Incredible Kim
Member
- Mar 10, 2021
- 35
- 39
Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi.
Huku kwa mataifa yetu tulitembea kifua mbele tukijua we have a Big brother. "What a proud moment to live" ilikua kama bahati kumshuhudia Rais wa kwanza wa Marekani kutoka kwa jamii ya watu weusi.
Alitukumbusha ndoto Maarufu ya Mwanaharakati Martin Luther King.
Ila sasa muhula wake wa kwanza ukapita muhula wa pili nao ukafuatia ukapita, akamaliza kipindi chake cha urais hata huko uraiani kama Rais mstaafu hatujaona kile ambacho tulikitegemea.
Mtu mweusi wa Marekani amebakia kua mtumwa, akiendelea kubaguliwa na kunyimwa haki nyingi kama raia wa Marekani.
Huku Afrika tumebaki tukipigana vita vyetu wenyewe kama ilivyokuwa kabla.
Juzi tu kama Tanzania, ilipopata msiba mkubwa, tulipata salamu za rambirambi kutoka kwa Malkia kwanza ila za Jirani yetu na ndugu yetu mjaluo Obama sikuziona. Kuna nukuu moja ya mpambanaji Samora Machel kama ntaikumbuka vizuri inasema "siku mtakayoona nikisifiwa na watu weupe msinipe siri zenu tena hata nikiwauliza maana nitakua nimeshawasaliti".
Nenda katembelee kwenye page zake za kijamii ni Rais anayependwa sana na kusifiwa na watu weupe. Kwa nafasi yake hakuna mtu mweusi anayeweza kuifikia kirahisi kwa miaka ya hivi karibuni ila mchango wake huwezi kuulinganisha na watu kama kina Malcom X, Martin Luther, Jesse Jackson pamoja na Mashujaa wetu wa Afrika kina Nyerere, Lumumba na wengine wengi waliopambana kutetea haki na utu wa mtu mweusi wa Marekani na Afrika. Anapoondoka anatuachia alama gani? Wamarekani weusi watamkumbuka kwa lipi sisi Waafrika tumkumbukeje?