya kawaida? Uzuri wake sio kwenye kuuchezea mpira tu lakini hata umbo lake ni zuri kiuchezaji. Ni mrefu na ana nguvu. Ukiangalia maumbo ya wachezaji wa Uganda na Kenya Baraka ndie mtu sahihi anaeweza kupambana nao. Mpira wa kisasa unataka wachezaji wa namna hiyo . Nitashangaa sn km Baraka Matogolo hatoitwa tena timu ya Taifa.
Km Juma Mgunda angempa nafasi mapema na kuacha kukalili wachezaji tuliowazoea kuna kitu kikubwa huyu ajamaa angeisaidia timu yetu.
Sent using Jamii Forums mobile app