Barafu na ice cream | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barafu na ice cream

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Che Kalizozele, Jan 27, 2009.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Binafsi matumizi ya maneno haya unitatiza kidogo.Nilipokuwa Mwanza,barafu umaanisha zile rambaramba.Lakini nilipofika Dar,barafu umaanisha lile bonge la barafu la maji matupu ambalo wakazi wengi wa dar utumia kupozea maji ya kunywa huku ice cream ikichukua nafasi ya rambaramba.Ninachouliza,kuna maneno ya kiswahili yanayoweza kutofautisha vitu hivi viwili barafu bonge na ice cream,na ni lipi neno la kiswahili kwa ice cream
   
 2. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Barafu/ice ni maji (peke yake) yameganda wakati ice cream ni maji yamechanganywa na maziwa (au kitu kingine)
  Kimatumizi; barafu/ice unapoozea maji wakati ice cream wailamba yakhe ndio maana ice cream huku kwetu inaitwa lamba lamba.
  Lakini kule kwenu kwa kuwa mnalamba hata ice/barafu- basi zote (ice na ice cream) mwaziita lamba lamba.

  Maoni yangu.
   
 3. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ufafanuzi wako,naomba unipe neno la kiswahili la ice cream ili nipate kutofautisha vizuri maneno haya.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kuna barafu ambayo inatoka na uchanganyaji wa maziwa na maji na radha kidogo ya kahawa ama iriki ama maji na ukwaju, na inaweza kuongezwa rangi ili kuvutia inaitwa Malai.
   
 5. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu Kibunango kwa kunikumbusha.Kiini cha kuuliza swali hili ilikuwa malai.Neno hili nilisikia Zenj,nilipouliza vizuri jamaa akaniambia wazenj wanatumia maneno yote matatu,yaani barafu,malai na ice cream.Na akasema ukimsikia mzenj anasema ice cream ujue anamaanisha zile za bakhressa.Na hapo ndipo nikapa hamu yakutaka kujua neno la kiwsahili la ice cream
   
 6. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Mara nyingi husikia watoto wakisema ashikrimu wakitaka hizo lambalamba (wengine husema rambaramba hichi si kiswahili sahihi neno kuu ni Lamba na sio ramba)
  Lamba inamaana ya kula kutumia ulimi kwa mtindo wa kutembeza ulimi ama kinacholiwa kwa kupakaza ulimi.
  Baba Wa3 kuna maneno umeyatumia huwa yananichefua kidogo nikikutana na mtanzania mtumiaji wa kiswahili akiyatamka mfano
  unitatiza badala ya Hunitatiza (ukiacha ile herufi H basi maana inabadilika na kumtatiza msomaji/msikilizaji)
  vilevile kwa maneno "umaanisha" usahihi wake ni humaanisha.
  Mkuu kibunango hebu tizama/tazama maneno niliyoyatilia rangi uniambie yakoje masikioni mwa msikilizaji
  'Kuna barafu ambayo inatokana na uchanganyaji wa maziwa na maji na radha kidogo ya kahawa ama iriki ama maji na ukwaju, na inaweza kuongezwa rangi ili kuvutia inaitwa Malai.'

  lengo langu sio linginelo zaidi ya kutaka tujitahidi kutumia kiswahili vizuri zaidi kwa kadri tuwezavyo ili tuweze kuwafunza na wengine kiswahili kizuri.
   
 7. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nina hakika nitanyooka tu,usikate tamaa endelea kunielemisha.Lakini mkuu tatizo la msingi bado halijatatuliwa.Neno la kiswahili la ice cream,nilipokuona nikajua tayari swali limeshapata jibu kumbe bado.
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Sawa sawa tupo pamoja katika hilo.
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
   
  Last edited: Jan 27, 2009
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nakubali kiswahili yaweza itwa Lamba, lakini wauzaji walipokuwa wanapita wanasema Lamba Lamba, sasa ndio ikapatikana jina lamba lamba. Tukija kwa Maneno uliyomuuliza kibunango na kuyawekea rangi tofauti nadhani amekosea kuyaandika, mfano si "radha" bali ladha, pia si "iriki" bali iliki.

  Nilipokuwa shule ya msingi, dio nilianza kulisikia neno Malai (ice cream), toka kwa watoto wa kipemba.
   
 11. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Neno Malai nijuavyo mimi lina maana ya ule utando mazito unaopatikana kwenye maziwa baada ya kuchemshwa na kuwekwa yapoe, yakipowa hufanya utando juu kama ngozi fulani, huo utando ndio huitwa MALAI (cream).
  Pia kwa wale wenzetu wa pwani kwenye madafu kupatikana MALAI ya madafu ila haya sasa sio utando bali baada ya kunywa maji ya madafu basi kwenye fuu la dafu huwepo na uji mzito ambapo mara nyingine kama dafu limeanza kuelekea kuwa nasi basi MALAI yake huwa magumu zaidi na huweza kuwa kama nazi. basi huo ndio ufahamu wangu juu ya malai.
   
Loading...